MWANDISHI ::HURU MEDIA
Maisha ya Vicky yalibadilika ikawa afadhari ya maisha yale aliyokuwa anaishi kwa kina masha , pale alipo hamia kula unajitegema alicho pewa ni eneo la kuishi tena kwa amani zote
Alitafuta vibarua vya kufanya ule muda ambao hana vipindi walau apate pesa za kuendesha maisha ..
Masha kwake maisha yalizidi kumnyookea hakufanya kazi lakini kila siku pesa ziliingia kwenye acc yake ..
Kwa kipindi chote Mr Alberto hakuwa amefika Tanzania bado aliendelea kuwasiliana na Masha kwa ukaribu kabisa
Moyoni mwake alikubali kumuoa kwa sababu aliamini yeye ndie ameharibu usichana wa huyu dada kwa matatizo yake , Kitu kingine anathamini kuwa alisaidia , ..
Siku zikaenda wiki zikapita ikawa mwezi hatimae miezi 7 ilipita tangu mambo yote yalipo anza kugeuka kwa Vicky
Mimba ilikuwa kubwa ya miezi 7 na zilikuwa bado wiki kadhaa afanye mitihani ya kumaliza Chuo , baada ya chuo ni kusota mtaani kusubiri ajira ambazo haujui mwaka gani utazipata ...
" yaan siku zinaenda jamani duuh hatimae tunaenda kumaliza chuo"
"Recho mie ndo hata sielewi ujuee , "
"Utakaa kwetu hata usijali mpaka utakapo jipata lakini kwa ushauri wangu usiende kwenu hivii ,bora Upeleke mtoto kuliko mimba aisee ,Halafu nimekumbuka ...."
Vicky na Rafiki yake ambae ndio anaishi kule kwao walikuwa wanapiga story za hapa na pale wakati wanarudi nyumbani
"Ninii??" Vicky aliuliza baada ya Recho kuwa kama amekumbuka jambo
"Kuna Bonge wa Studio imejengwa huko Bagamoyo ,Studio ya utengenezaji movie na Music , Ya mzungu nasikia kutokea Los Angels California Hukoo , Twende tukajaribu kuomba kazi tuna cheti sie "
"Hahah yaan wewe bwana una chet kiko wapi wakati ndio kwanzaa unatakiwa kufanya mitihani enyewe "
"Eeh Mungu wangu hahaha kweli nimedata Ila twende tukaombe kazi bado haijafunguliwa lakini nasikia kubwaa inachukua wafanyakazi mpaka 500
Twende tukaombe hata usafi mpaka inakuja kufunguliwa Tutahama ngazi tukiwa na vyeti"
"Hee mie usafi na hili tumbo naweza wapii??"
"Jamani embu twende acha ubishii"
"Basi Asubuhi kesho twende tukajaribu "
"Hapo sawa"
**********
Eeeh mungu wangu siaminii!! Yaan mie ndio nakuwa mke wa mmliki wa hapaa oooh Mungu wangu Eeh Yaani siaminiii kabisaaa "
Masha nae Asubuhi hii alikuwa huku pamoja na Rahul akitembezwa kila kona ya jengo kubwa la Studio za kisasaa
Rahul alikuwa anamwangalia tu matambo yake yalivyo ...
Mr Alberto moja kati ya uwekezaji aliamua awekeze kwenye Sanaa , Ndipo akajenga Studio kubwa ya Kisasa nje Ya mji wa Dar es salaam
Aliwekeza pia kwenye Afya Ndani ya miezi michache aliyomuacha Rahul Tanzania
Hospital kubwa ya kisasa ilikuwa imekamilika Mwananyamala Pamoja na Studio iliyopo Bagamoyo
Wakati Masha anafanya utalii ndani ya Studio ndio kina Vicky nao walikuwa wanakuja kupaangalia ili watafute kibarua cha kufanya usafi hapa
"Eeh nje tu pako hivi huko ndani sijui itakuwaje??"
"Bwanaa weee bonge wa Jengoo Duuh , twende ndani"
"tunapita wapi "
"Hapo getini si unaona hicho kidirisha Vicky wameandika Mapokezi tuanzie hapo"
"Anhaa haya twende "
Wanataka kupiga hatua kusogea, Geti dogo lilifunguliwa akatoka masha akiwa pamoja na Dereva wake na Rahul
Vicky alirudi mbio akajificha kwenye kona ya ukuta ulio kuwa karibu
Recho nae akamfata nyuma
"Masha anafanya nini hapa??" Recho akamuuliza Vicky kwa mshangao
"Sijui , mwenzetu siku hizi ana connection kubwa"
" yaan Mungu akitaka kukupa hakuandikii barua jamani , hachagui wa kumpa kaenda kumpa mtu mwenye Roho mbaya hamtaki hata mtoto wake khaa"
"Atajua mwenyewe "
"Kwahiyo tunafanyaje"
"Mie sijui bwana siwezi kuwa karibu na masha kaombe tu wewe kazi "
Vicky alichoka kumuona masha hapo tena alikuwa na furaha kweli anaonekana na maisha safii, amezidi kupendeza sanaa
"Sasa masha hapa ana fanya nini mana hapa wote ni watu wa marekani "
Kidogo Vicky akapata akili baada ya Recho kusema habar za watu wa marekani anajua mwanaume wa masha pia ni mtu wa marekani
"Anaitwa nanii??"
"Alberto Clinton "
"Mungu wanguu"
Vicky alihisi kuchoka akili
"Alberto, Alberto Kwanini yeye??"
'"Ndo niniii?"
"Kila naposikia jina la huyu mtu moyo wangu unalipuka sanaa nahisi kama kusalitiwa natamani kulia ,Yaan kuna hali naipata sijui kwaninii!! ,,, Huyo ndio mwanaume wa masha"
"Wee Vicky weweee, Eeeh Hakiamungu siamini yaan Masha ndio anamwaume tajiri hivyoo ,Eeh Heeee!! Nimekomaa walai, Wenzetu wanampa nini mungu jamani"
"We nenda tu nyumbani Recho mie ngoja niende kibaruani muda umeisha sanaa"
Vicky hakutaka tena kuendelea na hizo story wala kuwa hapo wakaondoka kurudi walipo toka
Tukio la Vicky kumuona masha hapo , lilimnyima rahaa , muda wote alijikuta anafikiria kuhusu mr Alberto ,
"Oooh mungu wangu kwanini yeye tuu!!" Alikuwa anajisemea pale mawazo yanapo zidi kumzoga hajui kwanini anamfikiria lakini kila linapo kuja hili jina kichwani kwake Anahisi kuumia sana moyoo
Rahul alimuacha Dereva wake amchukue Masha kumrudisha kwake , yeye akatoka na gari kwa kasi kuna sehem alikuwa anelekeza akiwa njiani Simu yake iliita Juu ya kioo Kulikuwa na Jina Boss
Akaipokea haraka
"Where are you, boy, I can't see you. I've arrived while I'm at the airport(Upo wapi kijana sikuoni Nimefika muda nipo Airport "
"I'm on my way right now. I'm arriving"
Rahul alijibu na kukata simu akaongeza Mwendo kuwahi Airport..
Ndani ya Airport alikuwa Mr Alberto baada ya kuondoka Tanzania miezi mingi , Ndio anarejea tena kwa mara ya pili .....
Hayaaaa Boss kubwa ndani ya nyumba amerudi Siri ya Masha inakwenda kujulikana au vipiii
Kumbuka Mr Alberto Hamjui mschana alietembea nae ile siku kutokana na kuwa alizidiwaaa
Tukutane sehemu ya kumi ina majibu kama yoteeee
ITAENDELEA........
Whatsapp
0657171961
KWETU morogoro.