MFALME KIPOFU 21 -- 22
Whatsapp.............0748697173
Ilipoishia sehemu iliyopita........
Malikia alichanganyikiwa baada ya kusikia maneno yale ya dakitari Malikia aliita walinzi na ,kuwapa maagizo ya kuwakamata matabibu wote......
ENDELEA NAYO.......
Walisubili pakuche msako uanze wa kuwakamata matabibu wote katika mji wote ADELI
Chike pamoja na rafiki wa Nzegi walijadiliana namna ya kufanya ili tarifa ziwafikie General na Nzegi,
"Mimi naona tusubiri kesho tukitoka sasa ivi hapa itaonekana kama sisi ndio tumepanga"
"Upo sahihi kabisa tutawapelekea tarifa kesho asubuhi na mapema",Cheki aliongea.
Cheki na Mlinzi yule walikubaliana tarifa zile za matabibu kutafutwa na kukamatwa watazipeleke kesho mapema asubuhi.
************
Upande wa Princess Nailet akiwa amechoka siku iyo baada ya kumtafuta Yao na Mama yake mlezi siku nzima mpaka usiku unamkuta pale aliamua kukaa na kupumzikaa,
Akiwa amekaa pale kutokana na uwepo wa giza alimuona kijana kwa mbali aliyekuwa akitembea kwa shida na alikuwa akielekea sehemu yenye kolongo kubwa mbele yake.
"Huyu haoni mpaka anelekea kwenye kolongo??au atakuwa na matatizo ya akili???.,Princess Nailet alijiuliza.
Alivyoona kijana yule amelikaribia lile kolongo alikimbia kwa kasi na kumsukuma pembeni.
"Unaakili wewe au umechoka kuishi mpaka unataka kujiua???"
"Kwani wewe nani??"
"Heeeeh Yao!!!!! kumbe ni wewe????"
Princess Nailet hakuamini kumuona Yao maeneo yale mtu ambae alimtafuta karibu kutwa nzima na hatimae anakutana nae kwenye mazingira asiyoyatalajia.
Alimukimbilia na kwenda kumkubatia Prince Yao ambae alibaki tu kumuuliza kuwa ni nani aliyemkumbatia??.
Palepale Lindwe pamoja na rafiki yake walifika na kukuta lile tukio la wao kukumbatiana, na Lindiwe alishangaa sana kumuona Princess Nailet maeneo yale.
Princess aliwaeleza amekuja ADELI kwa ajili yao, nao hawa kusita kumpokea na kumkaribisha katika makazi yao ila Prince Yao alikuwa na hasira kwa tarifa alizopewa za kitendo cha wazazi wake kumpeleka nchi za mbali.
**********
Ni asubuhi na mapema kamata kamata ilianza kwa yoyote yule aliyekuwa anafanya kazi ya utabibu katika ufalme wa ADELI.
Upande wa binti Amma akiwa hana hili wala lile alishangaa asikari wa kifalme wamewasili kwenye makazi yao,
"Karibuni,tuwasaidieni nini??"binti Amma aliuliza
"Sio kila anayekuja hapa anahitaji kutibiwa sisi leo tumekuja kuwatibu nyinyi",asikari aliongea.
"Kututibu sisi, kivipi???"
"Aise kamateni huyu binti hatuna mda wa kusubiri".
"Mbona mnamkata binti yangu???"
"Na wewe umejileta, aya kamata na huyu"
Hawakutaka maneno mengi walikamata karibu kila mtu aliyekuwa na chembechembe ya utabibu na kuwapeleka katika jumba la kifalme.
******************
Princess Nailet akiwa na Prince Yao wamekaa mahali,
"Princess kwanini unapoteza mda wako kunijali mtu ambae sina thamani yoyote ile?"
"Hapana usiseme ivyo wewe unathamin kubwa mno kwenye maisha yangu".
"Una mana gani kusema ivyo??"
"Nakupenda Yao nataka uwe baba wa watoto wangu".
Prince Yao alishangaa kusikia neno lile kutoka kwa Princess Nailet na licha ya upofu wake haikumaanisha kwamba hajui kama kwenye hii dunia hakuna kitu kinachoitwa mapenzi alifahamu na hakuamini kama kuna mwanamke atakaye mpenda kutokana na hali aliyonayo.
"Princess, huwezi kuishi na mimi mtu ambae sioni nitakuwa mzigo kwako naomba utafute mtu mwingine anayeendana na hadhi yako".
"Yao, ata mimi napenda kuwa na mizigo napenda uwe mzigo wangu na niishi na wewe mpaka mwisho wa uhai wangu"
Princess hakutaka kuipoteza ile nafasi ya kueleza hisia zake kwa Prince Yao ni namna gani anavyompenda na Prince alimuomba ampe mda kidogo ili atafakari kwa kina zaidi juu ya jambo lile.
*****************
Tarifa zinawafikia General na Nzegi juu ya mfalme kuwa katika hali mbaya na wanapongezana kwa kazi kubwa waliyoifanya,
"Safi sana Cheki wewe rudi katika jumba la kifalme ukashirikiane na mwenzako kutupa tarifa huku",
Alikuwa ni Cheki au Prince fake aliyewaletea tarifa zile General na Nzegi.
"Alafu nilitaka kusahau kuwapa tarifa mhimu asikari wa kifalme wana wakamata matabibu wote wa ADELI wakafanyiwe uchunguzi ni nani aliyetengeneza ile sumu tuliyompa mfalme".
"Mbona hukutuambia mapema shiiiiit!!!!",
General alichomoa upanga wake na kuanza kukimbia kwa kasi ya ajabu Cheki na Nzegi waliunga tela kumfata anapoelekea.
Safari ya General iliishia yalipo makazi ya Amma pamoja na baba yake ila alikuta kuna ukimya wa hali ya juu.
"Haitakiwi waishi hawa kamwambie mlinzi afanye afanyalo wauwawe kabra hawajatoa siri......ITAENDELEA..
BAADA YA HII KUNA FARASI MWEUPE 🦄🦄🦄 NA IPO FULL kwa Tsh 1000 tu unajipatia Hii ni🔥🔥🔥 NJOO TUPANDE FARASI MWEUPE PAMOJA.
Mambo yanazidi kuwa matamu Amma yupo kwenye hatari na Princess ameshaonyesha hisia zake kwa Prince Yao. tukutane sehemu inayofata..
[12/12/2025, 6:40 AM] zooper simulizi2: Story.....................MFALME KIPOFU
Mtunzi...................Zooper
Sehemu...ya........ 22
Whatsapp.............0748697173
Ilipoishia sehemu iliyopita............
Safari ya General iliishia yalipo makazi ya Amma pamoja na baba yake ila alikuta kuna ukimya wa hali ya juu.
"Haitakiwi waishi hawa kamwambie mlinzi afanye afanyalo wauwawe kabra hawajatoa siri........
ENDELEA NAYO.......
Cheki aliondoka kuwahi katika jumba la kifalme ili akampe tarifa mwenzake anayetakiwa afanye kazi ya kuwaua Amma na baba yake mapema kabra hawajatoboa siri yoyote.
Wakati Cheki yupo njiani anakuja katika kasili la kifalme,
Mabinti wa kifalme wote walikuwa kwenye majonzi makubwa juu ya Mfalme wao kuwa katika hali inayotishia maisha yake,
"Nyamaza mdogo wangu,nitamtafuta mtu aliye tengeneza hii sumu na kumpatia baba yetu lazima atalipa",Yanite aliongea huku akimkumbatia mdogo wake aitwae Yanni.
Malikia hakuwa na la kusema mbele ya binti yake mkubwa baada ya yeye kutamka maneno yale.
"Malikia tayali matabibu wote wamesha kamatwa na tunasubiri utaratibu wa kuanza kuwahoji".
"Ivi wewe mjinga ety, mnataka mpewe utaratibu gani?, kwani hamjui sheria za kifalme zilivyo??,
Wote wapigwe mpaka waongee ni nani aliyetengeneza iyo dawa".
Amri ilitoka kutoka kwa Malikia na asikari alitoka kwenda kutekeleza wajibu.
Hatimae Cheki anafika katika jumba la kifalme na kukuta watu wakitandikwa mmoja baada ya mwingine mpaka apatikane aliyetengeza sumu ya kumuua mfalme, cheki anaelekea kwa mwenzake wanaye shirikiana naye,
"Aise mambo sio mazuri huko"
"Kwanini???"
"General kasema wale watu walio tengeneza sumu inatakiwa wafe wakiwa humuhumu ndani. kabra hawajatoboa siri".
"Mimi nawauwaje sasa huoni walivyo wengi pale".
"Wewe ni asikari unajua mbinu zote tumia mbinu zako kuwaondoa duniani mimi tarifa nimekufikishia".
Cheki aliondoka baada ya kumfikishia tarifa mwenzake na kumuacha akiwatazama Amma na baba yake jinsi ya kuwaua wakiwa wanasubiri zamu yao ifike ya kwenda kuadhibiwa na kuhojiwa.
******************
"Lindiwe unahabari za kinachoendelea huko?????",
"Habari gani tena nasikia hali ya mfalme ni mbaya sana amepewa sumu na haijulikani nani kampa sumu".rafiki wa lindiwe aliongea na kumfikishia tarifa zilizomwacha mdomo wazi na ata Prince Yao nae alikuwa maeneo yale akiwa pamoja na Princess Nailet.
Damu ni nzito kuliko maji ndicho kilichotokea kwa Prince Yao alivyosikia yale mazungumzo hakuta kupoteza mda tena,
"Mama naomba unipeleke nikamuone Mfalme",
"Mfalme!!!!!!!!!!!"
Princess Nailet alishangaa ila Lindiwe alimsimulia kiufupi tu na hii kumfanya asiamini kama Prince Yao ni mwana wa Mfalme.
"Ni sawa nitakupeleka lakini ni hatari sana na ata kwenye mlango wa siri sizani kama tutapata msaada wa mtu kutufungulia ili tuingie ndani".
"Mama wewe twende nataka nikaongee na Mfalme",Prince Yao aliongea.
Lindiwe aliamua kutimiza ombi la Prince Yao la kumpeleka katika kasili la kifalme lakini pia Princess Nailet aling'ang'ania kwenda ili akajihakikishie kama Prince Yao ni mtoto wa Mfalme kweli licha ya Lindiwe kumzuia.
******************
Asikari waliotumwa na mfalme Tengu wanafanyikiwa kufika katika ufalme wa ADELI na kazi ya kumtafuta Princess Nailet inaanza ili wamrudishe kwa mfalme wao.
*******************
"Sasa hapa natumia njia gani kwenda kuwaua",
baada ya kuwaza kwa mda mrefu alipata wazo ambalo aliona ni sahihi kulifanya ili aweze kumuua Amma pamoja na baba yake na siri ibaki kuwa upande wao tu.
Kila tabibu alijuta siku iyo kwanini alichagua kufanya ile kazi, watu walikuwa wanapigwa na wengine mpaka kuzimia kutoka na mateso makali.
"Baba mimi naona sio sawa kwa hichi tunacho kifanya watu wanateseka kwa makosa yetu sisi".,Amma aliongea.
"Mwanangu hakuna njia nyingine ya sisi kufanya zaidi ya kunyamaza kimya, naomba unyamaze wakikusikia tu nitakukosa binti yangu".
"Nyie mnaongea nini hapo???"
Asikari aliongea kwa ukali baada ya kuwaona wakishauliana,
"Subrini zamu yenu ifike nakuja kuwatesa mwenyewe".
Vitisho vya asikari yule viliwafanya wakae kmya na kutii amri.
Asikari alipata njia sahihi ya kuwaua Amma na baba yake,
"Mimi mjinga kabisa mbona sikufikilia hii njia mapema ningekuwa nimeshamaliza kazi zamani tu".
Kwakuwa walikuwa wamepanga foleni ya kusimama, na mlundikano wa watu ulikuwa mkubwa basi alichomoa kisu kidogo ambacho ni ngumu mtu kukiona nakuanza kutembea alipo Amma na baba yake.
Amma akiwa hana hili wala lile asikari alimsogelea na aliandaa kisu ila baba yake aliona lile tukio,
Asikari yule alichoma alipo Amma lakini Amma alijikuta yupo chini na kisu kile kikamchoma baba yake aliyeanguka chini,
Asikari alijichanganya kwenye umati wa watu ili asikigundulike baada ya kufanya tukio.
"Baba!!baba!!",Amma aliita baada ya kuona baba yake yupo chini na akiwa na jeraha.
"Utanisamehe binti yangu kwakukuacha peke yako ila naomba nikuambie kitu cha mwisho tu"
"Baba usiongee tafadhalii, msada!!msada!!msada!!,
Watu walisogea kuangalia namna ya kumsaidia.
"Nisikilize mimi kwanza umeshachelewa binti yangu ninachotaka kukwambia ni kwamba ile ndoto ya
"CHUKUA MAJANI MAWILI KAYANYUNYIZIE MAJI YA MTO ADEYU, KISHA JANI MOJA MUWEKEE KATIKA JICHO LA KULIA NA JINGINE MUWEKEE KATIKA JICHO LA KUSHOTO",
mana ya iyo ndoto yako ni kumtibu mtu kipofu kwa kufata hayo maelekezo, nisamehe binti yangu sikutaka kukwambia sababu ungekuwa mbali na mimi kwa kumtafuta mtu kipofu,
ivyo kuanzia sasa ivi utakuwa mwenyewe naomba umtafute mtu kipofu umtibu ili ndoto isiwe inakusumbua.
Maneno yale yalipenya katika masikio ya Amma na baadhi ya watu waliokuwepo pale walisikia mazungumzo yale walikuwa wakitazama tu badala ya
kutoa msaada,Babaaaaa.............ITAENDELEA.
Kwanini Amma amepiga kelele je? amepata msaada au na yeye amechomwa kisu tena na asikari wa General na vip kuhusu Lindiwe atafanyikiwa kumpeleka katika jumba la kifalme Prince Yao, tukutane sehemu inayofata
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni