SEHEM YA 08
MWANDISHI ::HURU MEDIA
Baada ya vipimo kuisha Rahul akamuomba Vicky wakapate chakula pamoja , Vicky hakuwa na shida na hilo lakini swala la Rahul amtegemee kwenye matatizo yake hata halikumuingia akilini
Hakutaka kubishana na Rahul akamkubalia tu
Walitoka mpaka kwenye hotel moja Rahul ndio alimuaguzia chakula
"Vicky naomba muda kidogo nahitaji kuongea na wewe!!"
"Sawa nakusikiliza "
Rahul alikaa kimya kama anafikieria aanzie wapi , Vicky nae akamkazia macho hapo alishamwandalia majibu ya kumpa kama yote mana alijua wazi anataka kuizungumzia mimba yake
"Vicky, naomba tuongee kuhusu masha kuna vitu nataka kukuomba msaada"
Vicky akashusha pumzi akamuuliza vitu gani??
Rahul akajiweka sawa akainua maji akanywa wakati anaweka mezani akamtazama Vicky
"Unajua Vicky wewe upo cool sana kuliko dada yako, najua unaweza kuongea nae baadhi ya vitu, masha ni hana zile sifa za wasichana wa Africa nilizo kuwa nasikia kipindi chotee ,
Mr Alberto sio mtu wa hivyo kama anavyomchukulia yeye anaweza kumuendesha hivyoo ,asimchukulie udhaifu wake akajua ameshinda , Hapendi kufanya kazi ,Kusoma hataki,Anatumia pesa hovyo hovyo sanaa kiasi kwamba hata kama mtu unamiliki kisima cha pesa zinaweza kukauka ,
Embu jaribu kuongea nae Vicky wewe ni mtu makini sana nakuomba uongee na dada yako"
Mr Alberto na Mashaa??? Vicky alishtukaa
"Yaan huyo mchumba wa Masha ni Mr Alberto???"
"Ndio , kumbe hakuwaambia hili??"
"Mh,walikutana wapii??"
Swali hili lilikuwa gumu kwa Rahul , wakati Vicky anasubiri jibu , Yeye alikumbuka maneno ya Masha
Masha alimwambia "fanya ufanyavyo hii siri ibaki kati kati yetu sitaki aibu watu wajue mie nilibakwa au nimefanyishwa mapenzi kwa nguvu kama ukimwambia yeyote hata ndugu zangu naapa naenda kuwashtaki police "
Rahul akacheka kidogo akamwambia Vicky muulize dada yako mwenyewe mana yeye ndie anajua ukweli walivyokutana mie sikuwepo
Vicky akasema sawa namie siwezi kumchagulia maisha yeye akiamua kufanya kazi atafanya naomba unipeleke nyumbani!"
Rahul hakutaka kuendelea kubishana lakini la moyoni alitoa hampendi hata kidogo mashaa anatamani hata kurudisha siku nyuma tu ili kumsaidia kwa njia nyingine Boss wake
Akamrudisha Vicky nyumbani kwao , yeye akaondoka zake
Vicky anaingia tu chumbani akakutana na masha na alikuwa anamsubiri muda wotee
Alimvuta kwa nguvu akamtupia kitandani
"Ulikuwa unaongea nini na Rahul?? Ulikuwa unaongea niniiii!!? "
"Masha mbona hatujaongea kibayaa??"
"Hicho kizuri ndio nataka kusikia hayaa nambie ulionge nae nini??"
"Alinisaidia tu kule nilienda kumtafuta Moze nikaishia kugombana na Lydia basi hivyo tu"
"Mlienda wapi siku nzima na sahizi ndio unarudi ukanizimia simu"
"Kwani ulikuwa unanifatilia?? "
Masha akampiga bonge wa kibao hakupenda swali kama hiloo
"Na kwanini nikufatiliee" akamuongeza tena kibao kingine akaanza kumpiga anamwambia sitaki njaa zako usogeze kwa watu wangu wa karibu watu muhimu sitakiii sitakii mjinga kwanza toka kwetu tokaa "
Mama yake na masha akaja mbio baada ya kusikia kelele
"We masha ninii??"
"Simtaki humu ndani huyu simtaki"
"Kwani kwako humuu?? Si unakwako wewe?? Si umeamua kuwa na maisha yako huko umetukimbia humtaki hata mtoto wako tu sio wewe ,"
Mamaaa Vicky anamimba kaokota huko mtaani hamjui baba wa mtoto anataka kumpa mzigo Rahul mie sitaki mnataka tuonekane maomba omba ??"
Mama masha akashangaa , Siku zote anamjua Vicky ni mstaarabu anajua hana mahusiano yeye mwenyewe alisema mpaka atakapo maliza chuo
Akamgeukia akamwambia et ni kweli
Vicky akabaki kulia akasema ndio akamuuliza baba wa mtoto unamjuaa??
Vicky kabla hajajibu masha akasema amjue wapi analala na kila mwanaume mie siwezi toka hapaa
Duuh mama masha akabaki tu mdomo wazi
"Sina uwezo wa kukuhudumia wewe na mwanao Vicky sinaa" mama masha akajitetea
"Haina shida mama hata usijali mie bado kijana naweza kutafuta "
Masha akamfukuza huku anamwambia marufuku kabisa kumsogelea Rahul.marufukuuu
Akampokonya simu kukagua labda kuna namba ya Rahul na kweli alikuta namba ya Rahul
Masha alicheka kwa hasira yaan Rahul hajawahi kumpa namba yake yeye lakini amempa Vicky aliiblock halafu akaifuta kabisa ndio akampa simu yake Vicky ...
Vicky akakumbuka Rahul aliweka namba yake kwenye simu yake ili aipate namba yake akajipigia lakini hakukuwa na salio akamwambia naomba utanipigia niipate namba yako ukiwa na tatizo lolote nambie
Vicky akakubali lakini hakumtafuta ba hiyo namba ndio masha akaifuta haraka ...
Vicky alichukua nguo zake akampigia simu rafiki yake ambae wanasoma nae chuo akamuelezea kuwa amefukuzwa anapo ishi hana pa kwenda ,
Rafiki yake akamwambia haina shida njoo nyumbani kwetu,
Masha akajiapia moyoni hawezi kuruhusu huyo mtoto azaliwe mana atamuharibia kila kitu
Vicky akaenda moyoni anampango akimaliza tu chuo bado miezi michache atafute kibarua cha kufanya kuliko kurudi kijijini kwao tena na mimba atamvunja moyo baba yake
Hapo ndio maisha ya Vicky yaligeuka kuwa magumu sanaa mimba ilikuwa inamsumbua
ITAENDELEA....
KWETU morogoro.