NAKUPENDA BILA MIPAKA 121 - 130 SEASON THREE
:121
Nilishtushwa na maumivu yake kabla sijafanya kitu, mama akawa anaingia, nikamzuia mama, mama alinitazama kisha Dorice, nikamuonesha mama Ishara asiseme kitu na badala yake atoke.
Mama yangu ana upendo sana, alitii na alitoka bila kusema kitu. Mimi taratibu nilianza kuita “Dorice, Dorice rafiki yangu, Dorice tafadhali, usilie sasa amka uniambie nini shida.”
Dorice huwa mcheshi sana, mchangamfu sana, sio mtu wa unyonge lakini siku hii nashuhudia akili kwa maumivu sana. Alinikumbatia kwa nguvu akilia. Nilimkumbatia kwa upendo nikimtaka aache kulia.
Tulitumia muda kiasi chake, tulitumia muda kubembelezana. Na aliponyamaza nilimtazama na kusema “Sijawahi kuona ukiwa katika hali kama hii, sijawahi hata kusikia unalia au una huzuni iliyopitiliza namna hii.
Tafadhali nakuomba sana, nakuomba niambie nini kinakusumbua. Mara zote upo hapa na mimi, na sasa upo hapa husemi nyumbani kuna nini, nini unapitia. Dorice sisi ni familia, niambie tafadhali.”
Katika hali ya kunishangaza, hali ya kunipa maumivu zaidi neno la kwanza kwa maumivu alisema akinitazama machozi yakatoka “natamani kubadilisha mama, au nisiwe na mama kabisa.”
Nilishangaa, nilishangaa sana hata nikasema “unaongea nini Dorice, Unaongea nini dada, eemh ina maana una maanisha hiko unacho kiongea.”
Alifuta machozi, akalia na kusema “mama yangu ni mama wa ajabu sana, mama asiye na shukrani hata kidogo. Mimi napambana sana, napambana sana Nazwi lakini unaona hata nina kitu cha maana mimi, sina, sina cha maana.
Mama yangu hata aingie chumbani aone chupi mpya atanisimanga, atafoka akisema “binti una roho mbaya sana wewe, unanunua vitu wakati hapa nyumbani huna unachofanya, hufanyi lolote kisa wewe ndiyo una kazi ya maana au mbona mbinafsi roho mbaya tu.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:122
Wakati hapo yeye mwenyewe ana harakati zake lakini mimi ndiyi ninunue chakula, umeme ukiisha hata niwe kazini nitapigiwa simu, bill ya maji mimi, chumvi na kibiriti ni mimi, hata mtu aumwe kichwa panado ili mradi miatano ya panado itoke kwangu huyo ndiyo mama yangu. Hana huruma na mimi hata kidogo, hanihurumii mimi kabisa hataki kuniona naendelea wala nashika pesa.
Mama yangu kila baada ya siku mbili anaomba pesa, kila wiki anaomba marejesho, kila mwezi anaomba mtaji. Ulifika wakati mimi nilikuwa sasa naanza maandalizi nihame nyumbani. Alipiga kelele usiku ule sidhani kama hakuna ambaye hakusikia. Akanisema mimi nina roho mbaya, ninatelekeza familia, mbinafsi, nina roho ya kichawi na mengine mengi.
Mimi ni kama mume mule ndani, alifikia hatua ananiibia pesa zangu nikiweka ndani. Nikaanza kuficha kwa simu pesa zangu lakini mwani inasaidia kitu. Pale unapomuona mama ana madeni, vikundi kama vyote, halafu huko mimi ndiyo mdhamini wake mkubwa tu na anaringa akisema “binti yangu ana pesa atalipa tu.”
Niulize mimi hizo hela mama anapeleka wapi, mimi sijui, sijui mama anafanyia nini pesa, sijui mama anapeleka wapi pesa, sijui mimi zaidi ni ananitesa na kuninyanyasa huku mimi nikiwa sijui kabisa pesa zake yeye anapeleka wapi, na biashara gani anafanya ambayo hata umpe laki leo, siku mbili baadaye ataomba pesa ni kama pepo, pepo firisi rafiki yangu.
Umri unaenda na sijui nafanya kazi kwaajili gani. Najitahidi kucheka lakini wapi, siwezi kabisa.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:123
Unajua nini kimetokea Nazwii, huwezi kuamini. Mama yangu ameanza kuomba pesa mpaka kwa mwanaume wangu. Sikuwa najua hilo, lakini siku moja mpenzi wangu aliniuliza “mnaishi vipi nyumbani na mama ana kazi gani?”
Nilimtazama na kwa upole nikajibu, unajua aliniambia nini?, aibu rafiki yangu, aibu aliniambia “Dorice mama yako anaomba sana pesa, anaomba pesa mpaka nimechoka.”
Nilijikuta nimeishiwa nguvu, nilijisikia aibu kuliko kawaida, nilihisi kukata tamaa machozi yalinitoka.
Nilipomtazama aliniambia “sijakwambia kwa nia mbaya. Ongea naye. Sasa mimi nipo na wewe, sio yeye hata wewe huombi pesa namna hii.”
Nilizidi kuumia, sikuweza hata kuaga, niliondoka na maumivu.
Nilipofika nyumbani, moja kwa moja nilimfuata mama nikauliza nikilia “kwanini unanifanyia hivi, kwanini unanitesa, kwanini hunipendi mama, kwanini unanivua nguo mpaka kwa mwanaume wangu mama, hivi kweli wewe ndiyo unanifanyia hivi.”
Mama alinitazama akisema “wewe pesa huna unataka nidhalilike mimi, eenh unataka nichekwe. Yeye si mkwe wangu, wacha nimuombe yeye. Ndiyo unakuja hapa unalia hivi wewe binti una akili wewe.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:124
Nilimwambia kwa huruma “mama unaniumiza, unafanya mambo utadhani mimi sio binti yako, kuna muda natamani nikimbie niende mbali kabisa na wewe.”
Akacheka akisema “unafikiri nina haja na wewe, nenda popote, nenda unapotaka.Jichimbie popote, lakini mimi natamani upotee hata sasa.”
Nilichoka, nilichoka mimi. Sasa unafikiri mwanaume wangu ananipenda kama zamani, mpaka mimi nimtafute, nimuanze na simchukii ni haki yake maana mtu unajiuliza kama hii ndiyo familia hapa bado sijaoa nikioa itakuwaje.Namuelewa sina la kufanya mimi.Naenda naye tu hivyohivyo.
Kuna muda watu wa madeni wananipigia mimi mpaka naogopa namba mpya, kuna muda wanakuja nyumbani pale wanabeba vitu aibu aibu.
Sijui mama yako kama anajua ana rafiki wa hivi sidhani kama angeendelea kuwa rafiki yake maana mama yako ni mama mzuri sana. Natamani mama angekuwa kama mwenzie.
Hapa ninavyokwambia, pamoja na yote, nilikuwa nikisikia kwa ndugu zangu na majirani huko mtaani kuwa mama yangu ana penda vijana wadogowadogo kuwa nao kwa mahusiano, Nazwi juzi nikiwa natoka kazini nafika nyumbani nakutana na kijana anatoka chumbani kwa mama hata kwangu ni mdogo.
Nilishangaa hata na wao walishangaa, nadhani unamfahamu huyu kijana anaishi hapo anaitwa Mesha.”
Nikatoa macho nikisema “yule handsome boy?”
Dada alilia akisema “upo sahihi, ona mama yako anachofanya. Mbele ya ndugu zangu, familia na unaambiwa sio huyo tu kifupi mtaani tupo uchi. Nililia sana, nilishindwa kukaa nyumbani kabisa.Moyo wangu una maumivu, una mengi ya kusema, natamani sijui nifanye nini.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:125
Akachukua simu, ananionyesha meseji mama yake anatuma, mama anafoka kwenye meseji. Anatukana nasoma mpaka namtazama Dorice nikisema “una hakika huyu ni mama?”
Alinitazama na kuniambia “unafikiri naweza msingizia mama yangu, siwezi, unaona hivi nalia, kwasababu natamani mama yangu angekuwa mama mzuri, angekuwa ananiombea, ananitia moyo, ananipambania kama mama yako anavyokupambania wewe na binti yako.
Mama yangu mimi sio mama ambaye hata nikiumwa bado niliyepo kitandani ndiyo naambiwa nitoe pesa ya kula au dawa huyo ndiyo mama yangu. Kuna muda natamani angekufa, haya machozi yasingekuwa yanatoka hivi.
Mimi hakuna siku nimeingia nyumbani sijali. Nacheka tu sina la kufanya naumia sana, moyo wangu una maumivu makali hata ule upendo wa mtoto kwa mama sina mimi, sina kabisa.
Nazwi mama anafanya jambo baya zaidi, ananifanyia michezo mimi nisiolewe, nisitoke nyumbani, na nimsikilize yeye kwa kila kitu.
Nilitazama Dorice na kusema “sijaelewa, una maanisha nini?”
Alilia akisema “mama yangu mzazi ananiendea mimi kwa waganga, ananipumbaza akili, ananifanyia ushirikina ili azidi kunifanyia haya anayofanya na nisihoji kitu. Hivi unanielewa, mama yangu mzazi ananiroga mimi, ananiroga nisifanikiwe unanielewa Nazwi.”
Nilishika mdomo na kusema “shhhhhhhhhh!!!, wewe Dorice unaongea nini mama yako anawezaje kufanya hivyo eenh?”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:126
Alitikisa kichwa akasema “hata mimi sikuwa naaamini, sikuwa naamini, nikatetemeka, hata nilipata tumbo la kuhara kwa mshangao. Mama anapenda kuchukua viatu vyangu. Sasa hiyo siku kiatu nimenunua nivae yeye keshabeba.
Alitoka, hivyo mimi nikaingia chumbani kutafuta. Ile kuhangaika huku na kule natazama chini nikaona kiatu kimoja, kuinama nivute kingine, naona boksi chini ya kitanda chake. Ikabidi nivute lile boksi nikashuka kuona kuna chungu na udi.
Nilitetemeka nikijiuliza “kwani mama yangu ni mchawi?”
Basi nikatoa ule udi, nikaona karatasi, nikalichukua, kukunjua naona jina langu kwa wino mwekundu. Nilitetemeka nikilia. Nilianza hata kupata maumivu ya tumbo nikiwaza nini kinaendelea.
Ndiyo nikamfuata rafiki yake wa karibu sana nikilia maana huyo wanafanana akili. Ndiyo akanielezea kwa upana kinachoendelea, niliogopa, nilitetemeka, na sikuweza mwambia mama chochote, mpaka leo hii, rafiki yangu unaona huyu ni mama, sijui nifanye nini, sijui niende wapi sielewi unaweza kuhisi natania lakini naona nahitaji msaada kuliko yeyote.”
Dorice alikuwa analia sana, naishi naye siku zote hizi kumbe anapitia mambo magumu na mabaya namna hii kutoka kwa mama yake mzazi. Nilijisikia kuumia, nililia pamoja naye.
Mimi na mama yangu tunashirikiana kupunguza umaskini, mwenzangu mama yake anamkandamiza azidi kuwa maskini mpaka anaroga. Hii inaumiza, wapo wazazi hawana maana kabisa kama uwe huna tu ujue sina.
Mzazi ndiyo anakudidimiza namna hii, inaumiza, inatesa, inasumbua sana. Binafsi ilinifanya nimkumbatie rafiki yangu kwa nguvu nikimtaka atulie. Ni kama alikuwa anatafuta pakutoa fundo lake.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:127
Alilia kwa uchungu na maumivu sana. Alilia nikamuhurumia. Halafu baada ya hapo sasa, nilimtazama na kusema “la kufanua unalo rafiki yangu, unalo la kufanya.”
Aliniuliza kwa upole “nifanye nini rafiki yangu?”
Nilitabasamu na kusema “mimi sijui sana ila mama Gallen aliniambia ukikutana na Mungu mambo yanabadilika. Si unamuona kaka Baraka sasa hivi, hivyo ndiyo mambo huwa kwanza unatakiwa kujikomboa kwenye huo uchawi wa mama yako na kisha sasa unatakiwa kumuonyesha kuwa umebadilika.
Jifunze kusema sina, wewe unayoyafanya sio wajibu wako, sio kitu wewe unapaswa kufanya, sio kazi yako wewe. Rafiki yangu, sio lazima ukae hapa, kaa mbali na mama. Najua hii hata mimi itanisumbua lakini hama hapa, nenda mbali, anza upya, usiwasiliane naye, wala usitake kujua mambo yake.
Sio rahisi ila ni njia ya kupona haraka. Nakupenda na nataka ufanikiwe, najua inaumiza lakini haikubaliki. Rafiki yangu, unaonaje tukawa karibu na Mungu, tukaanza maisha upya, tukawa watoto wake na kusahau haya mambo.
Najua unaumia ila sijui niseme nini. Na pengine ongea na mama pia ni mtu mzima atakuwa ana lolote la kusema au kushauri. Usikae na mambo sisi ni familia rafiki yangu.”
Rafiki yangu alinikumbatia kwa upendo akisema “walau nimeongea na wewe kidogo nafuu, vipi muanko amekutafuta?”
Nilijikuta nacheka nikisema “una shida gani binti, mbona mkorofi lakini hata kwenye maumivu unawaza ujinga. Ungejua anasumbua mpaka nimezima simu.
Unajua rafiki yangu nawaza mambo mengi, naona kabisa sitaweza kufanya kazi tena kwa upendo ule nitakuwa kama najilazimisha na kuishi kwa wasiwasi mama asipatwe na chochote. Mimi naona tu niangalie mambo mengine ya kufanya.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:128
Kabla hata hajajibu mama aliita “Dorice, wewe Dorice njoo uchukue chakula ana dawa huyo.”
Dorice alisema akiinuka “nakuja mama, kumekucha sasa kumekucha.”
Nilimtazama kwa huruma, ana maumivu sana. Hakuna mambo yanaumiza kama ukitendewa na mzazi. Anajikaza tu ila sio kawaida. Inaumiza sana.Namuonea huruma maskini.
Alivyo mpole na mwenye upendo. Kuna wazazi jamani hivi inakuwaje mpaka unaroga mtoto wako badala umuombee. Hii ni mbaya sana.
Mimi naendelea vizuri ni nguvu tu ila siumwi. Alikuja na chakula tukala vizuri tukitaniana na baada ya hapo akaniuliza “eenh kuhusu suala la Mungu, tunafanyaje?”
Nilitabasamu nikisema “hapa mchungaji ni Baraka ndugu yangu mimi sijui kitu chochote.”
Tulicheka akisema “mambo yanabadilika leo hii Baraka ndiyo kiongozi wetu wa njia nzuri.”
Tulifurahia sana.
Lakini muda nao ukazidi kusogea. Dorice alilala mapema sana. Mimi nikabaki tu kitandani nawaza hili na lile. Kwenye haya maumivu yote nilipitia. Jambo la kunipa amani na furaha moyoni ni mimi kuacha kazi na kutafuta namna nyingine ya kuishi. Hivi ndiyo niliamua. Niliamua nitaacha kazi.
Nilikuwa kila nikikumbuka nakosa raha. Hii ilinifundisha kitu kwenye maisha. Sitaki kusema kuwa Mr Gallen ni mbaya hapana. Yule ni mama yake pengine ningekuwa mimi pia ningefanya alivyo fanya, au ungekuwa wewe labda ungefanya zaidi.
Binadamu tuna tabia ya kujitazama sisi tu. Hatuna desturi ya kutaka kujua tatizo, nini kimetokea, nini kinaendelea sisi ni kujipendelea tu.Hata uwe mwema vipi, watu waliowahi kukupigia makofi, watu waliokuwa wanakushangilia wanaweza kukugeuka haraka sana na ukawa kituko mbele yao. Hawa ndiyo binadamu na hii ndiyo asili ya binadamu sisi.
Jifunze kupenda watu na kutoruhusu wakuumize. Yaani mtu anaweza kuwa sio mbaya, ila ukaribu na mazoea uliyoruhusu kati yenu ndiyo yanayoweza kuwaumiza.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:129
Sikuwahi kutegemea nitafokewa namna hii kulingana na nilivyokuwa naishi na mama. Nilitakiwa kuwapa nafasi yao, kwamba wao ni matajiri zangu na mimi ni mfanyakazi wao hivyo hata wakifanya nini nisiumie badala yake nikaridhika na mazingira niliyoona yanafanyaa kwangu. Kumbe nilifanya tofauti.
Ndiyoo, kabla hatujaendelea, tafadhali ukisoma hii simulizi tofauti na hapa instagram kuanzia sehemu ya kwanza jua huyo ni mwizi anakuuzia. Mwandishi halali ni agathadastorywriter instagram.Naipost kwa raha zangu sio kwa kuibaiba hiyo ni tabia mbaya kama wewe mwandishi andaa kazi kwaajili ya shabiki zako. Nina vitabu pia guys guys😂😂. Na Ukikutana na Tangazo la vipodozi huyo ni mdhamini wetu tafadhali like, comment, ili tangazo lake lifike mbali na wengine wadhamini kazi kwa gharama nafuu. Tuendelee sasa maana kuna mtu kanuna, eenh wadhamini muhimu😂😂.
Niliamka Usiku usiku, nikachukua karatasi kwenye sanduku langu maana huku ndani nina kila kitu. Wakati ule Natafuta kazi nilikuwa naandika sana hizi barua mbona.
Nilianza kuandika Tena vizuri kabisa, niliandika huku nalia, naumia kwasababu siku ya kwanza naambiwa kuhusu hii kazi nilifurahi sana, ilikuwa Kama ukombozi kwangu halafu Leo kirahisi tu nashindwa. Sasa inabidi nianze upya kupambana na kuhangaikia kupata kazi sehemu zingine kitu ambacho sio rahisi.
Nikachukua bahasha nikaiweka vizuri Kisha nikaweka kwa pochi yangu.Siku iliyofuata asubuhi niliamka, nilikuta tayari mama ameamka.
Nilimsalimia mama yangu naye aliniambia “mwanangu, unaenda wapi unajua haupo sawa?”
Nilitabasamu na kusema “Hapana mama, naendelea vizuri kabisa. Nafika kazini Mara moja halafu narudi.”
Mama alinitazama na kuniuliza “eenh vipi umeongea na mwenzio?”
Nilimtazama na kusema “hili mama tutaongea nikirudi. Ni muhimu sana.”
Mama aliniambia “uwahi basi mwanangu, usichelewe sana.”
Nilitabasamu tu.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:130
Nilikuwa natembea mwenyewe nawaza nifike huko sikutani na yeyote zaidi ya mlinzi naondoka zangu. Kwani hata nimefika mbali, Muanko ananipigia, amenipigia sijapokea.
Yaani nasema wewe mbona bado Subiri ukutane na barua ya kuacha kazi ndiyo utajua sasa Mimi nini namaanisha. Wewe si tajiri, unalipa watu mshahara, basi utapata nesi mwingine mimi niache si sina akili. Najisemesha, makasiriko yamenijaa.
Nilipanda zangu dalala, akanitumia ujumbe “Nazwi, am coming!”
Natamani nicheke, am coming wapi mimi ndiyo am coming huko kwenu, unanitisha mimi. Wewe subiri hapo.
Nikaona hii nisimezee mate barua yangu ikachelewa kufika. Nikamtumia ujumbe “usijali, nipo njiani ndiyo nakuja huko.”
Alijibu haraka, “upo wapi nikusubiri kabla sijaenda hospitali?”
Kumbe mama bado yupo hospitali jamani, lakini hayanihusu mimi.Mimi nikae mbali na hii familia nisije pata tatizo nikashindwa kujielezea.Nikawa tu naona nikafanye tukio langu. Basi nikafika mpaka kituo changu cha mwisho, nashuka tu Baraka Boda huyu hapa.
Na vile sina hata nguvu mwilini nikasema “nichukue tafadhali nipeleke pale kazini.”
Baraka alinitazama na kutabasamu, halafu akaniambia “umepoa sana sister kwema?”
Nilimwambia kwa upole “naumwa kidogo Ila naendelea vizuri.”
Akaniambia kwa upole “pole sana dada ake, pole sana.”
Nilishukuru sana, alinichukua pale mpaka kwa Mr Gallen.
Nilibonyeza kengele pale huku nikimwambia Boda anisubiri. Basi nilipokuwa nafunguliwa, mlinzi alinikaribisha, Mimi nikamwambia “hata sikai, nimeleta hii barua hapa utampa Boss.”
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni