MFALME KIPOFU 17 -- 18
Sehemi..ya............17
Ilipoishia sehemu iliyopita......
Lindiwe alitege sikio vizuri na kweli alisikia sauti emu njoo huku alimvuta Prince Yao pembeni na kujificha sehemu ni ngumu kuonekana.
Namu sura ya General haikutoka
machoni mwake alimuona
General akiwa......
ENDELEA NAYO..........
General akiwa pamoja na mlinzi mkuu kwa wakati huo ambae ni Nzegi, alijiuliza ni kipi kilichowaleta usiku ule katika msitu huo ila hakupata majibu sahihi, walivyopotea machoni mwake na yeye alimchukua Prince Yao na kuondoka nae.
Akiwa njiani Lindiwe alitafakari ni sehemu gani atafikia kwa ajili ya kupumzika usiku huo, na ndipo kumbukumbu za rafiki yake waliyewahi kufanya kazi pamoja katika jumba la kifalme zilimjia na kuamua kuongoza njia kwenda kwenye makazi ya rafiki yake huyo wa enzi izo.
Lindiwe anafanyikiwa kufika akiongonzana na Prince Yao mpaka katika nyumba ya rafiki yake na kubisha hodi.
"Nani tena huyo anayebisha hodi usiku huu ????",sauti ya kike ilisikika.
Alinyenyuka na kufungua mlango, hakuamini macho yako baada ya kufungua mlango mtu aliyepotezana nae zaidi ya miaka 20 anamuona kwa mara nyingine tena.
"Ni wewe Lindiwe??"
"Ndio, ni mimi"
" basi karibu ndani".
Walikalibishwa vizuri na rafiki yake huyo baada ya kutokuonana kwa mda mrefu marafiki hao wawili na Lindiwe hakutaka kumtambulisha Prince Yao kama Mwana wa Mfalme bali alimtambulisha kama mtoto wake kwa rafiki yake huyo.
*****************
Tarifa zilimfikia Mfalme usiku huohuo juu ya kifo cha waziri mkuu na alijua lazima atakuwa General aliyehusika na kifo hicho.
Ilikuwa ni huzuni kubwa kwa familia ya waziri mkuu kutokana na kifo chake kuwa cha kikatili zaidi na hii ikawafanya viongonzi wote waimalishe ulinzi katika makazi yao,
Na katika jumba la kifalme ulinzi uliimalishwa mara mbili zaidi.
Cheki akiwa katika jumba la kifalme alishangaa kuvutwa pembeni na asikari wa jumba hilo la kifalme,
"Siri yako naijua wewe sio mtoto wa mfalme"
"Mimi ni Prince,nani kakwambia mimi sio Prince???
"Usijifanye hujui, hukumu yake ni kifo kama uki gundulika sio Prince kwahiyo fanya ninacho taka ili uendelee kuishi kwa amani humu ndani, alikuwa ni rafiki wa Nzegi aliyeamua kumtisha Cheki kama alivyotumwa na General".
"Kwani unahitaji nini kutoka kwangu?
"Kesho uongozane na mimi majira ya jioni utajua nini nahitaji kutoka kwako" aliondoka pasipo kusubiri jibu kutoka kwa cheki kama kakubali au la
. ****************
Kukiwa bado na masiba wa Wazari mkuu asubuhi ya siku inayofata General aliamua kumpa mbinu atakayo tumia kumu angamiza mfalme pasipo kutumia nguvu yoyote,
"Hapa inatakiwa tutafute watu mashuhuli wanaotengeneza dawa"
"Kwani unaumwa general mpaka utafute dawa??".
"Itakuwa dawa ya mfalme itakayomfanya aondoke duniani"
"General unaongea kimafumbo bado sijaelewa"
"Tunaitaji tutengeneze sumu maalum ambayo itamuangamiza mfalme ndani ya siku tano tu na watu peke wanaoweza kutusaidia ni hawa wanaotibu watu kwa dawa za hasili".
Nzegi alielewa mipango ya General na walianza kuulizia wanapopatikana matabibu hao wa dawa za hasili, maeneo yaliyo pembezoni mwa mji walielekezwa sehemu wanayopatikana.
Katika kijiji cha Nyengweli,
Binti Amma akiwa anatengeza dawa alipata ugeni ulio mfanya awakalibishe kwa hekima watu wale sababu ilikuwa ni kawaida watu kufika pale kwa ajili ya matibabu,
Na watu hao hawakuwa wengine bali ni General pamoja na Nzegi,
"Binti unatufahamu sisi???, General aliuliza ili kuona kama binti atakuwa amegundua kama wao ndio wanaotafutwa na mfalme"
"Hapana".
"Sawa mhusika wa hapa yupo wapi???"
"Ni mimi hapa nasaidizana na baba yangu???.
General aliangaza kuona kama kuna watu wengine wanaowaona alivyojihakikishia hakuna alimwomba binti amwite baba yake naye akatii maagizo yale,
"Karibuni", ni sauti ya baba yake na Amma.
"Asante, mzee mwenzangu tunaomba ututengezee sumu inayoweza kumuua mtu ndani ya siku tano tu yani akinywa ugonjwa unampata kuanzia masaa 4 yajayo"
"Siwezi kutengeneza sumu ya kumuangamiza binadamu mimi"
"Aaah huwezi sawa".
Palepale General alimkamata Amma aliyekuwa amesimama pembeni na kumuweka upanga kwenye shingo yake,
"Sasa chagua afe binti yako au utengeza sumu"
Baba Amma hakuwa na jinsi na ukizingatua ndie mtoto peke aliyenae
"Nipeni masaa 2 tu sumu itakuwa tayali".
"Sawa lasivyo......ITAENDELEA
Kwa 500 tu ya kitanzania unapata mwendelezo mpaka mwisho wa simulizi hii tamu lipia sasa kupitia namba 0613083801 HALOPESA Jina john Bugumba kisha njoo WhatsApp kwa namba 0748697173 upate simulizi yako mpaka mwisho
Nini hatima ya Prince Yao baada ya kufika katika ufalme wao?? na je? General atamuua binti Amma baada ya kumuwekea upanga shingoni mwake? Tukutane sehemu ya 18 inamajibu zaidi
[12/12/2025, 6:40 AM] zooper simulizi2: Story.....................MFALME KIPOFU
Mtunzi...................Zooper
Sehemi..ya............18
Whatsapp.............0748697173
Ilipoishia sehemu iliyopita......
Sasa chagua afe binti yako au unatengeza sumu"
Baba Amma hakuwa na jinsi na ukizingatia ndie mtoto peke aliyenae
"Nipeni masaa 2 tu sumu itakuwa tayali".
"Sawa lasivyo........
ENDELEA NAYO.....
"Nipeni masaa mawili(2) tu sumu itakuwa tayali"
"Sawa lasivyo mwanao utampoteza".
"Baba bora mimi nife kuliko utengeneze sumu ya mtu mwingine kwenda kufa asiye na hatia"
"Unajifanya unajua kuongea sana wewe binti",
General alimchoma kidogo Amma sehemu ya bega na kumfanya apige kele.
"Baba inaumaaa"
"Binti yangu tulia utakufa kuwa muelewa nione huruma mimi baba yako",aliongea kwa masikitiko makubwa na kumfanya Amma awe mpole mbele ya General.
********************
Katika Ufalme wa YUNDI Mfalme Tengu anabisha hodi chumbani kwa binti yake pasipo kuwa na majibu yoyote ya mtu kufungua mlango,Temu hii ana sukuma mlango na unafunguka,
Hakuamini baada ya kuto kumuona binti yake ndani ya chumba chake icho ila alipotazama pembeni alikutana na barua,
"KWAKO BABA KIPENZI, WEWE NI BABA BORA KWENYE HII DUNIA, NAJIVUNIA KUPATA BABA MWENYE UPENDO KAMA WEWE NIMEAMUA KWENDA KUITAFUTA FURAHA YA MTU NINAYE MPENDA KWA DHATI, KWANGU FURAHA NI MHIMU KULIKO KUWA MALIKIA NISIYE KUWA NA FURAHA NISAMEHE SANA BABA YANGU NIMEAMUA KWENDA KUMTAFUTA YAO NA SIWEZI KUISHI BIRA YEYE".
Alimaliza kuisoma ile barua huku machozi yakimtoka tu,
"Huenda nilikudekeza sana binti yangu ndio mana leo hii hutaki kunisikiliza mimi baba yako,Mfalme Tengu aliongea kwa uchungu sana baada ya kusoma ujumbe ule."
Maneno ya kwenye barua yalimuumiza sana mfalme na hakutaka tena kutuma watu wamfatilie binti yake, aliamua kuacha afanye kitu anachoona ni sahihi kwenye maisha yake.
***************
Masaa mawili yalikuwa yameshakatika na sumu tayali ilikuwa imeshatengenezwa na kuwekwa kwenye chupa maalumu,
Baba Amma alimpatia General sumu ile na kumfanya amwachie binti yake.
"Unabahati sana kuwa hai mpaka sasa ivi", Nzegi alimwambia Amma kisha wakatoka eneo lile
"Mwanangu unatoka damu"
"Hapa umi sana ila namuonea huruma huyo mtu anaye enda kupewa iyo sumu mpaka sisi tu tulio tengeneza ndio tunaweza kumtibu"
"Ni kweli unachosema na hapa tungekuwa tunamjua basi tungeenda kumsaidia najihisi mwenye hatia ya kuua mtu kwa utalamu wangu mwenyewe"
General na Nzegi wakiwa njiana baada ya kutoka kwao Amma,
"General sio kwamba tungeenda kuwamaliza kabisa moja kwa moja"
"Hapana, lengo letu sisi afe Mfalme tu kumbuka na sisi tunataka kile kiti tukianza kuua raia tutamwongoza nani???".
"Sawa general"
"Hapa sasa ana hitajika mtu wa kuipeleka hii sumu na mwenye ushawishi mkubwa kwa wapishi wa jumba la kifalme ndio mana namtaka Prince feki aje hapa afanye hii kazi"
Mipango yote ilikuwa tayali na walibakiza kidogo tu kukamilisha jambo walilokusudia kulifanya juu ya Mfalme Kojo.
*********************
Wakiwa kwenye maombolezo ya waziri mkuu,
Malikia Andwaa akiwa ameketi na mabinti zake Yanite pamoja na Yanni alifika Cheki au Prince feki na kujichekesha mbele ya Malikia Andwaa ambae hakuonyesha utani ata kidogo zaidi ya kumsihi afate kilichompeleka pale.
Cheki aliona sasa mambo yatabadilika mda sio mrefu.
"Hapa inatakiwa jioni niongozane tu na yule asikari mana hawa sura zao zipo tofauti hawataki mazoea na mimi kabisa au wamesha nishitukia nini??,
Cheki alijiwazia baada ya kuona mabadiliko makubwa kwa Yanite,Yanni na Malikia Andwaa"
Baada ya maombolezo ya mda mfupi mfalme alirudi katika jumba la kifalme akiwa na familia yake,
Alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana hali iliyopelekea kuzimia gafra kwa kuanguka chini,
"Mfalme!!!!!!!!!!!"
"Mwiteni daktari wa kifalme"
Daktari alikuja na hakukuta tatizo kubwa kwa mfalme zaidi ya msongo wa mawazo uliompelekea kuzimia . alipumzika kwa mda badae akawa amerudi kwenye hali yake ya kawaida
******************
Princess Nailet licha ya kuchoka kwa kutembea umbali murefu wa safari na hakuwa mzoefu wa safari ndefu ila hakukata tamaa aliendelea na safari kwa kutumia farasi wake ya kuelekea katika ufalme wa ADELI.
"Nakuja Yao najua sijawahi kukutamkia neno nakupenda lakini nipo njiani nakuja kwa ajili yako,
Ni mapenzi ya ajabu aliyokuwa nayo Princess Nailet kwa Yao licha ya kumfahamu kwa mda mfupi tu lakini aliteka sehemu kubwa ya moyo wake....ITAENDELEA.
Mfalme Tengu atafanya maamuzi gani baada ya Princess Nailet kuondoka katika jumba la kifalme???,na je? Nailet atafanyikiwa kumpata Yao sehemu ya 19 inamajibu zaidi hii si ya kukosa ndugu msomaji
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni