NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 04...5 Basi Ciara alilala chumbani kwa Mike,,,,saa kumi na mbili
"Kuna baridi endelea kulala"
"Kama nisipowahi kuamka nitapatiwa adhabu...."
"Nani huyo atakupatia adhabu na huku upo unanipumzisha?"
Ciara alikaa kimya, alirudi kulala kifuani kwa Mike.
Kwa namna mapigo ya moyo wa Mwanaume huyu yalivyokuwa yanaenda mbio aligundua ni kitu gani anataka.
Taratibu alipitisha mkono wake kwenye boksa ya Mike akaanza kuchezea sehemu zake.
Mechi ya asubuhi ilipigwa,
"Unaweza kuendelea sasa na majukumu yako..." Mike aliongea huku macho yake yakiwa kwenye mchoro wa Ciara
Ciara aliondoka akiwa mwenye kujiamini, watumwa wote walianza kunong'ona hasa baada ya kugundua alikuwa chumbani kwa Mike
Ile anakata kona, alikutana na Mlinzi wa Mike
"Niazime dakika mbili tu kwa ajili ya mazungumzo" Suzy aliongea
Ciara alifungua macho na masikio yake kwa ajili ya kusikiliza
"Naomba kujua kwanini uko hapa"
"Kwanini niko hapa?"
"Ndiyo"
"Niliuzwa hapa ili mtoto wa Shangazi yangu atibiwe"
"Uongo....nina uhakika lengo lako ni kuuteka moyo wa Mike, nikupe pole kwa sababu mambo siyo rahisi kama unavyo fikiria wewe" Suzy aliongea kisha akaondoka
Ciara alitulia kwa sekunde kadhaa, maneno ya Suzy yalimfungua akili.
"Nimenunuliwa hapa kama mtumwa, sikuwa na fikira nyingine. Ahsante sana kwa kunifungua akili...." Ciara alijisemea kisha akaondoka
Akiwa anatembea aliparamiana na Mtumwa mwenye umri sawa na Shangazi
"Sa.... samahani" Alijitetea
"Huna haja ya kuomba msamaha kwa sababu miguu haina macho, imekuwa bahati Mimi kukutana na wewe hapa. Jina langu naitwa Jala.... nitafurahi kama utanichukulia kama Mama yako kuanzia sasa" Jala aliongea
Ciara aliachia tabasamu kwa maneno anayoambiwa
"Haupendezei kuwa Mtumwa mahali hapa, unastahili kulala pembeni ya Mike"
"Una maanisha nini kusema hivyo"
"Kuwa ubavu wa Mike,.... jitahidi uonekane machoni mwake kwa namna yoyote ile" Jala aliongea kisha akaondoka
Ciara alidumu kwenye mshangao, hakuwa na hii ndoto hata kidogo lakini maneno ya Suzy na ya Jala yameshawishi akili yake.
Taratibu aliinua macho yake akayaelekeza usawa wa dirisha la chumba cha Mike.
Fikira zake zilienda mbali na hata akajiona akiwa kabebwa mgongoni na Bilionea.
"Ni kitu gani unatazama...." Sauti ya Mike ilimshtua
Itaendelea π₯
NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 05
"Namtazama huyo ndege aliyepumzika kwenye dirisha lako...."
Mike aliachia tabasamu akataka kuendelea na safari yake lakini alipiga pozi baada ya kukumbuka kitu
"Naenda kazini, nitamuagiza Suzy aje kukuchukua"
"Sawa..." Ciara aliongea kisha akaondoka, hakuonesha kushoboka na mualiko aliopatiwa
Mike alimsindikiza kwa macho, kuna namna anajikuta tu akitamani kumfahamu Ciara zaidi na zaidi
Muito wa simu yake ndio ulimshtua, aliacha kumshangaa Ciara
Upande mwingine Jessa (Mtoto wa Jasinta) alipona kabisa
"Nauliza kwa mara ya mwisho kama hautazungumza ukweli nitaondoka nyumbani kwako, naomba kujua Ciara yuko wapi"
"Nilimuuza kuwa Mtumwa kwa bilionea Mike ili wewe utibiwe"
"Kwanini usingeuza zile saa mbili za dhahabu?"
"Ni urithi nilioachiwa na Babu yako, siwezi kuuza hizo saa mbili na sitakuja kuziuza.....kila wakati mgumu utakapokuja nitatafuta njia ya kutokea. Ciara ni mtu mwenye roho ngumu sana usitarajie kuona machozi machoni kwake na hata hivyo kila kitu kimefanyika kwa ajili yako, punguza maswali mengi"
"Ciara hawezi kudondosha chozi mbele yako ....nina uhakika yupo katika wakati mgumu" Jessa aliongea kisha akaondoka kwa kukimbia
"Mbwa huyu hana shukurani hata kidogo, kwahiyo alitaka niuze utajiri wangu kisa yeye na huku Ciara yupo! mata..? yake asitarajie nitambembeleza kwa lolote" Jasinta alijisemea moyoni mwake
Jessa alielekea moja kwa moja kwenye jumba la Bilionea Mike. Aligonga geti mpaka akachoka lakini hakufunguliwa.
Alipoona hasaidiki alipanga mawe kisha akaanza kukwea ukuta.
Ukuta ulikuwa ni mrefu sana isingekuwa rahisi kuuweza,
"Aahhhhhghhh...." Alilalamika baada ya kudondoka chini
Bahati nzuri Suzy alifika akiwa na gari, isingekuwa rahisi kumpita Jessa bila kumsemesha
"Hujui kama unaweza kupigwa faini kwa kujaribu kukwea huu ukuta bila ruhusa" Suzy aliongea huku akisukuma na mguu mawe yaliyo pangwa na Jessa
"Nimegonga geti zaidi ya mara 20 lakini sijasikilizwa, sikuwa na njia nyingine tofauti na hii"
"Bila shaka wewe ndio sababu ya Ciara kununuliwa mahali hapa, inaonekana nyie wawili mnapendana kupita kiasi. Siwezi kukuruhusu kuingia ndani kwa sababu hauna biashara yoyote ya kufanya na Mike.....nimekuja kumchukua Ciara hivyo kaa hapa utamuona" Suzy aliongea kisha akaendelea na ratiba zake
Jessa alikaa kwa kutulia baada ya kusikia Ciara anatoka nje muda si mrefu.
Na kweli baada ya dakika 20 kupita Ciara alitoka nje akiwa na Suzy.
Moyo wake ulilipuka kwa furaha baada ya kumuona Jessa.
Suzy aliwapatia dakika 10 za kuzungumza
"Mama yangu ni mtu mwenye roho mbaya sana alikuwa na uwezo wa kuuza saa zake za dhahabu, sielewi kwanini kakufanyia hivi, naomba unisamehe Mimi" Jessa alijieleza
"Ni utoto wa hali ya juu kuongea hivi, ulikuwa katika hali mbaya sana.....ni jukumu langu kukusaidia"
"Usiniambie unafurahia kuwa Mtumwa wa Mike!...."
Ciara alimsogelea Jessa, ni wazi kabisa alihitaji kumuibia siri
"Ni suala la muda tu, nitahakikisha na uteka moyo wa Bilionea Mike, hivyo naomba usinihurumie kuwa hapa"
Jessa alikodoa macho tu, kwa kuwa muda ulikuwa umeisha Suzy alimchukua Ciara wakasepa
Mapigo ya moyo wa Ciara yalienda mbio baada ya kuliona jengo kubwa refu kwenda juu mfano wa urefu minara sita iliyounganishwa
"Hii ni ofisi ya Mike...." Suzy aliongea baada ya kumuona Ciara akishangaa kwa mara ya kwanza
Kwa pamoja waliingia ndani ya jengo.
Siku zote nyota njema huonekana asubuhi, Wafanyakazi wote walikuwa wakimshangaa Ciara kutokana na muonekano wake
Hii ilimpa maswali mengi zaidi Suzy na hata akatamani kujua ni kitu gani hicho cha kipekee kipo kwa Ciara na yeye hakioni
Mike akiwa katulia zake kwenye kiti aliachia tabasamu baada ya kumuona Ciara
Suzy hakusubiri kuambiwa aondoke, alijiongeza mwenyewe kwa kusepa
"Sogea ukae karibu yangu" Mike aliongea
Ciara hakuwa na shida alipiga hatua kisha akakaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na Mike
"Moyo wangu unawaza vitu vingi nitafurahi kama utabashiri ni kipi" Mike aliongea ni wazi alitaka kufanya utani na si serious muda wote
Ciara aliachia tabasamu kisha akanyoosha mkono wake taratibu ukashika moyo wa Mike
"Unawaza Kufanya mapenzi, ni aibu kwa sababu haya ni masaa ya kazi..." Ciara aliongea
Mike alikodoa macho kwa kitu akichoambiwa
Itaendelea π₯
FULL STORY 2000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni