BETWEEN SISTERS AND SECRET Chapter 5 "Samahani sana... ni kosa langu nitarekebisha sasa hivi na nitakupatia risiti, ungependa
kuangalia simu ipi?" Mia alimuuliza yule kaka.
"Muoneni yule kwani hajui kama yule ni mtoto
wa mama G?" aliuliza Dora, "Angemjulia wapi na yeye ndo kwanza mgeni,"
alisema Judith.
"Samahani Mr. Gael, huyu ni mfanyakazi mpya ndomana hakufahamu na kazi bado haimudu
vizuri," Furaha aliongea huku akicheka cheka. "Oh kumbe." Gael alimuangalia sana Mia kana
kwamba alijaribu kumuelewa kitu.
"Samahani boss, nitajitahidi kufanya vizuri," Mia aliongea huku anatetemeka, aliogopa sana
kufukuzwa kazi. "Usiwe na haraka ya kuomba msamaha. Jifunze
kuwa makini kwanza, na kingine mimi sio boss wako. Jina lako nani?" Gael alimuuliza.
"Mia... jina langu ni Mia," alijibu kwa kigugumizi. "Kuna mtu nakufananisha nae..." Gael alimuangalia kwa makini, Mia akaangalia chini
kwa aibu. "Okay, achana na hilo. Karibu sana," alisema
Gael.
"Asante..." Mia alijibu kwa sauti ya chini. Gael alimuangalia kwa mara ya mwisho kisha akaondoka.
Gael Maximilian ni kijana wa miaka 28, mtanashati na mtoto wa pili kwenye familia ya Bi Helen (maarufu kama Mama G) na Mr. Maximilian. Yeye ni mmiliki na CEO wa kampuni ya Purenex Company.
"Mia, uwe makini. Unatakiwa kutoa risiti kila unapo muhudumia mteja, na una bahati sio mama G aliyekukuta," alisema Furaha. "Nitakuwa makini," Mia alijibu huku akiketi.
Kila mmoja alirudi kwenye nafasi yake. Ghafla mlango ulifunguliwa, aliingia Gael tena akiwa na
mwanamke mzuri. "Nimerudi tena, nataka umsaidie mchumba
wangu kuchagua simu, Gael alimwambia Mia. Mia alibaki kumshangaa yule mwanamke, hata Furaha alishtuka.
"Huyu si ni Mira?" Mia alijiuliza kimoyomoyo. Mira alimuonyesha Mia ishara ya kunyamaza kama hamjui. Hata Furaha aliona kitendo hicho. "Mia, naongea na wewe!" Gael alimshtua. "Abee... aah sawa boss, nitamchagulia simu nzuri," Mia aliongea huku anatetemeka. Hakuamini kama angemkuta Mira Dar es Salaam, wakati alimuacha Morogoro.
Mia alipendekeza simu kwa ajili ya Mira. "Napendekeza simu hii, ni nzuri na ina uwezo mkubwa sana," alisema Mia. Gael allichukua, akaikagua.
"Unaionaje hii, sweetie?" Gael alimuuliza Mira. "Nimeipenda sana babe," Mira aliongea kwa madeko huku akiegemea kwenye bega la Gael bila aibu.
"Tutachukua hii... ila usisahau kutoa risiti," Gael alisema huku anatabasamu, akimchokoza Mia.
"Sawa boss," Mia alijibu. Gael alifanya malipo, Mia akawakabidhi simu pamoja na risiti.
"Asante babe..." Mira alimkiss Gael shavuni. "Nipo hapa muda wote kwa ajili yako, Gael alijibu kwa upole. Wakaondoka.
"Mia, yule ni Mira si ndio?" Furaha alimfuata haraka.
"Ndiyo, ni yeye kabisa. Alinizuia hata nisiseme kama yeye ni dada yangu," Mia aliongea huku machozi yakimtoka.
"Usilie kipenzi, kwani hujamzoea Mira alivyo na mashauzi?" Furaha alimkumbatia.
Mida ya jioni wakati wa kufunga duka, Mira alimfuata Mia.
"Nataka kuongea na wewe," Mira alimvuta Mia. "Unampeleka wapi? Ongea nae hapa hapa,"
Furaha aliuvuta mkono wa Mia. Mira alimuangalia Furaha kwa dharau.
"Wewe kama nani unaingilia mambo yangu na
Mia?" aliuliza kwa kiburi. "Mimi..." Furaha alitaka kujibu lakini Mia
akamzuia.
"Acha Furaha, nitaenda nae. Nataka nijue ataniambia nini."
Mia aliongozana na Mira.
"Sitaki mtu yoyote ajue kama mimi na wewe ni ndugu, hasa hasa mpenzi wangu Gael..." Mira aliongea kwa sauti ya chini.
"Mira, yani umeamua kufika huko-kuuvunja undugu wetu wa damu kisa watu wa nje?" Mia aliongea kwa uchungu.
"Embuu kaa kimya wewe! Undugu wenyewe upi
hapo? Na umwambie yule kibwengo mwenzio mimi sio level yenu tena. Mfunge hiyo midomo yenu, sitaki... tena sitaki mtu yoyote ajue kama
mimi na wewe ni ndugu!" Mira aliongea huku ameshika kiuno.
"Sawa, hakuna shida. Kama umeamua kuuvunja undugu kabisa... lakini vipi kuhusu baba? Anajua chochote kuhusu wewe kuwa Dar es Salaam na
sio Morogoro?" Mia aliuliza huku anafuta machozi
"Hayo hayakuhusu. Nitamwambia baba kwa muda wangu, na ukumbuke nilichokwambia," Mira alisema huku anamnyooshea Mia kidole. "Sawa, kwanzia leo mimi na wewe hatujuani, kama ulivyosema," Mia aliongea huku machozi yakimtoka.
"Vizuri." Mira alimpiga kikumbo Mia kisha akaondoka.
Mia alikaa chini akalia kwa uchungu.
"Mia, upo sawa?" Furaha alienda kumnyanyua. "Nipo sawa," Mia alidanganya.
"Hapana, haupo sawa. Niambie kila kitu alichokuambia yule mchawi. Dora na Judith wametangulia nyumbani, usijali." "Usimuite mchawi bhana, yule ni dada yangu
ujue"
"Anatofauti gani na mchawi? Tangia tukiwa Form Four alikufanyia kila hila, na kukuonea. Mpaka leo bado anaendelea kukuumiza. Furaha
aliongea kwa hasira.
"Amesema hataki mtu yoyote ajue kama sisi ni ndugu, na wewe pia hataki useme kwa yoyote kama mimi na Mira ni ndugu, hasa hasa kwa
mpenzi wake Gael." "Looh! Msichana ana balaa yule. Kwa hiyo anaona bora mapenzi kuliko undugu. Na Mr.
Gael wa watu alivyo mtaratibu na mu-handsome vile! Ilikuwaje akaenda kuanguka kwa Mira? Mbona kazi anayo! Bora hata angempenda. mrembo wangu Mia," Furaha alimtania Mia.
Full 1000
Whatsp
0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni