Masha alijichekesha tu mbele ya Mr Alberto lakini moyoni hakumtaka hata kidogo Rahul na hapo alipo kuja kumkatishia ndo kabisa akamuona mkosi kwakee
,"Mr Alberto ni zaidi ya mwanaume asante mungu umenipa huyu mwanaume jamani aaaah, najisikia hamu ya kumuona tenaaaa embu ngoja nimpigie ooh mungu wangu nimesahau hata kumuomba namba yake ya Tanzania hii haipatikani ,lakini si anakuja nyumbani mbona nina presha isiyo kuwa na maana?? Hahaha ooh jamani nahisi preshaaa sijawahi kuona mwanaume kamili kama huuyuuu "
Masha alikuwa anajisemeza mwenyewe ndani ya Gari wakati anaelekea nyumbani kwake...
Kabla ya kufika nyumbani kwanza alipitia sokoni akanunua mahitaji aliyoona yanafaa kwa ajili ya chakula cha Mr Alberto
"Nahakikisha namshika kuanzia kwenye chakula mpaka kitandani hachimoki kabisaaa, Aaah Vicky, Vicky Vicky aaaah "
wazo la mimba ya Vicky likipita kichwani kwake ndio kabisaaa linamuaharibia furaha zakee ........
Alinunua mahemezi yote akarudi nyumbani watu wake wakapika alihakikisha anasimamia chakula kiwe mwaah na ikawa hivyo kwelii ...
Hakuwafukuza tena ila aliwaambia kulala mapema sanaaa hataki jau kwa mgeni wakee..
***
Mpaka sa 6 usiku ndio kikao kilikuwa kinaisha sasaa ,
"Nitakuendesha Kiongozi umechoka sanaaa"
"Aah Rahul unajua mie kuna kitu kinaniumiza sana kichwa??"
"Mhu kipii??"
"Ingia kwenye Gari tutaongea "
Kabla hata Gari haijatoka Mr Alberto aliomba kuongea na Rahul mana yeye ni mwenyeji sana huku kuliko yeyee kidogo anauelewa na hii Nchi
"Unajua yule mschana nilisababishia ajali yulee"
"Mhuuu??"
"Hata sijui imekuwaje Rahul , Yaan nashindwa kabisa kupitisha sec bila kumkumbuka huyu dada, Sura yake sio ngeni akilini mwangu nahisi kabisaaa kuna mahala nilisha wahi kumuonaa lakini sikumbukii , ajabu sasa kinacho niumiza kichwa nina hisia nae et tena hisia kali ,nikwambie tu ukweli Rahul nilipo mshika masha sijahisi chochote tofauti na yule dadaa ,Halafu ni mjamzito sielewi hata"
"Usharogwa ujue"
"Aah sio kweli"
"Nimekutana na hizo story nyingi sana huku yaan huku wanawake wanaroga ili wapendwe mzee tena nasikia wakikuona una chochote kitu aah umeisha hivyo, afu wanatamaa sanaa ndo kinawaponza "
"Sio bana. , yule dada hana tamaa yaan hana kabisa tamaa na pesa za watu ningemuona tu "
Mr Alberto akamuelezea Kuhusu Abigael jinsi alivyokuwa anamkataa na yeye analazimisha kuwa nae karibu akamwambia kama angekuwa ameniroga I'm sure angeniganda sanaa lakini ananikatia sanaa"
Rahul akamuuliza
"Anaitwa nani??"
Abigael "
Vicky hakutaja jina lake halisi kwa Alberto aliongopa anaitwa Abigael hakupenda tu kutaja jina lake halisi
"Yaan Tangu nimeishi hapa Tanzania mpaka leo hii Kuna mdada mmoja tu ndio niliwahi kumuona hana tamaa kabisa na ninafikiri Tanzania hii yupo yeye peke yakee, Ajabu unaniambia kuna mwinginee, yule dada alikuwa anaitwa Vicky ni ndugu yake na masha nilishawahi kukupa story yake
Yule dada hata sijui alipotelea wapi
Nilishawahi kumuuliza Masha akasema hakuwa ndugu yake walikuwa wanamsaidia tu kwahyo hata hajui alipo enda dah yule alikuwa mwanamke bwana hana kabisa presha na vitu visivyo muhusu'"
Bila kujua Vicky ndie Abigael ,Mr Alberto akasema
"Sasa huyuu ndo nakwambia hanaaa tamaaa hata chembee ,Kesho asubuhi nampelekea Lain za simu utamuona"
"Usinambie tu ushaanza kuhudumia mimba?"
"Hahah hamna halafu natamani kweli kumsadia nina uhakika jamaa wa mimba hayupo"
,"daah hizo kesi nazo huku zipo nyingiii wanaume wanakimbia sana mimba. Hapo ndo nakuja kuunganisha matukio ndo mana wanarogwa sana"
" basi makosa ni ya wanaume sio wanawake zao, twende tukapumzike "
Walipiga story haoo usiku ukazidi kuwa mkubwa
Ndio wakakumbuka kuondokaaa...
****
Masha alisubiri mpaka usingizi ukampitia juu ya meza hapo hapo ..
Sa tisa kasoro usiku ndio Rahul alimfikisha nyumbani Kwa masha Mr Alberto
",sijisikii kabisa kuwa hapa Rahul"
"Ndo kwako bro ,Au unataka kuharibiwa sifa, mwanamke mwenyewe mtata sana huyo"
daah"
Mr Alberto alishuka kishingo upande tu lakini roho yake haikuwa tayari kwenda humo ndani ..
Mr Alberto alimkuta Masha amelala Juu ya meza alijisikia vibaya sanaa
"OMG!!! Alikimbia akamchukua kwa kumbeba ili akamlaze ndani..
Masha alishtuka yupo kwenye mikono ya Mr Alberto tena amebebwa akajikausha kimyaaa
Huku anasikilizia harufu nzuri ya kupoaa
Itaendelea..
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.