BETWEEN SISTERS AND SECRET Chapter 20
Mira aliongea huku amekunja mikono yake kwa hasira, Joel akamtazama akatingisha kichwa.
Kesho yake asubuhi, Mira alimfuata Gael ofisini kwake.
"Ni adabu za wapi hizo unaingia tu ofisini kwa boss wako bila ruksa wala kubisha hodi?" Gael aliongea huku amekunja sura.
"Babe kwanini upo hivyo kama umekasirika kwa kilichotokea kati yangu na ex wangu? Ilikuwa ni bahati mbaya tu, na hata wewe pia ulinilipizia ulilala na mfanyakazi wa mama yako. Tufanye tu yameisha, Mira alijitetea, akijaribu kumkumbatia Gael.
Gael akarmsukuma.
"Nilikupenda sana Mira, nilikuwa nipo radhi kugombana na kila mtu hata familia yangu kukulinda. Lakini hustahili tena penzi langu. Kwa sasa nampenda sana Mia, na yeye ndiyo mwanamke wa ndoto zangu."
"Gael huwezi kuniacha mimi kirahisi hivyo. Umenipotezea muda wangu halafu uniache? Haiwezekani!" Mira alipaza sauti.
"Unachekesha sana. Hapa aliyempotezea muda mwenzie ni wewe, na siyo mimi. Toka kwenye ofisi yangu kabla sijakudhalilisha mbele ya kila mtu!" Gael alifoka.
Mira akaondoka.
"Mia usijione mshindi. Nikimkosa Gael hautaweza kumpata pia," Mira alicheka kisha akaondoka, akaelekea kwenye duka la Mama G.
Mara alipomwona Mia, akaanza kumvuta nywele.
"Mira unaniumiza!" Mia alilalamika.
"Haya maumivu unayoyapata ni kidogo kuliko yale ninayoyapata mimi kwa kumkosa Gael,"
Mira aliendelea kumvuta nywele.
"Niachie inatosha, siwezi kuwa mnyonge kila siku!" Mia alimsukuma Mira akaanguka chini. "Umethubutu vipi kunisukuma? Kumbe umenisahau!" Mira alitaka kumvamia Mia, Furaha akamzuia.
"Dada taratibu tena ukome. Umemuona mtoto anavyoita kisura baby face, ngozi laini kama ya katoto kachanga. Unataka kumvimbisha mwenzio, umtie nuksi kwa kosa lako mwenyewe? Nani aliyekutuma ukamsaliti mpenzi wako tena na ex wako? Loooh, yani unarudia matapishil" Furaha aliongea huku ameshika kiuno.
"Bila haya akaenda kupasha viporo, na chakula kilichotokea jikoni kipo mezani," Dora aliongea huku anampandisha na kumshusha Mira.
"Hahah! Kwahiyo umeungana na hawa makahaba wenzio kunishambulia? Umesahau kabisa kama mimi ni dada yako?" Mira aliendelea.
"Kwanza tuheshimiane Mira. Nilikuheshimu sana lakini hukuijali heshima yangu kwako. Na leo iwe mwanzo na mwisho kuniita mimi kahaba. Wewe ndiyo kahaba mzoefu!" Mia aliongea kwa kujiamini mbele ya Mira kwa mara ya kwanza.
"Unasemaje wewe?" Mira alitaka kumvamia Mia,
Furaha na Dora wakamzuia. "Usitufanyie fujo, ondoka haraka sanal" walimwambia,
"Mia tutaonana tu mimi na wewe, hili halijaisha bado!" Mira aliokota pochi yake akaondoka kwa hasira.
Mia alikaa chini kama mzigo.
"Vipi mwenzetu, ndiyo presha imepanda?" Furaha alimtania Mia.
"Ata siyo hivyo.." Mia alijibu..
"Sasa ni vipi? Lakini hata usiwaze shoga angu, kila kitu kitakuwa sawa," alisema Judith.
"Hakuna kitakachokuwa sawa. Sikuwahi kufikiria hata siku moja kama nitakuja kugombana na dada yangu kipenzi kisa mwanaume. Sijui baba atalichukuliaje hili akisikia watoto wake wanagombania mwanaume," machozi yalianza kutoka kwenye macho ya Mia.
"Najua ni ngumu lakini Mira ndiyo mwenye makosa hapo," Furaha alisema.
"Hata mimi nimefanya makosa makubwa sana. Kwanini nilikubali kuwa rafiki kwa Gael, na kwanini sikumwambia ukweli kama mimi na Mira ni ndugu tena wa baba mmoja na mama mmoja," Mia aliongea kwa uchungu.
"Sasa wewe unaamua vipi hapo?" aliuliza Furaha.
"Sitaki kugombana na yoyote wala sitaki kusema uongo kwa mara nyingine. Nataka kumaliza hili." "Utalimaliza vipi?"
"Nataka kukaa mbali na Gael, na nataka kumuomba msamaha Mira. Hatuwezi kuvunja undugu kisa mwanaume. Yeye ni mtu, baki tu kwetu," Mia alifuta machozi akasimama.
"Mmmh, uamuzi ni wako. Sisi hatuwezi kusema umeamua vibaya au vizuri. Ila nakuomba ufikirie vizuri kabla ya kufanya hivyo," Furaha alimshauri.
"Asanteni kwa kunijali. Nyie ni marafiki wazuri sana. Hili nitalimaliza mwenyewe," Mia alisema.
Kila mmoja akarudi kwenye kazi yake.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni