BETWEEN SISTERS AND SECRET Chapter 17 "Mama G anatupenda wote pale dukani acha story zako za kutunga." Mia alijilaza kitandani.
" Sawa kama hutaki kuamini."
Kwa upande wa Gael, Gian na Gavin wallenda kumtembelea.
*Tumesikia unaumwa na hukwenda ofisini leo," Ni mafua tu kidogo, nimetumia dawa mpaka kesho nitakuwa sawa." Gael alikuwa na huzuni.
"Mbona umepoa hivyo kama unaumwa sana tukupeleke hospital." alisema Gavin.
Hapana kaka nipo sawa, ni moyo wangu tu unanisumbua. Gael aliweka mkono wake mmoja kifuani.
Nitampigia simu doctor Enosh aje haraka kukufanyia vipimo." Gian alitoa simu. Gavin alianza kucheka.
Dogo unazingua, huyu haumwi ni mapenzi
yanamsumbua." alisema Gavin.
"Ni yule mwanamke tena? Kwanini unapoteza muda wako kwa mwanamke mwenye tabia za
ajabu kama Mira? Tayari unajua ukweli kuwa anakudanganya lakini bado umemn'gan'gania sijui amekuroga." aliongea Gian kwa hasira.
Sio Mira, ni Mia anautesa moyo wangu." aliongea Gael kwa huzuni.
"Unampenda kweli au unamtafuta sehemu ya kumsahau Mira?" Gian alimuuliza Gael.
"Nampenda kweli sio utani, nilimpenda zamani tu sema sikuwa naelewa kama nampenda kama
rafiki au nahitaji kuwa nae zaidi ya urafiki."
"Basi mwambie ukweli wa jinsi unavyojisikia juu yake." alisema Gian.
"Amenitolea nje hataki kabisa kusikia hizo
habari." Usikate tamaa, ongea nae tena kwa mara
nyingine huenda akakuelewa, na kabla ya kuwa na Mia hakikisha umeshaachana rasmi na Mira,
la sivyo sitokuruhusu uwe na Mia." aliongea Gian akiwa yupo serious,
Okay hilo sio jambo kubwa, nitajitahidi anielewe,"
"Utaongea nae vizuri lini?" aliuliza Gavin. "Hata sijui ila nitaongea nae."
alitoa simu akampigia Mia.
"Acha kupoteza muda, ngoja nikusaidie." Gavin
"Gavin... mbona anapiga usiku? Kuna nini?" Mia alijiuliza maswali alimua kupokea simu.
Mia njoo haraka sana nyumbani kwa Gael, amezidiwa sana tafadhali naomba ufike hapa
haraka, amekuwa akitaja jina lako tu." "Sawa nitakuja sasa hivi." Mia alivaa haraka
akatoka akakodi tax mpaka nyumbani kwa Gael.
"Gael anaendeleaje?" Mia alimuuliza Gavin na Gian.
"Amepumzika kidogo lakini hali yake sio nzuri
kabisa. alidanganya Gavin.
"Naweza kwenda kumuona?" aliuliza Mia. Ndiyo, ingia tu hapo chumbani kwake. Gian alimuonyesha Mia chumba cha Gael.
Mia aliingia chumbani alimkuta Gael amelala kitandani.
Gael upo sawa?" Mia alimgusa Gael kwenye paji la uso kumpima joto.
"Naumwa Mia... naumwa sana." Gael aliushika mkono wa Mia.
Gael umeanza tena na umesema unaumwa, kama ndo hivyo mimi naondoka." Mia alitoa mkono wake kwenye mikono ya Gael alisimama
aondoke, Gael akamkumbatia kwa nyuma.
"Usiniache Mia, sikufikiria siku moja nitakuwa hivi, nimekutana na watu wengi, wanawake wengi wazuri... lakini hakuna hata mmoja
aliyewahi kunifanya nihisi namna ninavyojihisi
nikiwa karibu na wewe. Upole wako, uaminifu wako, hata jinsi unavyocheka kwa aibu, hayo yote yananifanya nikuone upo tofauti na wanawake wengine."
Nakubali huenda unaniona nipo hivyo lakini mimi sitaki kuwa karibu na wewe, natamani
tuendelee kuwa marafiki lakini siwezi tena, naomba uniachie niondoke. Mia alianza kumsukuma Gael.
Mia sikuachii, huwezi kuondoka saizi muda umeenda sana sitokaa kwa amani ukiondoka,
vipi kama kitu kibaya kikikukuta njiani?" Gael unajua kama unanipa wakati mgumu?"
Macho ya Mia yalianza kulengwa na machozi. "Kivipi?" Gael alimgeuza Mia upande wake.
Vipi kama nikiishia kukupenda watu watanichukuliaje? Sitaki historia ijirudie tena... naogopa sana. Mia alianza kulia.
Shhhh, usilie, sipendi kukuona unalia, unauumiza moyo wangu Mia na nikuhakikishie
tu siwezi kukuacha na nitakuwa upande wako maisha yangu yote." Gael alifuta machozi yaliyoteremka kwenye mashavu ya Mia.
"Muongo na vipi kuhusu Mira?"
Tumeshaongea kuhusu Mir kufupi ni kama tumeshaa wasiwasi Gael alimuuta Mia
Gavin na Gian walichunguli
aliwape ishara weandoke
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni