MFALME KIPOFU 23 -- 24
Whatsapp.............0748697173
ilipoishia sehemu iliyopita.......
Maneno yale yalipenya kwenye masikio ya Amma na baadhi ya watu waliokuwa pale wakitazama tu badala ya kutoa msaada,Babaaaaa............
ENDELEA NAYO..........
"Baba amka",Amma alimwita baba yake,
Aliye kuwa tayali amepoteza maisha na kilibaki kilio tu kwa binti Amma.
Japo matabibu wenzao walikuwa kwenye msululu wa kwenda kuhojiwa na kupokea adhabu zao walijikuta wakimuonea huruma binti yule.
"Nani huyo anaye piga kelele kwenye jumba la kifalme"
ilikuwa ni sauti ya Malikia Andwaa ambae nae amevulugwa na ugonjwa wa mume wake alifika maeneo yale.
"Ni huyu binti Malikia amefiwa na baba yake hapa kuna mtu kamchoma kisu",aliongea mlinzi wa jumba hilo la kifalme.
"Itoeni iyo mauti na taratibu zingine ziendelee", Malikia Andwaa aliongea pasipo kujali kama aliyekufa ni binadamu na sio mnyama.
Kwamaneno aliyozungumza Malikia Andwaa yalimpandisha ukichaa binti Amma aliye nyenyuka kwa hasira na kusogea alipo Malikia Andwaa.
"Baba yangu amefia hapa alafu mnataka kuitoa maiti ya baba yangu bira kufanya uchunguzi ni nani aliyemuua???"
"Wewe ni nani mpaka unaongea na mimi Malikia kwa kujiamini, hujui kama kunazoezi hapa la kutafuta watu waliotengeneza sumu ya Mfalme???"
"Kwanza haina haja ya kuendelea kuwapiga watu wasio na hatia nimeshapoteza kila kitu sasa",Amma aliongea huku akipiga magoti chini na machozi yakitililika.
"Unamaana gani wewe binti kusema tusiendelee kuwahoji watu???",Malikia andwaa alihoji.
"Mimi hapa ndie niliyetengeneza sumu ya Mfalme".
Amma hakutaka kuendelea kuficha tena ile siri licha ya baba yake kuhusika kutengeneza sumu ile,lakini aliamua kuzibeba lawama zote na hakuona tena sababu ya watu wengine kuendelea kupigwa huku wahusika ni wao.
Watu wengine wasiohusika waliachiliwa na alibaki binti Amma peke yake pamoja na maiti ya baba yake pale chini ambayo ilitolewa na kwenda kuzikwa bira kufata taribu zozote zile za mazishi na hii ni kutoka na Amma kuwa chini ya uangalizi mkali.
Shariti la kwanza alilopewa binti Amma nikutengeneza dawa ya ile sumu kabra haijamzulu kwa kiasi kikubwa mfalme na kisha adhabu nyingine itakuchukua nafasi baada ya kukamilisha kazi ya kwanza.
*****************
Lindiwe akiwa na Prince Yao pamoja na Princess Nailet wanafika katika jumba la kifalme karibu na mlango wa siri wa jengo la kifalme, na Lindiwe alikuwa anaufahamu vizuri mno mlango huo.
"Kufika tumefika ila sijui kama kuna mtu karibu humo ndani atakaye tufungulia mlango"
"Jaribu kugonga kwa umakini zaidi"
Lindiwe aligonga sehemu ile yenye mlango wa siri karibu mara tatu pasipo mtu yoyote kuja kufungua.
Malikia andwaa sehemu ambayo hupenda kutulizia mawazo yake basi ni karibu na mlango ule wa siri mana ni sehemu aliyo aliachana na mtoto wake kwa mara ya mwisho na ata leo pia aliamua kwenda kutuliza mawazo karibu na ule mlango.
"Hamna mtu yatupaswa tutafute njia nyingine tu".,Princess Nailet aliongea.
"Ngoja nigonge kwa mara ya mwisho"
Lindiwe aliongea na kugonga kwa mara ya mwisho.
Namu Malikia andwaa temu hii alisikia mlango ukigongwa alisogea kwenye ule mlango na kufungua,
Hakuamini macho yake baada ya kumuona Lindiwe mtumishi aliye potezana nae kwa mda mrefu na alipotazama pembeni alimshuhudia mwanae akiwa bado na upofu wake uleule akiwa pamoja na binti ambae ni Princess Nailet.
Ilikuwa ni furaha sana kwa malikia ivyo aliwapitisha katika mlango ule wa siri na kwenda kuwainginza ndani hakutaka tena kumficha Prince Yao kama alivyofanya miaka ya nyuma.
********************
Tarifa zinamfikia General kuwa binti hakufa na amekubali kumtibu mfalme kwa kumtengenezea dawa itakayoondoa sumu iliyo katika mwili wa mfalme.
"Haiwezekani huyu binti aje avuluge mipango yetu"
"General nini tufanye kwenye hili??"
"Kwakuwa sasa ivi anaishi chini ya uangalizi mkubwa inatakiwa akafie humohumo katika jumba la kifalme".
"Nzegi wewe utaenda katika jumba lile la kifalme kumuua yule binti"
"Huoni ni hatari kwangu General???", Nzegi aliuliza.
"Kuwa na amani tu umeishi mle kwa mda mrefu unajua njia zote na unajua mapigano vzuri sioni mtu wa kuweza kukuzuia."
Nzegi alikubali kishingo upande na hakulizika kabisa na mawazo ya General aliyompa ya kwenda katika jumba la kifalme.
*****************
Malikia alimtambulisha Prince Yao mbele ya Yanite na Yanni kama huyo ndio kaka yao licha ya upofu alionao walifurahi kumuona na kilicho wafurahisha zaidi ni uzuri aliokuwa nao Prince Yao.
Cheki akiwa anazunguka katika jumba la kifalme kuendelea kudadisi baadhi ya mambo alishangaa kumuona Yao mle ndani.
"Ivi ni macho yangu au naota huyu sindio yule mpuuzi niliye muacha kule kwenye ufalme wetu wa YUNDI aliyekuwa na mazoea na mwanamke niliyekuwa nampenda???",Cheki aliongea.
"Karibu sana Prince Yao"
Alisikia akiitwa Prince.......ITAENDELEA
Mambo yanaendelea,visa bado haviishia katika simulizi hii nzuri nini hatima ya binti Amma ambae General ameamua kumtuma Nzegi aje amuangamize katika jumba la kifalme na vip kuhusu hatima ya Cheki baada ya mwenye nafasi yake kurudi
[12/12/2025, 6:40 AM] zooper simulizi2: Story.....................MFALME KIPOFU
Mtunzi...................Zooper
Sehemi..ya............ 24
Whatsapp.............0748697173
ilipoishia sehemu iliyopita.......
Ivi ni macho yangu au naota?, huyu sindio yule mpuuzi niliyemuacha kule kwenye ufalme wetu wa YUNDI aliyekuwa na mazoea na mwanamke niliyekuwa nampenda???"
"Karibu sana Prince Yao"
Alisikia akiitwa Prince.......
SEHEMU YA 24
ENDELEA NAYO.......
Alisikia akiitwa Prince na hii kumfanya azidi kushangaa zaidi inakuwaje Yao awe Prince huku amekulia kwenye ufalme wa YUNDI,
kilicho mshangaza zaidi nikumuona Princess wa YUNDI akiwa pale hapo akaanza kupata uhakika na ukweli halisi wa kwanini walimu tafuta yeye kama Prince wa mda mfupi,
"Kumbe ndio mana walinitafuta mimi kisa Prince wao ni kipofu" yalikuwa ni maneno ya Cheke.
aliondoka katika jumba lile la kifalme na kuelekea msituni kumpa tarifa General pamoja na mwenzake.
Baada ya utambulisho wa Prince Yao kwa wadogo zake, Princess Yanite alimchukua kaka yake kwa kumuongoza na kumpeleka sehemu ambayo Mfalme Kojo amelazwa.
Walifika na kumkuta binti Amma anahangaika na matibabu kama alivyoahidi,alisogea pembeni na kuwacha watoe salamu kwa Mfalme kojo ambae alikuwa hajiwezi ata kuongea,
Prince tunajua huwezi kuona ila huyu ndie baba yako Malikia andwaa alimshikisha mikono yao kati ya Prince Yao pamoja na wa Mfalme Kojo.
"Natamani ningekuwa na uwezo wa kuona ningelipa kwa yule mtu aliyemfanyia mabaya baba yangu",Prince Yao aliongea huku ameshika mikono ya Mfalme Kojo.
"Mtu mwenyewe ata hayupo mbali kaka yupo hapahapa".Yanite aliongea na kumfunya Prince Yao anyenyuke,
"Emu mleteni katika mikono yangu huyo mtu mara moja nimnyonge".
Binti Amma aliona kweli wao ndio wenye makosa mana kama wasinge tengeneza ile sumu yote hayo yasingetokea alisogea karibu na Prince Yao yeye mwenyewe na kupiga magoti.
"Nipo hapa nifanye chochote unachoona ni sahihi kwa dhambi niliyoweza kuifanya ya kumfanya Mfalme awe kwenye hali mbaya". Amma aliongea huku amepiga magoti kwa Prince Yao.
"Unajifanya unajua kuongea sana na unabahati sina uwezo wa kuona ningekuwa na uwezo wa kuona basi adhabu ungeipata wewe binti", Prince Yao aliongea kwa hasira.
Binti Amma alikumbuka maneno ya baba yake aliyoambiwa kabra ya kufa kwake amtafute mtu kipofu na afate maagizo ya jinsi alivyokuwa akiota.
"Kama tatizo huoni mimi nitakufanya uone".
Watu wote mle ndani walishangaa maneno aliyotamka Amma kwamba anaweza kumfanya Prince Yao kuona.
Malikia Andwaa palepale alimsogelea Amma.
"Kama ni kweli unaweza kumponyesha mwanangu nitakutoa kwenye hichi kifungo na ukimaliza kumtibu mfalme utakuwa huru na utaendelea na mambo yako".
Binti Amma na Malikia waliweka makubaliano kama akifanyikiwa kumfanya Prince Yao kuona na kumtibu Mfalme basi atakuwa huru na ataendelea na maisha yake.
****************
Asikari waliotumwa na Mfalme Tengu kumtafuta Princess Nailet ilikuwa ni mtihani mgumu kwao kwani mpaka mda huo hawakufanyikiwa kumpata Princess.
"Tunafanyeje mana princess haonekani mpaka sasa au turudi tukamwambie mfalme tumemkosa??",moja ya asikari aliongea.
"Naona umechoka kuishi wewe",asikari mwingine aliongea.
"Mhimu yatupaswa tuongeze juhudi za kumtafuta tukirudi iviivi mfalme hatatuelewa kabisa"
Walikubaliana kuendelea kumtafuta Princess kila pande za ADELI.
************
Cheki anafika polini na kufikisha habari ambazo zinamfanya General azidi kuchafukwa zaidi.
"Unauhakika na unachokisema???"
"Ndio General prince wa kweli yupo katika jumba la kifalme na ni kipofu haoni,tuliishi nae katika ufalme wetu wa YUNDI karibu miaka 20 iliyopita "
"Huu sasa utani yani tunaelekea mwishoni mambo ndio yanazidi kuhalibika zaidi, Nzegi jiandae uende katika jumba la kifalme ukamumalize haraka huyo binti".,General aliongea.
Hakukuwa na mda wa kupoteza Nzegi anaianza safari ya kuelekea katika jumba la kifalme ili kukatisha uhai wa binti anayemtibu mfalme ambae ni Amma ili mfalme asipate mtu wa kumtibu.
************
Katika jumba la kifalme Baada ya kuweka makubaliano kati ya Malikia Andwaa na binti Amma,
"Kwani kuna uwezekano wa kuipata iyo dawa??",Malikia alimuuliza binti Amma
"Ndio ata sasa ivi mhimu tuwe na usafiri wa haraka".,Amma aliongea na kumfanya Malikia Andwaa afurahi na wote waliokuwa pale.
"Na vipi kuhusu mfalme, hatapata shida kama ukienda mbali na yeye mana wewe ndie unaye mtibu??",
"hapana malikia dawa mpaka kesho tena ndio nitampatia Mfalme kwa sasa inatakiwa apumzike tu", Amma alijibu.
"Aya twendeni hatuna mda wa kupoteza"
Malikia Andwaa alianza kuondoka.
Princess Nailet alitaka kuongozana nao
ila Lindiwe alimzuia,
"Usijali Prince Yao inatakiwa akirudi akukute umependeza zaidi mana naamini atakuwa anaona naamini maneno ya huyu binti kwa jinsi alivyo ongea inaonyesha kweli dawa anaifahamu".
Maneno ya Lindiwe yalimfanya Princess Nailet kutabasamu nakutulia kuwaacha waongozane watu watatu tu Malikia, Prince Yao na Amma mwenyewe kwenda kutafuta iyo dawa........ITAENDELEA.
Amma atafanyikiwa kumtibu Prince Yao na vip kuhusu Nzegi anayekuja katika jumba la kifalme kwa ajili ya kumuua Amma huku Amma mwenyewe akitoka katika jumba la kifalme tukutane sehemu inayofata..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni