BETWEEN SISTERS AND SECRET Chapter 13 Gael alimuangalia Mia kila mara na kutabasamu,
alimrudisha nyumbani na yeye akaondoka. "Bibie ndo unarudi saizi, umekosa mambo
mazuri, alisema Dora.
"Mambo gani hayo?" aliuliza Mia.
"Mpenzi wake na Judith alituletea biriani na
chips," Dora alimtambia Mia. "Asikudanganye, hakuna mtu yoyote aliyekuja hapa leo," alisema Judith.
"Aaah kwanini unaharibu mchezo, nilitaka tu aseme alienda wapi na boss Gael, Dora
alikasirika.
"Kumbe hiyo ndo michezo yenu! Tulienda tu
kituo cha yatima kule Tumaini na baada ya hapo
ndo akanirudisha nyumbani." Wote walimcheka Dora.
"Mia, leo tunatoka! Tunaenda club usiku,"
alisema Judith huku anatabasamu.
"Sawa, hata mimi nitaenda, nataka kuona hizo starehe za club mnazozisema kila mara, alijibu
Mia huku akicheka kwa aibu kidogo.
"Okay basi, tuchague nguo kabisa za kuvaa club," alisema Dora.
Ilipofika saa tatu usiku, walifika kwenye club ya Blue Heaven C mahali palipojaa muziki, taa za rangi, na sauti za watu.
Kwa upande wa Mia, huo ulikuwa usiku wa
kwanza kabisa kwenda club.
Baada ya kama dakika kumi, alimuona Mira akiingia na Joel huku wameshikana mikono. Mia alishtuka, alisimama kwa mshangao.
"Yule si Mira," alisema Mia. "Ndiyo... ni yeye kweli tena yupo na Joel," alijibu
Furaha. "Sitaki kuamini anatoka na Joel tena na ni
mpenzi wa Gael."
"Kwahiyo unataka kusema yule kaka ni mpenzi wa Mira wa zamani?" Dora alimuuliza Mia.
"Ndiyo, na Mira ni dada yangu," alisema Mia.
Siku ya sherehe ya kufunga mwaka ilifika kama kawaida, wafanyakazi wote walialikwa.
"Mia unachelewa chelewa nini, fanya haraka basi," alisema Furaha. "Natoka jamani, Mia alitoka taratibu akiwa
amevalia gauni la blue refu lililompendeza sana. "Hili gauni naona kama limenibana, na viatu virefu hata sijazoea mwenzenu," Mia aliongea
kwa kulalamika.
"Ona ulivyopendeza, usitake kuniambia unataka kubadilisha?" aliuliza Furaha.
"Nataka kuvaa kawaida."
"Ukienda huko utajiona wewe peke yako upo tofauti, vumilia kwa leo tu."
Judith na Furaha walimshika mkono, walipanda tax.
"Hapa ndo nyumbani kwa Mama G?" aliuliza Mia. "Ndiyo, umeona palivyo pazuri na pakubwa."
"Kama hoteli vile, ila kuna watu wanaishi jamani!" Mia alishangaa, kila kona kulikuwa kumepambwa vizuri.
"Njoo nikuonyeshe sasa shoga yangu."
"Unionyeshe nini?" Mia alimfuata Furaha.
"Umewaona wale pale wakaka wawili waliokaa meza moja na Mr Gael?"
"Ndiyo, ni kina nani?" aliuliza Mia.
"Yule pale sasa ndo Gavin, mtoto mkubwa wa
Mama G, na yule pale ndo Gian, mtoto wake wa mwisho. Umeona walivyo ma-handsome, wanawake wanawashobokea kama nini! Mimi nampendaga Gavin, anaonekana ni mpole,"
Furaha aliongea huku anacheka cheka. "Mmmh shoga yangu huishiwi vituko, haya nimeshawaona, twende tukakae."
Mia na Furaha walienda kukaa.
Sherehe iliendelea, muda wa kucheza muziki
ulipofika, Mia alimuona Gael anacheza na Mira.
"Kumbe amekuja kwenye sherehe pia, sikumuona mwanzo, sijui ametokea wapi."
"Kwanini anajipendekeza kwenye familia ya Mr Maximilian na wote hawamtaki?"
"Amekosa haya na anaonekana anatamaa ya pesa, ndomana haoni ajabu kutukanwa na
kufukuzwa. Nani anataka mka-mwana mwenye
tabia za ajabu kama Mira?"
Yalikuwa ni maneno ya wafanyakazi wenzie na Mira.
Yale maneno yalimuumiza sana Mia, alitamani kuongea lakini alijizuia.
"Furaha, naenda msalani mara moja."
"Usichelewe kurudi, Furaha aliendelea kucheza.
muziki.
"Sijui nimefikaje hapa, mbona kama nimepotea," Mia aliangalia huku na huku.
"Mambo mrembo, Gian alimsalimia Mia. "Poa, samahani, msalani ni wapi? Mia
alimuuliza Gian. "Aaah ni mbali sana, unaweza kuchukua hata
nusu saa kufika, Gian alimchokoza Mia.
"Sasa itakuwaje? Namaaanisha ni wapi,
unaweza kunielekeza au kunipeleka labda?"
"Ndiyo bila shaka, lakini mpaka unilipe," Gian
aliongea huku anatabasamu. Mia alifungua pochi yake, ilikuwa na elfu moja
tu.
"Sawa, nipeleke, nitakulipa," aliongea Mia huku
anatabasamu.
"Unaahidi?" aliuliza Gian.
"Ndiyo, naahidi."
Gian aliongoza mbele, Mia alimfuata nyuma.
Hawakuchukua hata dakika mbili walifika.
"Ndiyo, kwani huoni hiyo alama?" Gian alimuonyesha Mia mlangoni.
"Hapa ndo msalani?' aliuliza Mia.
"Sawa, asantee. Mia alitaka kuingia, Gian
Sawa, asantee. Mia alitaka kuingia
"Oh, nilitaka kusahau, subiri kidoga alifungua pochi yake, alitoa mia tano, al
kwenye mkono wa Gian. "Hii ni nini? Gjan alimuuliza Mia
akamzuia. "Malipo yangu yako wapi?
"Malipo yako, au ulitaka nikulipe nini?" "Sitaki pesa, nataka kucheza Gian aliongea huku anatabasamu. wewe
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni