BETWEEN SISTERS AND SECRET Chapter 10 Gael alinyanyua glass yake, akanywa pombe yote kwa mkupuo. "Babe, naenda toilet mara moja." Mira aliondoka.
Wakati anatoka chooni, alivutwa kwenye giza na mtu.
"Wewe ni nani? Kwanini unanishika hivi bila ruksa yangu? Na unataka nini kutoka kwangu?" Mira alimsukuma yule mwanaume.
"Kwahiyo yule ndo bwana ako mpya?” aliuliza yule mwanaume, sauti yake ikiwa imejaa hasira.
"Joel..." aliita Mira kwa mshangao.
"Ndiyo, ni mimi, hujakosea hata kidogo. Au ulidhani nimekufa?" Joel alimvuta Mira akamkumbatia.
Joel, acha bhana, ngoja niende, nitakupigia baadaye, Mira aliitoa mikono ya Joel kwenye kiuno chake.
"Nakuacha uondoke, ila nakupa onyo ole wako usinitafute, nitakuharibia kwa huyo boya wako.
Nadhani unanijua vizuri," Joel alimtishia Mira. "Najua siwezi kukuangusha, nitakutafuta tu,"
Mira alimkiss Joel kwenye shavu akaondoka.
"Nilitaka kukufuata, mbona umechukua muda mrefu?" aliuliza Gael.
"Aaah, tumbo kidogo halipo sawa, nataka kurudi nyumbani," Mira aliongea huku amejilaza kwenye kifua cha Gael.
'Pole sweetheart, basi twende hospitali."
"Nope, nataka tu kwenda nyumbani. Nina dawa
zangu, nikimeza nitakuwa sawa. "Okay, twende, Gael alimshika mkono Mira wakatoka nje.
Joel aliwasindikiza kwa macho.
"Mmmh, enjoy kwa sasa ila Mira ni wa kwangu, na yeye analijua hilo, Joel aliongea huku anaiminya glass iliyojaa pombe.
Baada tu ya Mira kufika kwenye nyumba aliyojengewa na Gael, alitoa simu yake akampigia Joel.
"Niambie mrembo, umeshamaliza kudeka kwa huyo mshamba wako?” aliuliza Joel. "Joel, hebu tueachane na hayo mambo, niambie
umehamia lini Dar es Salaam?"
"Mbona nipo siku nyingi, nina kama mwaka hivi."
"Kumbe upo Dar es Salaam na hukuniambia jamani!" Mira aliongea kwa kulalamika.
"Ningekwambia vipi na ulitaka tuachane."
"Zile zilikuwa ni hasira tu, Joel. Mimi
nimekumiss mwenzio."
"Hata mimi nimekumiss pia."
"Basi nakutumia location, uje nyumbani kwangu sasa hivi," Mira alikata simu huku anatabasamu.
Alimtumia Joel message: "Nilijua tu bado
ananipenda, hao wengine ni wapita njia." Joel alilipia kinywaji chake, kisha alichukua
pikipiki yake na kuelekea nyumbani kwa Mira.
"I miss you, darling," Mira alienda kumkumbatia
Joel, walianza kukiss.
Joel alimbeba Mira, wakaenda chumbani.
Asubuhi Mira aliamka akiwa kwenye kifua cha Joel.
"Simu yako ilikuwa inaita sana, hebu angalia ni nani, ananipotezea usingizi wangu, aliongea Joel kwa sauti iliyojaa uchovu.
"Sorry babe, endelea kulala, ngoja niangalie," Mira alimkiss Joel, alichukua simu yake
akaangalia mpigaji alikuwa ni Gael.
"Anataka nini asubuhi asubuhi huyu naye," Mira
alitaka kumtumia message Gael, Joel alimvuta akamkumbatia kwa nguvu.
Sasa upo na mimi, sitaki umuwaze hata kwa dakika moja," aliongea Joel huku anamkiss Mira
kila kona.
Mira alitabasamu, akasahau kabisa kuhusu Gael.
"Simu zangu hapokei, na message zangu pia hajibu, atakuwa amepatwa na nini?" Gael alipata wasiwasi.
"Doto, nina ratiba gani sasa hivi?" aliuliza Gael kwa secretary wake.
"Una kikao na wafanyakazi wote, boss, alijibu Doto.
"Aaah, okay, twende kwenye kikao."
Gael aliingia kwenye kikao lakini akili yake yote ilikuwa kwa Mira.
Kwa upande wa Mira na Joel, walilala mpaka saa 3 asubuhi..
"Mira, hebu amka uondoke, unatakiwa kuwahi
kazini, Joel alimuamsha.
Kwanini hukuniamsha? Natakiwa kuwa kazini Joel, ona sasa nilivyochelewa!" Mira alijiandaa haraka, alifika kazini mida ya saa nne na nusu.
"Mira, Mr. Gael alikuulizia sana leo, hata kwenye
kikao hukuwepo. Ulikuwa wapi?" alisema
Mwaija, mfanyakazi mwenzie na Mira. "Nitaenda ofisini kwake, na mengine
hayakuhusu," Mira alimuangalia vibaya Mwaija, akaingia ofisini kwa Gael. "Unaingia ofisini sasa hivi? Na kwanini simu
zangu hukupokea?" Gael alimuuliza Mira akiwa serious.
"Babe, kwani hujui jana uliniacha na hali gani jamani?" Mira alienda kumkumbatia Gael.
"Pole kwa kuumwa, lakini kwanini hukupokea simu zangu wala message hukujibu? Unajua ni kiasi gani ulinipa wasiwasi?"
"Nisamehe babe, nililala usingizi mzito baada ya kumeza zile dawa."
"Okay, kaendelee na kazi, baadaye tutaongea vizuri."
Mira alimkumbatia Gael kwa mapenzi yote, lakini nyuma yake alimzomea kimoyomoyo.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni