Binti mmoja aitwaye Turi, ambaye ni yatima mwenye umri wa miaka 25, anayeishi na mama Yake wakufikia ambaye anaitwa Mama Vero, katika Kijiji cha Ndarimo.
Lakini, mama Vero upendo wote ameuelekeza kwa mwanaye Vero na kumuona Turi kama takataka, licha ya kuwa Turi ni msichana mwenye adabu na upendo kwa mama na mdogo wake wa kufikia,
ila,
juhudi zake zote zinachukuliwa kama mtu anayejipendekeza na kuitwa mnafiki na mama Yake wa kufikia!.
Maana ingawa Vero, alitambua wema wa dada Yake wa kufikia ambaye ni Turi,
Lakini, Mama huyo, kila alipomuona Vero akiwa karibu na Turi aliweka vipingamizi visivyo na sababu za msingi.
Siku moja, Mama Vero alimuita Turi kwa kufoka!, kama kawaida Yake tena muda huo huo, Turi akiwa amerudi kutoka Sokoni, na kusema,
"We Yatima, inamaana niliposema ununue na sabuni ya unga ya mia tano hujasikia au ndo kumekucha Bi.jeuri eeeh!, muone vile kama mtu!".
Lakini, Vero alikuwa na huruma ila tu mama Yake ndo shinikizo kubwa la yeye kumchukia Turi, Vero akamjibu Mama yake akisema,
" Mama ngoja tu niende Mimi, nisaidie dada".
Loooh!, ila jibu alilolitoa Mama Vero lilimliza mpaka Vero na Turi,
" Sikiliza na wewe mfuata bendera, wewe unamjua huyo , umezaliwa naye tumbo moja!?, Kwanza hana hata kitu kimoja kinachomuhusu humu, nashangaa mpaka leo anang'ang'ania hapa".
Vero huku machozi yakimtoka kwa mbali akasema,
" mamaaaa!, mbona maneno makali hivyo lakini!?",
Mama Vero akamkata jicho Vero kisha akasema,
" we we we ,tena funga bakuri lako na wewe,usijfanye kijukuu cha mtume hapa, ndo nishasema".
Baada ya mzozo huo, siku kadhaa zilipita, lakini, mateso ya Turi yalikua ni sehemu ya maisha yake, na mbaya zaidi,
mpaka Vero ambaye alikuwa na huruma kwa Turi naye alifuata tabia za mama Yake,
maana hata wahenga walisema kwamba "maji hufuata mkondo".
Lakini, chakushangaza!, siku moja Mama Vero alimuita Turi akiwa na bashasha na furaha kuriko kawaida,
mpaka Turi alihisi kitu,
maana hata kipindi Baba Yake Turi yuko hai, Mama huyo hakuwahi kumuonyesha tabasamu kama hilo!,
" Turi mwanangu uuu!, njoo mara moja Mama", Turi akamjibu Mama Yake ," abee mama nakuja!".
Turi akakimbia haraka haraka mpaka kwa mama huyo maana ndo maisha aliyozoea kuishi, na alipofika , Mama Vero akasema,
" Usikimbie mwanangu, tembea tu, utaumia bure!".
Kumbe!, bashasha hilo la Mama Vero halikuwa la bure, alikuwa na jambo lake moyoni alilolipanga!, akasema,
, " Mwanangu Turi, nisikilize Kwa makini, Baba Yako kabla hajafariki aliniachia usia kwamba, nikulee na nikutunze mpaka ukipata mume wa kukuoa,
Lakini, si mume tu ilimradi mume bali nimchunguze, kwahiyo, kuna tajiri mkubwa Sana atakuja kukuchumbia kesho, hii ndio fursa kwako mwanangu, mmh! mmh!".
Turi, kwa sababu alichoka maisha ya manyanyaso na mateso aliyokuwa akiishi na mama huyo, hakupinga wazo hilo, tena alipokea kwa furaha, akiamini wenda ndo ingekuwa nafuu kwake, akasema,
" Aaha!, nashukuru Mama kwa kunisaidia katika Jambo hilo nashukuru Sana Yani!", Mama Vero naye akajibu akisema ,
" usijali mwanangu,huo ni wajibu wangu nikiwa kama Mama yako kipenzi".
Siku iliyofuata asubuhi na mapema, Turi akiwa chumbani kwake, mara akasikia mlango wa chumba ukigongwa,
alipofungua Kumbe alikuwa ni mama Yake wa kufikia ambaye alikuwa na furaha isiyo ya kawaida na kumwambia Turi kwamba,
" Turi mwanangu jiandae haraka ,mchumba wako ameshafika yuko nje, jitahidi ujiandae haraka, jipodoe vizuri mrembo wangu"
Turi naye kwa bashasha akasema," Sawa Mama ngoja nijiandae haraka haraka,sasa hivi nakuja".
Lakini, chakushangaza!, Baada ya mama Vero kutoka kidogo nje ya mlangoni wa chumba cha Turi...!,
ITAENDELEA...,
#simulizi #storytelling #story.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments