Mimba?? Hapana haiwezekani siwezi kuwa na mimba mimiπ₯Ήπ₯ΉVicky aliyakataa majibu ya mimba aliondoka hadi duka la dawa akanunua kipimo cha mimba akajipime mwenyewe nyumbani..
Masha alikuwa nyuma yake anafuatilia mchezo mzima ..
baada ya Vicky kuondoka duka la dawa , Masha akashuka kwenye gari yake mpaka mule ndani
"Habari dadaa" akamsalimia muuzaji huku anasogea
"Poa karibu"
"Samahani et yule dada alikuja kununua dawa gani hapa"
"We dada wewe hahah na kwanini niongee habari za mtaje"
Masha hakumjibu alitoa Elfu 30 akampa
"Haya nambie basi nanunua hizo taarifa "
" hahaha yaan wewe bwanaaa!!, amenunua U.P.T"
Masha hata hakujibu alitoka zake anawaza
"Kwahiyo ana mimba??,???"
Masha akarudi kule hospital akanunua taarifa za ugonjwa wa Vicky bila shida Doctor akamwambia kuwa yule ni mjamzito
Sasa masha kichwa kilimuumaa yaan mambo si yatavurumuka kama akijifungua mtoto rangi lazima afate kwa Mr Alberto
"Mungu wangu nafanya niniii??" Alienda andesha kichwani anawaza afanye nini na hii mimba ya Mr Alberto ...
Vicky yeye hakwenda nyumbani baada ya kutoka hospital alienda moja kwa moja pale hotel alipo kuwa akifanya kibarua
Alimkuta mlinzi mwingine akamsalimia akamuulizia Yule mlinzi aliesemekana ndie alimbk akaambiwa mbona alisha aacha kazi siku nyingii ana zaidi ya wiki mbilii
Akaomba ajue hata anapo kaa wote wakasema hakuna anepajua wala mawasiliano hakupata
Alirudi nyumbani kachoka akili na alipo pima na UPT ndio kabisaa alihisi kudata baada ya kipimo kutoa mistar miwili
"Mungu wangu ntafanya nini mimi nazaa vipi mtoto hana babaaa aah "
Vicky alikuwa amejifungia ndani analiaa
Muda huo huo Mlango wake ukafunguliwa akaingia masha ,Vicky akafuta haraka machoziii
"Unalia niniii??"
"Hamnaa"
"Kwahiyo siku hizi tunafichana "
"Masha nina mimbaa!" Vicky alijikaza akamwambia mana huyu ndio anajua mpango tangu mwanzo
"Hee !! Ya nanii"
" yule mjinga mose" Vicky akafuta machozi kwa hasira akimtaja huyo moze yaan yule mlinzi
"Uwii sa utafanyajee??"
"Sielewi hataa "
"Toa"
"Niniii"
"Toa mmb hiyo acha ujingaa"
"Hapana siwezi mwanangu hana kosa "
"Hee !! Mwanao au mwanake ?? Mtoto akizaliwa ndio wako kama hajazaliwa ni wa baba yake achana nae bwanaa ,
hivii we Vicky una maisha shoga angu au una hela mie sijui auuu hiyo mimba unataka mie tena nikufuge hapa kwetu eeh?? ,
Toa hiyo bado ndogo , ngoja nikakuletee vidonge utoe kwakweli mie siwezi nikulee wewe na mwanao ??" Haiwezekani
Vicky akabaki njia panda ,masha ashatoka nje mudaa sana akachukua gari yake mpaka Pharmacy akaelezea shida yake haswa kutaka dawa za kuharibu mmb
Vicky hajui kinachoendelea alibaki ndani amejiinamnia tu maneno ya masha yanapita kichwani kwakwe
"Sina maisha kweli,nimekuja mjini kusoma lakini hii ilikuwa ajali ndio nimmalize mtoto wangu??, na Nyumbani baba nitamwambia niniii imekuaje nimebeba mimbaa mungu wanguu Embu nipe njiaaa"
machozi tu yalikuwa yanamtoka mbele anaona giza nyuma Giza swala ka kutoa mmb Vicky wala halikujaa kichwani kwakee
Mwisho alipata shaurii akainuka akavaa nguo zake
Anafungua mlango kutoka ndio na masha nae kafika
"Unakwenda wapi"
"Nakwenda kumtafuta moze mpaka nimpatee "
"Vicky bwana embu acha ujinga unaenda kumpatia wapi?? Akikukataa??"
"Baada ya yeye kukataa hii mimba ndio nitajua niende wapi lakini nakwenda huko huko"
"Okay safari njemaa"
Masha akampisha njia Vicky apite ,
Baada ya Vicky kuondoka masha akajitupa kitandani anachekaaa
" hahaha yaan hapo nimecheza kama pereee hahaha daah sijui ingekuwaje kama nisinge mlipa pesa nyingi yule mjinga kumuhamisha mkoa daah Ngoja amtafuteee lakini hiyo mimba lazima iondolewe lazimaaaaa"
"Kwanza siwezi kulala hapa nina raha gani mie aah, anaweza pata chochote "
Masha akainuka kumfatulia Vicky huku moyoni akijisemea hii mmba lazima iondolewe leoleo..
Je itakuwaje??
KWETU morogoro.