ONE NIGHT ONE MISTAKE Chapter 10 Baada ya dakika kadhaa Romex aliwasha gari akaondoka na kuelekea mgahawani. Alimkuta
Karibu.
"Asante, pole kwa kutangulia.
"Hata sina muda mrefu tangia nimefika.
Wakiagiza chakula wakawa wanakula huku wakiendelea na maongezi. Siku zote walizokuwa waliona Lilian na Romex, Lilian alikuwa mpole, mwenye aibu, muda mwingi alikuwa Bize na simu yake. tabia zake zilikuwa tofauti na Salsa ambae alikuwa muongeaji na mwenye ushawishi wa kutamani uendelee kukaa nae.
Siku zilizidi kwenda salsa alikuwa Bize na kazi zake hakutaka kabisa kuendelea kuwa na mazoea na Romex hata alipompelekea chakula Salsa alikipokea tu lakini hakuwa na furaha nacho kama zamani na wakazi mwingine alikuwa anagawa kwa watu wengine.
Siku moja Romex akimpeleka biriani na sifa ya pepsi baridi ile alipotoka tu salsa alichukua simu na kumpigia Nzela.
"Nzela umeenda lunch?
"Hapana shoga yangu leo sina hela napiga pass
ndefu.
"Njoo ofisini kwangu kuna chakula hapa.
Nakuja sasa hivi shoga yangu.
Nzela alikata simu na haraka akanyanyuka na kwenda kwenye lift na kuelekea ghorofa ya nne ofisini kwa Salsa.
"Niambie mama kija.
"Chukua hicho hapo.
Nzela alifunua.
"Weee kitu cha biriani, nichukue na hii soda?
"Ndio chukua.
Asante Mwaya Nzela alibeba chakula na
kutoka ofisini kwa Salsa, alipofika mlangoni akakutana na Romex. Romex alipoona kile
chakula alijisikia vibaya akaenda ofisi kwa Salsa. "Mbona umegawa chakula? Hivi umekula kweli?
"Nimeshiba.
"Umekula nini?
"Viazi vya bibi kwani huoni tumbo lilivyokuwa
kubwa mimi nimeshashibishwa Romex haina haja ya wewe kuhangaika na mimi usilete tena
chakula chako hapa. Acha tubaki kama boss na mfanyakazi wake.
"Salsa hicho unachokiongea kinatoka moyoni? "Ndio sababu kilichonileta hapa sio kuonewa huruma bali ni kazi.
"Sawa mama kuanzia sasa kutakuwa na mipaka
kati yetu mimi sio Romex jifunze kuniita Boss.
Sawa BOSS. alitamka salsa kwa herufi kubwa tena kwa kujiamini.
Romex akitoka pale ofisini kwa Salsa akaelekea ofisini kwake
Siku zilisinga na mambo yakibadilika, salsa alikuwa anafanya kazi zake kwa bidii, alieoiluka maongezi ya kawaida na Romex waliongea
kuhusu kazi tu.
Salsa aliendelea kuonyesha tabasamu huku akishirikiana na wafanyakazi wengine.
Kwa upande wa Romex hakuwa na amani kabisa
japo alijaribu kuficha hisia zake lakini ilimuumiza sana kuwa mbali na Salsa alikuwa kamzoea sana, akumiss maneno yake na vitendo vyake
vya ucheshi.
Japo kuwa walikuwa anatoka sana na Lilian lakini hakuwa anafurahia alikuwa anaboreka na kuna wakati alikuwa akijisahau na kumuita Lilian jina la Salsa.
Siku moja jioni Salsa alikuwa akiandaa chakula chake, ugali na matembele pamoja na dagaa wa
kukaanga. Alifanya kazi kwa shida huku tumbo lake kubwa la miezi saba lilikuwa likionekana. Baada ya kupika aliandaa chakula chake chini
kwenye mkeka, wakati akiwa anajiandaa kukaa "
chini mara mlango uligongwa. Nani tena huyo jamani?
Mlango uligongwa tena salsa akaamua kumkaribisha.
"Pita mlango uko wazi. *Surprise...
Mlango ulifunguliwa na Meena aliingia
"Meena? Salsa alishangaa, Meena alimfuata na kutaka kumkumbatia lakini ghafla aliacha na macho yake yakaanza kwenye tumbo la Salsa.
*Salsa hiki ni nini?
Salsa alishusha pumzi ndefu kisha akasema
"Karibu dada, kaa kwanza. Salsa alikaa chini na Meena alikaa juu ya kochi.
"Mbona unakaa huko kaa chini tule. "Mmmmh siwezi salsa, siwezi kula wakati nina
shauku ya kutaka kujua, hiyo mimba niya nani na mbona hakusema mapema mpaka tumbo limekuwa kubwa hivyo? Ona ulivyochoka.
Salsa alimuangalia dada yake hakujua aanzie wapi kumuelezea.
Nataka kusikia kitu kutoka kwako Salsa. Aliongea Meena huku akiwa kamkazia macho usoni.
"Ni mimba ya boss wangu. "Ya boss wako? Mungu wangu, salsa unefanya
nini sasa? "Haikuwa dhamira yangu. Alisema salsa kwa
unyonge kisha akaanza kumuelezea kila kitu kilichokuwa kimetokea siku ile mpaka kupelekea
kupata mimba.
Meena alitulia kwa muda kama vile akiwa anatafakari kitu.
Nimekuelewa mdogo wangu umekosea ulitakiwa kusema mapema na hata muhusika ajue hill..
Hapana dada, Romex sasa ana mchumba wanataka kufunga ndoa ni bora asijue chochote kuhusu hii mimba. Nitajusimamua mwenyewe
kwa kila kitu, huyu mtoto ni baraka kwangu.
Alisema salsa huku akishika tumbo lake. Meena aliachia tabasamu kisha akamkumbatia. Haya ni mapigo tu mdogo wangu kila kitu kitakuwa sawa.
"Vipi baba na mama wakijua?
"Hata wakijua hawana la kufanya watakubaliana na ukweli. Nitaongea nao na wataelewa tu.
Itaendelea.....
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni