CHAGUO LA MOYO ❣️ 8 -- 10
SEHEMU YA 08
"Kwanza haoni ajabu kukufukuza,na akisema hakutaki ujue hakuna was kukutetea hata mama hataongea .... kwaiyo muangalie hivyo hivyo kauli yake moja tu inakuondoa...........
Nicole aliposema hivyo nilimuogopa sana Berat
"Ndio yuko hivyo toka utotoni au kaanza ukubwani"nilimuuliza Nicole........
"Toka utotoni yuko hivyo na ndio maana wanawake wanamkimbia kwa sababu ya ukauzu wake".............
"Mmmmh haya"
"Ndio hivyo kuwa makini usiseme sijakwambia,huyo Johari anajifanya kichwa mbovu ila mbele ya Berat anakuwa sisimizi"
Basi Nicole aliondoka na mm nikapanda juu ili nikachukue nguo maana huwa anafunga chumba chake........nilifika nikagonga lakin sikufunguliwa niligonga tena wala hakuitika .......basi nikawaza atakuwa hayumo chumbani. Kwaiyo nikafungua mlango ili nichukue hizo nguo..........😳nilitoa macho baada ya kukutana nae akiwa ametoka bafuni huku amejifunga taulo kiunoni sasa badala nirudi haraka nikabaki namshangaa alikuwa na kifua kipana huku tumboni anakama matuta hivi ............. sijui kwasababu ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mwanaume akiwa hajavaa shati ..........
"Ni Nani aliyekupa ruhusa ya kuingia chumbani kwangu bila hodi 😡"aliongea huku sura yake ikionesha kukasirika
"Na bado umesimama "
Yaani huyu kaka akikuangalia unaweza kusema anaona dhambi zako zote anamacho makali balaa .........haraka nikataka kukutetea
"Samahani ka........"toka chumbani kwangu"........... aliongea kwasauti ya kuamlisha Mimi ninani nibaki 🏃 nilitoka kwakukimbia.........
Sasa wakati na kimbia nikapamiana na Rahul nikataka kudondoka akanidaka fasta
"Vp mbona unakimbia asubuhi yote hiii"aliniuliza huku akiniangalia usoni
"Aaaa hapana"
"Kuwa makini usjie kuumia sawae na ujiandae mapema"
"Sawa, unaweza kuniachia"nilimwambia maana alikuwa bado kanishika Sasa ile ananiachia tu mr kauzu huyu hapa............😳mara ii kashavaa .....kila kitu hata dakika 3 hazijaisha ......🤔nawasi wasi na huyu mtu
Huyu mama atakuwa alizaa na jini inawezekanaje mtu apake mafuta na kuvaa ndani ya dkk 2 hata hizi 2 sidhani Kama zimefika......... wakati nawaza hivyo alitupita bila hata kumsalimia mdogo wake.........
"Aaa mzoee ndio alivyo tena hakuna mtu mkarimu kama Berat"
"😁😁Hivi unajua mtu mkarimu yukoje au unaongea tu kwanza akikuangalia unaweza kusema anaona dhambi zako zote"
Rahul alicheka sana aliposikia hivyo
"Hamna bhn niamini mm ni mtu wa pekee sana sema hapendi kuongea ".
"Hujanishawishi Wala siwezi kumzoea mtu wa hivyo"
"Kumzoea hutoweza si wewe tu hata waliokuja kabla yako hakuna aliyewahi kumzoea kwanza ukimkosea hana nafasi ya pili anakuondoa mda huo huo, wala hakuna atakae kutetea"
"🥺Duh "
"Ila usiwe na wasi wasi nipo kwaajili yako 😊"
"Umeshasema hakuna wa kunitetea alafu unageuza tena ute upo kwaajili yangu😏"
"Yeah soni.......... kabla kajamaliza aliitwa na Berat( mr kauzu ) "baadae"aliniaga na kuondoka chap niligeuka na kukutanisha macho na mr kauzu uwiiiii huyu kaka anatisha yaani akikuangalia tu unaishiwa nguvu.......nikajifanya naangalia pembeni ....wakaondoka ......Mimi huyo nikaingia chumbani kwake nikachukua nguo na kubadilisha mashuka Kisha nikatoka .......nilienda kwenye chumba chakufulia nikafua na kutoka nje nikaanika ........ nilipomaliza nikaenda kunywa chai mda huo wote walikuwa wameshaondoka tumebaki mm na Johari tu......."unakumbuka nilichokwambia jana ee"
"Aliongea Johari baada ya mm kukaa mezani
"Ndio nakumbuka"
"Vizuri"
Nilikunywa chai Kisha nikaendelea na kazi zingine mida ya saa sita Rahul alirudi na kuniambia tuondoke Sasa nikakumbuka Johari aliniambia nikatae hivyo nikamwambia
"Rahul naona ungeenda mwenyewe tu bado Nina kazi"
"Utafanya kesho"
"Yeah hatakiwi kuondoka hajamaliza kazi kama ni nguo tutamchukulia maan ninajua saiz anayovaa"
Rahul hakuongea neno badala yake alinishika mkono na kuondoka nje
Huku Johari alivimba na kuninyoshea kidole .....😓😓
SEHEMU YA 09
Tuliingia kwenye gari na safari ikaanza
"Sonia"Rahul aliniita baada ya kimya kirefu kupita
"Abee"
"Una boyfriend"
"Boyfriend ndio nin"
"Naamanisha una mpenzi?"
"Hapana"
"Kwanin "
"Sijui"
"Hahaha haya ngoja nisikuchoshe na maswali"
Baada ya mda kadhaa tulifika na tukaanza kuchagua nguo
Nilichagua nguo chache nikihofia kukatwa hela yote
"Nimemaliza"nilimwambia Rahul
"Umemaliza kufanya nn"
"Kuchagua nguo"
Nilivyosema aliinuka na kushika nguo nilizochagua nakukagua moja baada ya nyingine
"We unatani kweli hizi nguo ndio umechagua".
"Zinanitosha"
Anilisogea na kunishika pegani na kusema........."Sonia naomba ukiwa na Mimi uwe huru kwa chochote sawae.... Na ukihitaji chochote usisite kuniambia napenda kukuona ukiwa na furaha so nitafanya chochote kuhakikisha kuwa unafura ".........nilimuangalia tu bila kujibu chochote
"Kaa hapo "aliniambia na kuchagua mwenyewe........alijachugua nguo nyingi pamoja na viatu
"Nimemaliza tunaweza kwenda"
"Unataka kula nn"
"Sijui Johari atakuwa amepika nn"
"Hatuli nyumban kuna mahari nataka tupite"
"Ooo chochote"
"Chochote ndio chakula gani hicho"
"Usijisumbue mm nitakula tukirudi nyumban"
"Sonia nimekwambia kuwa uwe huru kwangu so please usiongee hivyo"
"Lakin kama tukila huku chakula cha nyumban si kita haribikia"
"Anaweka kwenye fridge"
"Sawa"
Tulienda sehemu ya chakula ....... Nilijisikia aibu kwa jinsi nilivyokuwa nimevaa ila Rahul alinionesha tabasamu mda wote .......baada ya dakk kadhaa chakula kililetwa ..... mimi kuona tu mate yakanijaa 😋 ilikuwa 🍕
"Karibu"alinikaribisha Rahul
Nilianza kula
Bila hata kunawa Rahul aliniangalia kwa tabasamu nono na kusema kama ukipenda nitakuleta kila siku
.......mimi mda huo nasikilizia utamu wa 🍕 nikaona nusimjibu ........basi tulikula na baada ya kula tulienda sehemu moja hivi Rahul akashuka mm nikabaki kwenye gari badaa ya kama dakika 20 akarudi na mfuko
"Samahani nimekuweka mda mrefu"
"Haina shida"
"Okay kuna kitu chochote unahitaji au sehemu yoyote unayotaka kwenda?
"Hapanaa"
"Okay so tunaenda nyumban"
Aliwasha gari safari ya kurudi nyumban ikaanza mda wote alikuwa akiongea jinsi gani amefurahi kuwa na mm kwa mda wote huo.......Mimi nilikuwa nikekaa kimya tu maana sikuwa hata na lakujibu
Tulifika nyumban milinzi akapeba vitu kupeleka ndani
"Aaaa peleka chumbani kwa Sonia"
"Mlinzi alipeleka na mm nikaenda moja kwa moja jikon ile nafika hee nilipokelewa na hiyo sura 😡 umerudi ee umekizungusha huko wee saiz ndio unarudi ......... Sasa mda si mrefu Berat anakuja akikuta hujapasi nguo zake safari ya kwenu inakuhusu........uwiiii alivyoongea hivyo nikakumbuka kuwa nilitakiwa kupasi nguo nilizofua haraka nikaenda kuanua na kuingia ndani ili nipasi
"Hey vp mbona unaharaka hivyo mwishoni utaumia" alikuwa Rahul
"Aaa nimekumbuka sijapasi nguo za kaka yako"
"Oo ondoa shaka,na ufanye ukiwa umetulia usije ukaungua ". Yaani huu mda naongea na huyu ningekuwa nimeshamaliza nguo moja lakin niko bz nafanya ujinga"niliwaza na kuondoka wakati napasi Rahul alikuja na
"Acha nipasi mimi usije ukajiunguza kwa haraka zako Kama unakazi nyingine kafanye"
"Hapana asante acha niifanye mwenyewe hili ni jukumu langu"
"Hata wewe ni jukumu langu so niache nifanye"
"Haya kama umeamua"
Nilikaa pembeni huku yeye akipasi na mda huo alikuwa akinipigisha story kama zote
Kwa mda niliofika humu ndani nimemuona Rahul mtu watofauti Sana na wengine
Au wewe unaonaje
Baada ya kupasi nilizipanga nguo kabatini na kutoka
"Naonda kuoga mda wa dinner unakalibia,na I ngekuwa vizuri na wewe ukaenda kuoga Ila ukipenda"
"Sawa asante Sana"
"Karibu"alijibu na kuondoka
Na Mimi nilienda chumbani kwangu na kumkuta Johari akiwa amekaa kitandani huku kamwaga vitu vyote kitandani
"Nilikuonya hukusikia Sasa utanikoma".aliongea na kuondoka
Hee jamani kwani mm nimefanya nn
Nilikusanya vitu nakuweka kabatini Kisha nikaenda kuoga........mda wa chukula ulifika na wote walikuwa wamesharudi hivyo wote tulikutana mezani........
"Sonia umepata vitu vyote ulivyohitaji"aliuliza mama
"Ndio"
"Okay vizur"
"Asantee mama ubarikiwe"
"Hahaha sio mm nilietoa hela ni Rahul kwaiyo abarikiwe yeye"
"Nilimgeukia Rahul na kutabasamu bila kuongea kitu....nayeye nae alitabasamu na kunikonyeza Sasa kile kitendo Berat aka Mr kauzu akakiona aisee alituangalia Hilo jicho .......kila mtu akaangalia kwenye sahani yake fasta
T
Kama kawaida mr kauzu ndio anakuwaga wakwanza kumaliza kula aliinuka na
"Sonia ukimaliza kula nakuhitaji chumbani kwangu"
"😳😳Nimesafanya nini
SEHEMU YA 10
Baada ya kumaliza kula nilienda chumbani kwake nilifika na kugonga........mara kadhaa hakuitikia wala hakufungua....…..."Sasa alivyo niambia nije alafu nagonga haitiki wala kufungua anamaanisha nn"niliongea mwenyewe na kugeuka ili niondoke......nilipiga hatua mbili mara nikashtuka navutwa na kuangukia kifuani mwake huku mkono wake mmoja kanishika kiunoni ...... Niliinua uso nikamuangalia vizur mda huo tulikuwa zero distance na yeye aliinamisha kichwa maana nimrefu kwangu navile tulikuwa na pua ndefu😂 zikawa zimegusana Kama vile alitaka kunikiss au nina fikilia mbali.........baada ya kuinua uso wangu ukakutana na wake niliona aibu hivyo nikaangalia chini..........Ila hata Kama ingekuwa wewe huyu mtu hafai hata kumuangalia machoni....... yaani anamacho makali balaa sijui huyo mwanamke wake anamuangaliaje au ndio kashamzoea.........ila huyu kwa jinsi alivyo kweli anaweza kuwa na mwanamke 🤔sidhani labda maana kunawatu wanajua kujitoa muhanga Ila mm hapana"......"hiki ndicho ulichikuwa unakitaka sindio"..aliongea na kunishtua kutoka kwenye mawazo".........."ndio"nilijibu hata bila kuelewa naongea nn.... aliniangalia kwa jicho Kali huku amenikunjia ndita balaa...........haraka alinivuta na kunipeleka kabati lilipo ...."kwani huyu kauzu ananipeleka wapi "niliwaza ............alifungua kabati kabla hata hajasema kitu nilitoa macho namna nguo zilivyokaa shagalabagala wakati nilipasi na kuziweka vizuri "huu upuuzi gani umefanya, nilikwambia nn na umefanya nn"......aliongea kwa hasira kiasi Cha kuniogopesha nikitetemeka na machozi yakaanza kunitoka. Kwajinsi nilivyokuwa muoga nilishindwa hata niongee nini said nilitikisa kichwa kuashilia hapana........."umekuwa bubu ghafula,nakuuliza nimekwambia ufanye nn na hikk nini"........."Be be berat mi mi nimefua na kupasi Kisha nikaziweka vizur "..,. kwaiyo hivi ndio umefua na ukapasi kisha ukakunja"........aliongea huku akinionesha moja ya shati cheupe nilishangaa lilikuwa chafu na limejikunja kunja kuliko hata lilivyokuwa kabla sijafua......."wewe".......aliita kwa ukali mda huo nilihisi tumbo la kuhara kinaanza kumbukumbu za kipigo cha mamdogo zilinijia nikanywea kama kifaranga aliye nyeshewa na mvua...huku nikiwaza kipigo kitanihusu sekunde yoyote"nisamehe Ila sio mim".........niliongea huku machozi yakinitoka sikuwa hata na ujasiri wa kuinua sura yangu..........."moja kati ya vitu ninavyochukia kwenye hii dunia ni uongo,namchukia sana mtu muongo "........."hapana kaka mi"......"kimya"......aliongea kwa ukali kiasi walioko sebleni wakasikia........."bro kuna nini"...... ilikuwa ni sauti ya Rahul.......lakin hakuna aliyoongea kitu kumjibu....."nataka hzi nguo zote ziwe safi ndani ya lisaa na ole wako ifike asubuhi nguo hazijakauka utajua mm ninani......... aliongea na kufungua mlango kisha akatoka ...... Rahul alitaka kuingia Ila alimzuia kuwa hataki mtu chumbani kwake
Nilitoa nguo nje ili nizifue mda huo huo Rahul alikuja na kuniulza......"Sonia Nini kimetokea mbona unafua nguo ambazo ulikuwa tayari umeshazifua" .........sikumjibu niliendelea kufua alipoona simjibu aliondoka akionesha wazi kuwa amekasirika .....baada ya dakika 3 Nicole nae akaja....."Sonia Kuna nn mbona unafua usiku alafu Rahul anagomba huko ndani ".......Sasa Nicole alivyosema hivyo nikama vile ameniambia Sonia lia weee nilianza kulia kwa kwikwi yaani nikilia kwa uchungu Sana moyoni niliwaza mda simrefu nitafukuzwa nitaenda wapi Sina mama Wala baba Wala mtu yoyote na vp mamdogo akijua niko huku akinishika sijui ataniua kwa silaha gani......"acha hizo nguo nipe nifue mimi"............."hapana Nicole nitafua mwenyewe"
"Sonia Cha nifue hauwezi kufua katika hali hiyo"......... niliendelea kukataa lakin Nicole akachukua beseni lenye nguo kwa nguvu nikaona nimuache tu........wakat anaendelea kufua mara akaja Mir kauzu huku kakunja uso hatari Mimi nikaisi mkojo unataka kutoka...."Nicole" aliita Nicole aligeuka kwa mshtuko "abee" ............."ingia ndani" ...... Nicole aliacha kufua fasta akaondoka bila hata kubisha......mim mda huo nilikuwa natetemeka balaa aliangalia saa yake na kusema........"unadakika 10 tu "Kisha anaondoka ....... niliamka nakufua haraka haraka hadi nikamaliza nikaingia Ndani nikamkuta Rahul amekaa huku kainamisha kichwa alivyoniona alikuja na kunikumbatia mimi mda huo nilikuwa nimetoa 😳 tu...."I'm sorry Sonia"......sasa ile nataka kuongea nikamuona Berat aka mr kauzu yuko juu anatuangalia haraka nikajitoa mikononi mwa Rahul na kuondoka bila kusema kitu Rahul nae alitaka kumifuata naona alipomuona kaka yake akasimama .......yaani huyu kaka wana muongopa Kama vile ndio anafanya waishi😡 nilifika chumbani kwangu nikashangaa kumkuta Johari amelala kitandani kwangu ....."huyu nae vp"nilivyo sema hivyo akaamuka na kuanza kucheka "hahahahahaha unajisikiaje kijakazi mrembo".......niliona huyu anataka kuniletea maigizo tu nikapiga hatua kuelekea bafuni Mara akanivuta kitambaa Cha kichwani kikatoka ukumbuke hapo ninakipara changu niligeuka fasta ili nimng'anye kitambaa alimuwahi na kujitupa juu ya kabati Kisha akaanza kuongea "heeee yaani mda wote umefunga kitambaa tunadhani unajistili kumbe unaficha kipara mm! Makubwa utakuwa unaukimwi wewe maana sio bure mdada Kama wewe hawezi kukaa na upala "
Nikaona huyu nikiwa hivi atanipanda kichwani"nisikilize Johari tena nisikilize kwa makini naomba unikomee tena usinizoee kwani nikiwa na ukimwi we inakuhusu nn"......."hahahhahahaha heee kipofu kaona mwezi kwaiyo ukajitutumua kujibizana na Mimi, nilikwambia kuwa siku zako za kukaa humu ndani zinahesabika unaona nilichofanya leo Sasa huo nimwanzo"......."hee kumbe wewe ndio umechafua nguo "...."kumbe ulijua Nani na kama hautokaa mbali na mwanaume wangu utatolewa humu ndani kama mbwa" aliongea kisha aondoka nikabaki nimesimama tu........."jamani kwani huyo mwanaume wake mimi nimemchukua? ........ nikaona nilale tu maana siku yenyewe imekuwa nzito..........
Nililala asubuhi na mapema niliamka na kuanza kazi wakati nadeki alikuja Berat........."unategemea nitaenda kazini na nguo za kulalia au nakaa nyumban"........aliposema hivyo nikatamani kumwambia nguo zingine siziko kabatini au unataka nn Ila nikaona nikiongea nitafukuzwa bure........haraka nikaenda nje na kuchukua shati moja na kuingia nikawa naipasi Sasa kwakuwa ilikuwa haijakauka nikaweka Moto mkali sangap nisiunguze ........... Hapo nilitamani ardhi ipasuke niingie.... wakati nikiwa na waza nifanye nn kidume huyu hapa akiwa ametoka kuoga......."naomba nguo"........ nilianza kulia hata kabla sijaanza kuongea........ alivyo hivyo akasogea na kuchukua shati Sasa siakaona ilivyoungua alinigeukia na kuniangalia kwa macho makali kama vile anataka kunimeza......"nu upuuzi gani huu"
"Samahani ni bahati mbaya"
"Hivi mama aliwezaje kuleta msichana mjinga Kama wewe ambae hujui hata kitu chochote, ili uje kufanya nn hasa.....ni mwanamke wa aina gani usiye jua kufua hata kupasi pia hujui huyo mama yako anakufundisha nn eee"aliongea mm nikainamisha kichwa chini haraka alinishika nakunivuta kuelekea sebleni ambapo alipofika aliniachia kwa kunisukuma "Berat mbona unamsukuma mtoto wawatu hivi amefanya nn"
"Sitaki kumuona huyu binti humu ndani"
Nilivyo sikia hivyo nikapiga magoti kuomba msamaha
"Boss naomba unisamehe nakuahidi sitorudia tena"
....."we usiniguse kafungashe kila kilicho chako uondoke"
"Kwann aondoke au nikosa gani alilofanya ambalo haliwezi kusameheka"aliongea Rahul huku akinishika mkono........"eti mwanangu umefanya nn"
"Mama nimeunguza nguo yake bahati mbaya"
"Berat mwanangu kuwa na moyo wakusamehe hilo sio kosa la kumtoa humu ndani"
"Mama Berat yuko sahihi huyu binti aondoke kwanza anaukimwi hapo alipo nywele zimenyonyoka hana hata moja"aliitikia Johari
.....na baada ya kusema hivyo Berat alisimama na kugeuka Kama vile hajasikia vizur......"ana nn"
Alipouliza hivyo Johari alinifata nilipo akanivua kitambaa nikabaki kipara nje.......wote waliniangalia kwa mshangao "ninani aliye kwambia kuwa mtu akiwa na ukimwi anakuwa na kipara"Rahul aliongea akionesha kuchukizwa ........" kweli hakuna mahari palipo andikwa kuwa mtu akinyoa kipara basi anaukimwi na Kama akiwa nao shida iko wapi kwani niajabau au yeye ndio wakwanza kuumwa huo ugonjwa?
Aliongea Nicole
"Johari nimeshakwambia upunguze ukali wa maneno yako "aliongea mama
"Mama narudia sitaki kumuona huyu msichana humu ndani"
"Berat hii imezidi hivi unajiona Kama Mungu humu ndani kiasi Cha kuamlisha kila mtu sasa nisikilize Sonia haondoki humu ndani Kama Kuna mtu anashida juu ya hilo anaweza kuondoka yeye"
"Wow Mom kwaiyo uko tayar kufukuza watoto ulio wazaa kwasababu ya huyu kijakazi asiye na mbele wala nyuma"
Aliongea Lee
" Kama hataki kuni heshimu itakuwa hivyo haiwezekani mnipangie sheria ndani ya nyumba yangu huu upuuzi sito uvumilia tena,Sonia nenda kaendelee na kazi zako"
"Asantee mama"nilimshukuru na kuondoka Ila jicho alikokuwa akiniangalia Berat na Lee lilikuwa linatisha niliona humu ndani sio salama kwangu na sikutaka kutenganisha familia ambayo nimekuta iko vizur............kabla sijafika mbali nilisimama baada ya kusikia Rahul akiongea
"Mama naomba utafute mtu mwingine,kwajinsi ninavyomjua Berat na Lee watamfanya Sonia aishi humu ndani kama kuzimu na siko tayari kumuona Sonia akiumia hivyo nitamtafuta kazi nyingine na nutajua mwenyewe aishi wapi"
"Hapana akae humu humu "alijibu Nicole
"Sonia atakaa hapa na sitoleta mtu mwingine "
Alijibu mama na kuondoka ...... Rahul alimgeukia Johari na kusema na wewe kibonge mweusi ole wako nisikie au kuona unamsema Sonia kwa lolote baya au ahuzunike sababu yako hiyo siku ndio itakuwa mwisho wako kumbuka hili neno utajuta"
"Lakin Rahul mim" hata kabla hajamaliza kuongea Rahul aliondoka na kuja nilipo
"Sonia I'm sorry kwa kilichotokea nakuahidi kukurinda daima"
"Rahul mbona unaomba msamaha kwa kitu ambacho hujafanya wewe"
"Hapana Sonia kosa lolote litakalo fanya na familia yangu basi na mm nimo kwakua mimi pia ni mmoja wao"
"Kuwa na amani haya nimambo ya kawaida tu"
"Hakunaga Mambo ya kawaida kwenye manyanyaso"
"Haya yameisha"
"Sonia"
"Abee"
"Sorry kama nitakuwa nakosea kukuuliza hivi,kwann umenyoa nywele zako zote".......aliponiuliza hivi niliwaza kabla ya kumjibu nikaona Bora nimdanganye maana sikuwa tayari mtu kujua historia yangu nilihisi ikijulikana inaweza kuwa fimbo nyingine ya kunichapia kwaiyo nikajibu
"Mama yangu mdogo alifariki kwaiyo nikanyoa kuashilia maombolezo".
"Ooo pole "
"Asantee".
"Lakin unakichwa kizuri ingekuwa mm hapa na kichwa changu kama yai sijui ningefananaje"alivyosema hivyo nilicheka sana
"Una tabasamu zuri sana natamani mda wote uwe unafurahia "aliongea kwa hisia hadi nikaogopa
"Okay nenda kanywe chai mda unaenda"nilimwambia .
"Sawa vp wew unakunywa sangp"
"Nakuja sasaiv "
"Okay "aliinuka na kuondoka baada ya kuondoka Johari akaja
"Umetangaza Vita na mm Sasa nakwambia hii nyumba utaiona chungu".
"Hivi Johari unapepo au nini kwani nikitu gani nilichofanya Cha kutangaza vita na wew"
"Mfyuuuu"alisonya na kuondoka Ila huyu dada sio mzima Kama shida ni Rahul siukamwambie kuwa anampenda kuliko kujaziana nzi hapa mfyuu
SEHEMU YA 11
Nilienda mezani kunywa chai nikamkuta Nicole yuko bz na simu yake aliponiona akaweka pembeni
"Pole dear".
"Asantee".
"Ila kuwa makini maana usije ukadhani mama amekutetea leo atakutetea na kesho kiufupi Berat ndii roho ya mama unaweza kushangaa akaenda huko chumbani akajifikilia Kisha akaja kukwambia ondoka so usimwamini hata kidogo pia hakikisha haumkwazi Berat tena maana inaonesha wazi hakupendi kuhusu Lee yule ni chawa tu kila anachofanya Berat anafagilia so akili yako iweke kwa Berat sawa dear"
"Haya asantee "
"Poa baadae mm naenda kazini "
"Haya byee"
Aliinuka na kuondoka baada ya dakika 3 akashuka Lee na Kaka mr kauzu.....nikipowaona nilihisi kutetemeka balaa niliinuka haraka na kutaka kuondoka Ila sauti nzitu ya Berat ilinistisha"subiri"......uwiii nimeishaa
"Nifuate"haraka hata bila kuuliza nilimfuata nyuma tunaenda kwenye chumba kimoja hivi akafika akaniambia
"Unga macho"
"Eee "
"Hujasikia au kiburi"
Nikaona isiwe tabu nikafumba baada ya sekunde kadhaa akasema "unaweza kufungua"
😳Nilitoa macho baada ya kuona pale chini kumefunguka na kuonesha ngazi zinazoshuka chini niligeuka nyuma kuangalia Kama niko humu ndani au nyumba nyingine ilikuwa ni nyumba hii hii nilitamani kuuliza imekuwaje hapa chini kumefunguka na hapaoneshi kuwa kunaweza kufunguka maana nadeki karibu kila siku
"Mbona umesimama nifate"
"Huko chini"
"Hapana huko juu"aliongea na kunivuta mkono tulishuka chini zaidi nilishangaa kuona kuna nyumba nyingine huko Ila kulikuwa kuchafu sana
"Nahitaji ufanye usafi humu ndani ya saa moja ukichelewa kunajifunga na hakuna mtu anaweza kukufungulia zaidi yangu na mm naondok.......
"Boss humu ndani nipachafu sana kwa huo mda hautotosha "
"Hiyo ni shida yako sio yangu"alijibu na kuondoka nikabaki na dua tu nisielewe kuwa nianzie wap niishie wap..... Nilizunguka kuangalia sehemu zote nyie kulikuwa kuchafu haswa kiasi ambacho ningetakiwa kutumia siku nzima ili pakae sawa Sasa hili lisaa nitafanya nn
Mwishoni niliamua kuanda huku nikijiongelesha mwenyewe......kutoka na kuwa ni chini nilishindwa kujua mda umeenda au bado maan hata jua nilikuwa silioni taa tu ndio ilikuwa on ...... Nilifanya usafi kila mahari na nikajikuta nasahau kuwa nilipewa aaa moja tu baada ya kumaliza nilipanda ngazi kwenda juu ili nitoke kweli Kama alivyosema nilikuta kumefungwa "Mungu wang nitatokaje humu ndani"niliongea mwenyewe nikaona nigonge niligonga lakin wapi nikaita wapi mda ulizidi kwenda njaa nayo haikuwa mbali nilihisi njaa hatari.......nilikaa Sana bila mtu kuja nikaona Bora nichukue daftal na penseli nikaanza kuchora moja kati ya vitu alivyonibariki Mungu ni kuchora ...... sijawahi kufundiswa na yoyote Ila nipe kazi nikufanyie hutaamini Kama ni mimi .... kwaiyo picha ya kwanza nilimchora Mr kauzu sijui kwann ila sura yake ilikuja machoni mwangu hivyo nikamchora yeye kwanza alafu nikachora na vingine.......nilitumia mda mwingi hadi nikachoka ila bado hakukuwa na dalili ya mtu kuja nilikaa mwisho nikapitiwa na usingizi ..........nilikuja kushituka na kujikuta nimelala kitandani kwangu haraka nikakurupuka " hee vp unaota"ilikuwa ni Nicole naona alikuwa amekaa pembeni yangu "hapana nimefika je hapa"
"Umefikaje hapa kwani ulikuwa wapi?
"Nilikuwa kule c"kabla sijaongea alikuja mr kauzu na kumuita Nicole aliamka haraka nakwenda "imekuwaje niko hapa nani alinileta na mbona sikusikia🤔"nilijiuliza swali ambalo sikuwa na jibu nalo .......niliamka na kwenda sebleni hakukuwa na mtu niliangalia saa ilikuwa saa tano usiku.....😳heee inamana nilikaa kule Hadi usiku au nimelala Sana.........
Nikaenda jikon nakukuta chakula kwenye sufuria nikakifakamia chap Sasa wakati nikiwa natafuna sinikamuona mr kauzu kasimama ananiangalia aisee nilipaliwa kidogo nife Sasa jinsi alivyo katili hakunipa hata maji badala yake aliondoka
Nilimaliza kula na kwenda chumbani kwangu kulala asubuhi niliamka na kwenda jikon nikakuta johari yuko bz anapika "za asubuhi"
"Salama,anhe jana ulienda wapi maana had tunaenda kulala ulikuwa haupo au ndio ushapata mwabwana huko"
"Hayakuhusu nilimjibu na kuondoka"
"Ha ha ha amakweli masikini akipata mata* hulia bwata leo hii unanguvu za kujibizana na Mimi"
Sikumjibu tena zaid niliondoka zangu nikaanza kufanya kazi nilifanya usafi kote ikabaki kwa Berat niliwaza namna ya kuingia nikawa nimesimama
Mara akaja Rahul"Sonia unaendeleaje"
"Niko poa vp wew"
"Safi mbona umesimama hapa badala upimzike sio vizur kufanya kazi ukiwa unaumwa"
"Nani anaumwa"
"Si wew au haumwi"
"Ndio mimi siumwi'
"Kwaiyo Berat alitudanganya maana wakati tunarudia alituambia kuwa unaumwa"
Mmmm huyu sialisema hapendi uongo sasa mbona kadanganya niliwaza"ndio nilikuwa naumwa Ila Sasa niko poa "
"Kweli "
"Ndio"
"Haya basi
Aliondoka nikabaki nawaza namna ya kuingia humo chumbani Ila naogopa nini so Niko kazin nikagonga hakujibu nikaingia " za asubuhi"nilimsalimia Ila hakuitika nikaona utajiju kikubwa nimeshakusalimia nikaanza usafi yeye huyo............ nilifanya usafi nikamaliza nikaoga na kisha nikaona nilale zangu ..........zilipita siku mbili nikiwa na amani moyoni nikaamini kuwa maisha niliyokuwa nikiishi nyuma hayatajitokeza tena ............ Siku ya j mos niliambiwa kuwa kutakuwa na jumiya pale nyumban hivyo nilitakiwa kuandaa mazingira vizur baasi nikaanda kila kitu na mda ulipofika watu wakaja na sis sote tukatoka nje............ibada ilianza Sasa mda wa kusoma neno Berat akanipa biblia ili nisome neno kwakuwa sijui kusoma nilitikisa kichwa kuashilia hapana Ila alinikazia jicho kuwa nichukue 😓nikapokea Sasa kipengele kinakuja naanzia wapi naishia wapi niliganda Kama sanamu "wewe siusome mbona unatugandisha hapa"aliongea Lee basi kinyonge huku mapigo ya moyo yakienda Kasi nilianza n e e m a y a m u n g u..... watu wote waligeuka na kuniangalia maana nilikuwa nasoma herufi moja moja Kama vile mtoto anaeanza kujifunza kuongea haraka Rohit/Rahul alikuja na kuning'anganya na kusoma yeye Mimi mda huo niliinamisha kichwa chini kwa aibu kulikuwa na watu wengi balaa ........baada ya ibada kuisha tulirudi ndani mda huo niliamua kuonesha tabasamu Kama vile hakijatokea kitu "Sonia haujui kusoma"ilikuwa ni kauli ya kwanza mama aliuliza mara tu tulipoingia ndani.. ....."ndio" nilijibu Kama nikitu kizuri vile "Sasa Kama ulijua hujui kusoma ulikubari kuchukua biblia ya nn siungekataa kuliko kujidhalilisha vile"
"Huyu anakuwaga na kihalehele Sana anajiona anaweza kila kitu"alijibu Lee hatakabla sijamjibu mama
"Unaringa na uzuri kumbe kichwani zero brain mh makubwa "aliongea Johari huku akinipandisha na kunishusha"
"Inatosha kwani kipi Cha ajabu " aliongea Nicole ......
"Naomba msahama kwakua nimewaaibisha"niliongea
"Sonia hina haja ya kuomba msamaha kwani haujakosea kitu"alinijibu Rahul huku akionesha kukosa furaha
Berat aliinuka na kuondoka bila kusema chochote Lee nae akafuata ...... nikaona niondoke zangu
Nilitoka sebleni nikaenda chumbani kwangu nikafungua mlango na kuingia bafuni Kisha nikafungulia maji kisha nikasimama huku maji yakitiririka nilikuwa na maumivu makali 😓 japo sikutaka kuyaonesha kwa mtu yoyote .......hivyo niliona nibora nikalilie bafuni
........ nililia huku maji yote yakinishukia na nguo zangu nililia kwa uchungu Sana
Baada ya kulia kwa mda mrefu nilinyamanza na kutoka bafuni ..........Ile nafungua mlango tu nilishtuka kumuona Rahul akiwa amekaa mlangoni ..........aliponiona tu alinikumbatia huku machozi yakimtoka ........nilijiuliza kaingiaje wakati nilifunga mlango mda huo nilikuwa nimejufunga taulo tu
"I'm sorry kwakuruhusu macho yako kutokwa na machozi Ile hali nilikuahidi kuwa nitakurinda na kukupa furaha"aliongea kwa hisia Sana huku akiwa amenikumbatia kwa nguvu
"Rahul haujani"
"No Sonia nimekukosea nilitakiwa kuirinda furaha yako na sio kuiondoa"
"Laki"kabla sijamaliza Rahul alinikatisha kwa kuniwekea kidole mdomoni 🤫 nilikaa kimyana kubaki nikimuangalia tu alionekana Amelia mda Sana maana alikuwa mwekundu Kama nyanya vile 😁
Alinyoosha mikono yake na kunishika usoni na kusema "umenisamehe"
"Ndio"nilijibu hivyo ili asiendelee kuongea badala yake alinisogelea zaidi na kunikiss kwenye paji la uso. ........Mara mlango ukafunguliwa nilishtuka nikataka kugeuka lakin Rahul alinivuta na kunikumbatia tena .............."usiogope niko nawewe"alisema huku akiwa amenikumbatia.........huyu annitakia nn Mimi
"Rahul"ilikuwa ni sauti ya Berat tena alionekana kukasirika Rahul baada ya kusikia sauti ya kaka yake aliniachia harka na kugeuka mlango ulipo ........Mimi hapo nilitamani kukimbia Ila ningekimbilia wapi wakati mzee kasimama mlangoni
"Ni upuuzi gani huu unafanya"
"Brother huu sio puuzi Ila"
"Ila nn hujui huyu ni nani"
"Najua na ndio maana nafanya hivi "Rahul aliongea na kunishika mkono akanisogeza kwake mm hapo mkojo ulikuwa umeshabana niliona kuwa mda wangu wa kukaa humu ndani umeisha na sijui nitaenda wapi .......hivi kwann nisingekataa alivyonikumbatia badala yake nikasimama tu Kama mjinga ona Sasa nimeshaharibu 🙍♀️ nilimuangalia Rahul kwa jicho la niachie ila hakusikia
Berat alikuja na kunivuta kutoka kwenye mikono ya Rahul navile nilikuwa kembamba nilijikuta naangukia kifuani mwake aliniangalia kwa jicho kali huku akiwa amenishika kiunoni ............
"Mara watu wote wakaingia chumbani kwangu wakakuta Berat bado kanishika Nicole alivyoona alibaki😮
"Nini kinaendelea hapa mbona nasikia mizozo na mbona "kabla hajamaliza Berat aliniachia na kunitupia kitandani huyoo akaondoka bahati yangu taulo nililojifunga lilikuwa ndefu kidogo kwaiyo mapaja yangu hayakuonekana Ila alivyonirusha vile taulo lilitaka kudondoka nusura nibaki uchi Ila niliwahi kilishika Rahul alipoona hivyo na yeye katoka akiwa kafura hasira 😡
Kina mama wakabaki wananishangaa tu Mimi mda huo nimeinamisha kichwa chini
"Mnafanya nn ondokeni "mama aliwaguekia vijana wake na kuwaambia ......... wakaondoka akabaki yeye na Nicole wakiangaliana mama alikuwa nikama anajiuliza kimetokea nn hapa Ila akaondoka
Nicole alisogea karibu yangu nakusema
"Wewe ni Nini kinaendelea mbona nimeona Berat kakushika kiunoni tena uko na taulo tu"
Kwakuwa nilimzoea Nicole nikamwambia kila kitu
"Heee makubwa tangu lini Berat akaingia chumbani kwa mdada au kuingilia Mambo yasio muhusu hii ya leo Kali vp lakin Rahul alipokukumbatia umejisikiaje "aliniuliza huku akitabamu
"Sijasikia chochote"
"Na alipokukiss je"
"Sijahisi chochote"
Bwna mim nawewe ni marafiki so hauna haja ya kunificha kwanza natamani uwe wifi yangu lakina kwa
SEHEMU YA 12
Natamani uwe wifi yangu Ila kwa Berat
"Eee😳"
"Ndio unajua pamoja na kwamba Berat ni kauzu Ila akipenda anapenda kweli na Hana kauli mbili sio Kama Hawa wengine wana manenoa elfu vitendo zero"
"Naona umenichoka wewe "
"Kweli Sonia au unampenda Rahul"
"Hapana ".
"Basi mpenda Berat kaka yangu nae apate mrembo"
"Kwamba hana"
"Kwajinsi unavyomuona unadhani anae"
Niliinuka maana naona huyu anaongea vitu vya ajabu ajabu tu eti nimpende Berat katika watu wakupendwa alendwe yule mtu mwenyewe yuko Kama Askari wa motoni 😏 siwezi mm Bora nikampenda Rahul kwanza anajali mcheshi na ana upendo Ila huyu Hana hata kimoja
Basi nilivaa na kwenda kunywa chai Ile nafika tu Johari huyu hapa "malkia Kama malkia aka miss kilaza naona ulikuwa umeshikiliwa na Berat eee yaaani kitoto kimalaya hata mwezi bado unaanza kuwachanganya wakaka wawatu puuee "
"Shida yako nn Kama unataka kagawe na we siunacho au ulitaka akushike wewe 🥴"
"Alafu hiyo jeuri ya kunijibu hivyo nitakuja nikupige na huo weupe Kama papai lililo Iva ukawe wa nyanya"
"Sawa thubutu unipige uone Kama huo weusi Kama kwapa na la nyani mjane nitauongeza mara mbili"
"Unasemaje wew "aliongea nakutaka kunivamia Ila akaa kimya huku akiwa amesimama nilisikia harufu ya marashi ya Berat nikageuka nyuma kweli bhn alikuwa amesimama huku mikono iko mifukoni uongo mbaya alipendeza Sana nikama vile alitusikia hivyo akaondoka bila kusema kitu
"Huyu ndio mwanaume Nicole anataka niwe nae kuongea tu anahesabu maneno 😏"niliongea kwa sauti ya chini
"Una bahati"aliongea Johari
"Sema Nina bahati sio unahabati "
Nilichukua chai na kunywa huku Johari akiwa ananiangalia tu
Ulipofika mchana tulitoka familia yote na kwenda sehemu kula nyie huyu kaka anatisha yaani haongei wala kucheka yukoje sijui maana hata mizimu inaongea Ila yeye hapana .............walileta menu Rahul alikuwa amekaa karibu yangu hivyo akaniambia "utakula nn "
"Chochote "
"Okay "akanichagulia pale tukaa Kama dakk 20 chakula kikaletwa tulikula Kisha tukazunguka maeneno mbali mbali na usiku pia tukala huku hivyo tukarudi nyumban
"Sonia tunaweza kuongea"
Rahul aliniuliza
"Bila shaka"
"Asantee tunaweza kwenda kuongelea kwenye bustani"
"Sawa".
"Njoo chumbani kwangu sasaiv". Ilikuwa saut ya Berat niliangalia juu alikokuwa nikaitika "sawa, Rahul tangulia nakuja"
"Okay"
Nilipanda ngazi nakuingia chumbani kwa Berat
"Abee"
"Nifuate" aliongea na mm nikamfuata tulienda hadi kwenye kile chumba ambacho kuna njia ya kwenda kule chini ..............alifika na kunigeukia Kisha akaniangalia kwa sekunde kadhaa ....(huyu anataka kunijinja au mbona ananipeleka huku usiku huu)niliwaza
"Funga macho yako"alisema bila hata kuuliza nikafunga ............nilisisimka baada ya kushikwa mkono haraka nikafungua macho "nimekwambia funga macho"aliniambia baada ya kuona nimefungua macho ........... niliangalia mkono alikokuwa amenishika Kisha nikafunga macho mda huo moyo unakimbia balaa.........."unaweza kufungua"aliongea na nikafungua tulishuka ngazi najiuliza huyu anataka kunifanya nn
"Kaa hapo"
"Ee"aliniangalia hilo jicho nikaaa chap alikaa na kupiga kinanda mm mda huo nimekaa tu .............alipiga kinanda kwa mda mrefu bila hata kusema kitu Sasa kanileta hapa ili nione anavyopiga kinanda au nn maana haongei wala hajanipa kazi yoyote.........Kuna mda nilitamani niinuke ili niondoke Ila ningeanzaje hivyo nikaona nitulie tu...........nilikaa wee mwishoni nikapitiwa na usingizi nilikuja kuamka nikiwa kitandani chakwanza nikasikia harufu yake nikakurupuka Kama vile nimemwagiwa maji ya baridi kuangalia hakuwepo na chumba nilicholala hakikuwa changu ilikuwa kule kule chini nikaamka fasta Ile natoka tu nakutananae mlangoni akasogea
"Shikamoo"nilisamia Ila hakuitika huyo nikataka kukimbia nilivutwa Kama kawaida naagukiaga kifua tu🙈 nilitoa macho Kama vile mjusi aliyebanwa na mlango moyo nao hauchelewi kila Mara huyu jamaa akiwa karibu yangu unakuwaga unataka kuniacha maana sio kwa kwenda mbio huku sasa sijui unataka kwenda wapi...........
"Umeamkaje"aliuliza kwa sauti flani hivi nzito
"Mhu"
"Unajisikiaje"..huyu atakuwa anataka kunitoa kafara sio bure kwanzia nili akataka kujua nimeakaje........." salama" nilivyomjibu tu akaniachia "unaweza kwenda"
Sijufanya kosa nilitoka ndukiii hadi juu Sasa ile natoka like chumbani Nicole huyu hapa
Enheee nimeshikwa sijui nitasema nimelala wap
"VP mbona unakimbia asubuhi yote hiii".
"Hapanaa nilikuwa na"kabla sijajibu Rahul alitupita bila kusema kitu kwanza alikuwa kanuna balaaa
Sote tulibaki tunamshangaa maana sio kawaida yake.......Ila niliwaza atakuwa amenuna Jana sikutokea
Nilitoka na kuenda chumbani nikaingia bafuni nikapiga mswaki na kwenda kuanza kazi
Hadi unafika mda wa chai Rahul hakuja mezani
"Huyu Rahul leo ananini Hadi saiz hajaja kunywa chai"aliulza mama
"Naona leo ya uhindini yameamka "
Baada ya chai niliona nikaongee na Rahul maana nilihisi kuwa atakuwa amekasirika sababu yangu
Ngo ngo ngo niligonga mlango "ingia"
"Mamboo"nilisamia baada ya kuingia
"Kwann ulinidanganya"
"Rahul sikuwa na Nia ya kukudanganya ila "
"Ukaona haina umuhimu na lala wapi'?
Nilijikuta nakaa kimya baada ya kuulizwa hilo swali
"Ulilala wapi Jana"aliuliza tena
"Nililala nae mm kuna tatizo"
Ilisikika sauti nyuma yangu hakuwa mwingine zaid ya Nicole
"Alilala na mm na kuhusu jutokuja garden mm ndio nilimzuia so kama nikasirikie mm sio yye "
Baada ya kuongea hivyo niliona tabasamu la Rahul likirudi
"Sorry nilikukasirikia bure"
"Haina shida"nikijibu kwa wasi wasi huku nikimuangalia Nicole ambae alikikonyeza kwaishara nitulie"huyu anataka kufanya nn mbona kaongea uongo Kwan jana sialikuwa ameshall au alikuja chumbani kwangu akakuta sipo na mbona wakati tunaonana hakuniambia"nilijiuliza
"Nikakuketee chai"nilimuuliza Rahul
"Hapana nitaenda kunywa mezani".
"Haya bye"
"Asantee kwa kujali"
Niliinuka na kuondoka Nicole nae akanifuata .........
"Mbona umemdanganya Rahul"
"Ulitaka nimwambie ukweli alafu akununie"
"Hapana kwanza Umejuaje kama sikulala chumbani kwangu".
"Mwenyewe sijui labda nikuulize ulilala wapi ".
"Acha kunichota basi kama hujui kwann ukasema nililala kwako"
"Nilisema kwasababu nilisikia akisema kuwa hukulala chumbani kwako hivyo nikaisi utakuwa ulikuwa mahari labda kwa shem minitajuaje "
"Kwa Shem?"
"Ndio kwani wewe sister hadi usiwe na mtu, kwaiyo niambie ulikuwa wapi ".
Nilishusha pumzi Kisha nikasema" nililala huku chini"
"Chini? Chini wapi"
"Huku chini "
"Acha utani Umejuaje kama huku chini kuna nyumba wakati sijakwambia wala sidhani ka Rahul ameshakwambia pili huko chini hakuna mtu anae ingia zaid ya Berat tena na yeye hajaingia huko mwaka wa 3 huu Sasa wewe unasema umelala huku umefikaje na umejuaje?"
"Berat ndio alinipeleka "
"Weeee😳 Berat huyu kaka yangu au mwingine"
"Huyu huyu kaka yako".
"Ilikiwaje"
Kwakuwa ni shositito wangu nikamwambia kila kitu
"Ulichanjwa au kabla ya kuja huku ulipitia bahari ya Hindi ukatoa mikosi au ulivunja nazi maana hakuna msichana yeyote aliwahi kuingia huko na si kuingia tu hata kujua walikuja hadi wakaondoka bila kujua hatae huyo Johari hajui Sasa ilikuwaje wew akakupeleka tena ukalal huko huko"
"Sijui "
"Mimi naona atakuwa amekupenda sio bure"
"😂😂nicheke kwanza wakunipenda awe yule'
"Ndio kwasababu haijawahi kutokea kabisaa".
"Bwanaee tuachane nayo ngoja nikamalizie kazi zangu"
"Haya leo nitakuja kulala kwako tuongee vizur"
Tuliishia hapo kisha nikaenda kufanya kazi zangu
Usiku Nicole alikuja kulala chumbani kwangu tuliongea maengi Sana hadi tukalala
Kesho yake mchana nikiwa nimekaa alikuja Rahul na kusema
"Mamboo "
"Poa mzima"
"Yeah".
"Mbona umewahi kutoka kazini"
"Nimekuja ili nikufundishe kusoma,"
"Alisema na kutoa vitabu akaviweka mezani
Nilimwangalia nikajikuta natoa machozi
"Sonia kimetokea nn mbona unalia au nimekukwaza"
Nilitikisa kichwa kuashilia hapana kisha nikamkumbatia na kusema
"Asantee kwakunijali "
Alitabasamu na kunikumbatia vizur Kisha akasema "niwajibu wangu kukujali so usilie"
"Mda huo huo akaingia mama uwiii nilikurupuka na kumsukumia pembeni Rahul mama alibaki amesimama kwa mshangao
Itaendelea
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni