DOZI NI SAA 7:00 MCHANA (01)
Kwa jina naitwa Oscar tarehe 1.5.2022 ni siku ambayo sitakuja kuisahau kwenye maisha yangu kwa kitendo nilichofanya kwa mke wangu aitwae Martha.
Siku hiyo niliamka asubuhi na mapema kama ilivyo kawaida yangu na kujiandaa kwa ajiri ya kwenda kazini mke wangu kipenzi Martha aliniandalia maji ya kuoga kama ilivyo kawaida, nilienda kuoga na kujiandaa kwa ajili ya kuelekea kazini.
"Mme wangu nakupenda sana ufike salama kazini kwako"Malikia wa moyo wangu alisema.
"Nakupenda pia mke wangu mwaaaaaaaa " Nilimpiga kiss Martha na kumuacha nyumbani na mimi uyoooo nikaelekea zangu kazini.
Nilipanda usafiri wa daladala kama ilivyo kwaida na kufika mida sahihi bahati nzuri siku hiyo nilikuta boss bado hajafika mana alikuwa ni mkali hatariiii hasa ukichelewa.
Nilikuwa nafanya kazi katika kampuni la usafirishaji japo mshahala ulikuwa mdogo ila ulitusaidia kusukuma maisha mimi na mke wangu nilipofika nilimkuta rafiki yangu tunayefanya nae kazi pamoja
anayeitwa Max tayali ameshafika,
"Oyaaah Oscar bora umekuja nilikuwa nakusubiri kwa hamu ninamchongo na una ela balaa"Max alisema.
"Mchongo gani?"
"Kuna doctor anatafuta mtu wa kufanya nae kazi kuna milion 100 zipo njenje"
Kwanza nilishituka mana milion 100 nilikuwa nazisikia tu kwa watu nikamwambia Max,
"Kwani wewe hautaki huo mchongo kama vip nenda ukauchukue wewe"
"Wewe siunajua mimi sijaoa bado ule unahitaji mtu mwenye mke tayali",Max aliongea nakunifanya nishutuke kidogo mambo ya mke tena yanaingilianaje na huo mchongo ila nilitamani kujua ni mchongo wa aina gani huo,
"emu niunganishe na mtu mwenye huo mchongo tupige ela",nilimwambia Max ambae alinipa namba za mhusika.
Kisha baaada ya hapo tuliendelea na kazi mpaka pale mda ulipoisha wa kazi na mimi nilianza kurudi home ila nikiwa naelekea kwenye usafiri wa daladala,
milion 100 bado zilikuwa kwenye kichwa changu niliamua kumpigia simu huyo doctor ili nijue ni mchongo gani.
"Hallo"
"Nani wewe pigia mimi simu" sauti ya mtu aliyekuwa akiongea kishwahili cha kuunga unga ilisikika.
Nilimwambia kitu kilichonifanya nimpigie simu palepale doctor akanielekeza sehemu alipo na mimi sikutaka kuchelewa nikamfata na kufanyikiwa kuonana nae ,
Alikuwa ni mzungu aliyejitambulisha kwa jina la Peter na tulianza kuongea nae japo kuna mda alikuwa anaongea kiingeleza ila ivyoivyo kidogo nilikuwa nakamata maneno machache.
Doctor peter alinipa mchongo wa mimi kuipata iyo milion 100 kama nitakuwa tayali kumfanyia kazi yake,
"Kazi gani Mr. Peter..?",nilimuuliza.
Badala ya kujibu alitoa sindano na kunionyesha ikiwa na dawa ndani yake,
"Hii sindano ndio pesa yako na unatakiwa umchome mke wako"
"Mke wangu doctor!!!",Nilishangaa kwa alichokisema Peter.
"Tulia kijana nipo kwenye majaribio ya kutengeneza dawa kwa ajili ya kuiingiza sokoni..
alisita na kuendelea kuongea...
na kazi yake ni ndogo tu mke wako atakuwa na hisia kali za kimapenzi zidi yako kama ukimchoma."
Kwanza nilicheka nikasema kumbe kazi yenyewe ndogo hiyo,
"Ndio kazi yenyewe iyo doctor??"
"Ndio kijana na ukishakamilisha kumchoma utapata pesa yako yote kwanza hapa nitakupatia kama milion 30 kama kianzio ikiwa utaenda mwenyewe ila tukienda wote na mimi nimchoma sindano mke wako nitakupatia pesa yako yote milion 100".
Sikutakata kujiuliza mara mbilimbili pasipo ata kufikilia nikamwambia doctor.
"Doctor haina haja ya kunipatia pesa nusu twende wote ukamchome mke wangu iyo sindano na unipe milion100"
Tuliweka makubaliano na alinitishia sitakiwi kuitoa iyo siri kwa mtu mwingine yule na ikiwa nitafanya ivyo nitajuta, kwanza tuliongozana wote akiwa amebeba begi lenye pesa mpaka nilipokuwa na kaa maeneo ya uswahilini nilimkaribisha doctor Peter huku majirani wakijiuliza tangu lini nikawa na mazoea na mzungu.
Nilimkuta mke wangu Martha, ata yeye alishangaa kuniona nimekuja pale na doctor peter, sikutaka kufanya siri nilimweleza kila kitu Martha japo alikuwa ni mwenye hofu kubwa ila baada ya kuona kuna pesa pale mezani nae alikubali kuchomwa ile sindano, doctor peter alimchoma sindano mke wangu na tukafanya makaniziano ya pesa nilipo zihesabu zile pesa kweli zilikuwa milion 100 kisha yeye akaondoka na kutuacha pale mimi na mke wangu.
"Oscar naogopa sana, hii sindano niliyochomwa haitaniletea matatizo kweli?"
"Mke wangu haina tatizo lolote lile kuwa na amani tu kwanza hapa tunahama sasa ivi sio pakukaa tena"
Milion 100 zilianza kuiendesha akili yangu tulitoka pale huku vitu nikiwagawia majirani kana kwamba nimeyatoboa maisha kwanza tulielekea kwenye hotel ya kifahari mimi na mke wangu na tulikaa hapo kwa siku iyo nzima mpaka ikaisha tukiwa na pesa zetu.
Siku iliyofata sikutaka kabisa ata kwenda kazini nilishinda na Martha palepale hotelini tukiendelea kuzagamuana,
Ilipofika mida ya saa 7:00 mchana hali ya Martha ilibadilika kwanza alianza kutetemeka kama simu ndogo au kiswaswadu miguu yake ikiwa haitulii na anahema kwa kasi hali iliyonifanya niogope.
Nilichukia simu yangu na kumpiga doctor peter ambaye alipokea,
"Doctor hali ya mke wangu mbaya anatetemeka kama genaretor"
"Fanya nae mapenzi atatulia"
"Doctor!!!"
"Huyo si mke wako unaogopa nini nimekwambia fanya nae mapenzi atatulia na ikifika saa 7:15 tu anakufa ili arudi kwenye hali yake inatakiwa ufanye nilichokwambia".
Nilikata simu ili nifanya kile doctor alichoniambia ila tatizo sasa nikuwa karibu usiku mzima wa jana tulikesha tukifanya mapenzi na ata leo tuliamkia kwenye mizagamuo na nilivyomtazama mke wangu ndio hali yake ilizidi kuwa mbaya, nikimwangalia asikari wangu kalala hataki ata kuamka,kucheki dekika zimebaki tano tu
ifike saa 7:15. ......ITAENDELEA...