MWANDISHI ::HURU MEDIA
Masha akabaki kufikiria kwa sec, msaidizi wa Mr Alberto akahisi kama hajatoa maelezo yanayo faaa
Akamwambia tena
" Naitwa Rahul ni Msaidizi wa Mr Alberto ,Anaomba Radhi kwa...."
"Haina hajaa mwambie nimemsamehee lakini Kwa..yaan lazima police wajue " masha akaanza kulia
Rahul akamchukua haraka akamuweka ndani ya gari akaanza kuongea nae sasa kwa utulivu huku anamuombea samahani Boss wake akamsihi sana masha asiende huko kumshtaki
Rahul akamwambia Masha Alberto anasumbuliwa na ugonjwa wa hisia humkuta mara chache sana kwa miaka na hiyo ndio kama Tiba yake
Masha akasema napata faida gani kama nisipo kwenda kushtakii??
Rahul akamwambia nimepewa Kibali cha kukupa kila kitu unachohitaji nitakuhudumia chochote kile utalipwa kiasi kikubwa cha pesa na kila kitu ...
Masha akatabasam kwa mbali hakuonesha kwa rahul akasema moyoni asante mungu mbona kirahisi sanaa hivii
Akakubali akamwambia Rahul sawa nimekuelewa ukienda kinyume takwenda kukushtaki police nyie wote na huyo Sijui Alberto yupo wapi
Rahul akamwambia amerudi nyumbani mara moja atachukua muda kidogo kuja tena huku Tanzania ...
Wakati Rahul anaondoa gari hapo , ndio muda ambao Vicky alikuwa anatoka ndani ya hotel taratibu anajikokota kuondoka hapo
Tumbo lake lilikuwa linamaumivu sana miguu yake inatetemeka bila hata kujua kuwa masha ametembelea shida yake , akaondoka kwenda nyumbani kwao, hata hamu ya kwenda chuo hakuwa nayo
Alifika akalala tumbo linamuuma sana alilia mnoo
Alilia mpaka usingizi ukampitia hakuwahi kuwaza et ipo siku atabakwa tena ndani ya Hotel kubwa kama ile hotel ya nyota tano aliyoamini hapo hakuna wahuni kuna watu wenye hadhi sana
Vicky aliamka jioni baada ya kusikia makelele yamekuwa mengiii , masha ndo amerudi na mizigo kibaooo
Inashushwa kwenye tax
Vicky akabaki kushangaa tena imejuwajee
, akamwambia we Vicky changamka bwanaa embu katoe vitu kwenye gari hukoo afu mbona kama unalia vipiii??
Vicky akamwambia mie nipo sawa tu mbonaa
Mama masha akamwambia huyu leo hajaenda chuo na karudi hayupo sawa anaumwa ,Vicky nenda kapumzike "
"Hee mama akapumzikeeee??? Halafu nani anashusha vituuu??? "
Masha akafoka yaan swala la vicky kwenda kupumzika kwake ilikuwa kama keroo
"Mashaaa!! Mbona upo hivyoo , Vicky nenda nitabeba mimi"
" mamaaa!! Acheni nitavirudisha majitu nataka kuyaokoa na njaa yanajishaua aah sipendi yaaan wewe mtu mzima ufanye kazi wakati kijana yupo achaa nitavirudishaa"
Vicky akashangaa kwani masha anashida gani akasema basi isiwe shida mie nitabeba hata usijali masha,
Masha akamwambia ndo ubebe sio utabeba bado umesimama sehemu mojaa "
Vicky akaenda kushusha mizigo analeta ndani hivyo hivyo alikuwa anaumia sana bado alikuwa na maumivu chini ya tumbo..
"Mamaa kuanzia leo mie sintaishi hapa tenaa ila nitakuwa nakuja kuwaona "
"Enhee unaenda wapi tena , masha huishiwi matatizo mwanangu"
"Mamaa safari hii sio matatizo embu ogeni twende niwapeleke kwangu halafu nitawaambia , we Vicky embu jiandae ,Gloria Yupo wapi mamaaa??"
Groly ni mtoto wa masha ambae alimzaa akiwa Chuo mwaka wa kwanza ,,, mama Yake akamuuliza unataka ukaishi nae huku kusiko julikana
Masha akasema akaaa!! Niende nae wapiii atabaki hapa hapaa ukimshindwa ataenda kwa baba yake ...
Vicky akainuka zake akaingia ndani , Masha akamfata
"We vipii unaumwa??"
Vicky akasema ndio akamuuliza umefanya nini nambie ukwelii unaonekana kabisa haupo sawa , Vicky akaanza kulia aliliaa kwelii
Akamwambia masha mie leo nimebakwa masha alishtuka akasema mungu wangu na nanii??
Vicky akasema simjui hata ni mtu wa aina gani??
"Hukumuona??" Masha akamuuliza huku anakaa sawa
"Mashaa , naumiaa"
"Embu nielezee ilivyokuwa mwanzo hadi mwisho, ujue mie pale nilijua mama anakutetea tu kama kawaida yake palee!!"
Vicky akaelezea mwanzo mpaka mwisho tukio lilivyokuwa
"Mungu wangu kwahiyo sura yake huikumbukii??"
"Sijaiona hata wala sikuwa makini nayo , lakini nimesikia hicho chumba amelala tajiri sijui kutoka Los angels , mie nataka nikamshtaki tu itajulikana huko huko"
"Eeh mungu , we unaamini Tajiri akubake wewe kwa lipi shoga angu ulilo nalo et?? , hahaha yaan wewe unachekesha aisee "
Vicky anataka apate faraja masha ndo kwanza alicheka mpaka akashika na mdomo
"Sikia nikwambie Vicky usiende police kwanza mie nitakutafutia mtu aliekufanyia ujinga na tutamfunga sawa ,Nimepata mwanaume anahela sana tutamtumia huyoo"
"Nashukuru masha asante sanaa"
"Hayaa jiandae twende ukapaone kwangu"
ITAENDELEA...
KWETU morogoro.