ONE NIGHT ONE MISTAKE❤ Chapter 5 Ukali wa Romex ulimfanya achanganyikiwe, Salsa Romex alimshika mkono na kumuangalia usoni kwa macho ya hasira lakini Salsa alikuwa na wasiwasi sana
"Samahani boss nilihisi uchovu kidogo tu. alisema kwa sauti ya kigugumizi huku akiinamisha macho yake chini.
Romex alikaa kimya kwa sekunde chache,
aligundua kuna siri kubwa salsa anaficha. "Uchovu? Salsa, huu ni uchovu au kuna kitu
kingine unachonificha? aliuliza huku akiwa na mashaka
Salsa alihisi koo limekauka ghafla. Akageuka upande mwingine na kujifanya kuchukua faili mezani.
"Hakuna kitu boss nipo sawa......
kabla hajamaliza kuongea, ghafla tumbo lake likachafuka akahisi kichefuchefu alichukua kimfuko ambacho akijiandaa na kuanza kutapika ndani.
Romex aliruka kutoka alipokuwa amesimama na kusogea nyuma haraka.
"Salsa! Wewe una tatizo kubwa, hii sio kawaida Salsa alijifuta midomo huku machozi yakimtoka.
"Boss, naomba naomba niseme ukweli sijisikii vizuri siku.
Romex alinyamaza, akamwangalia kwa muda mrefu kisha akavuta pumzi ndefu. "Twende hospitali sasa hivi. Hakuna muda wa kupoteza, afya yako ni muhimu zaidi.
"Hapana boss nitakuwa sawa.
"Au una mimba?
Salsa alishituka na kumtolea macho Romex maana hicho alichojionea alikuwa anahisi na
alikuwa aliogopa kupima. Salsa alitetemeka, moyo wake ulidunda kwa kasi, wakati huo Romex alikuwa akimuangalia
usoni.
"Hospitali?
"Ndio hospitali huko ndiko kila kitu kinaenda kuwa wazi. Nenda kajisafishe utanikuta nje.
Romex alitoka nje Salsa hakuwa na ni namna ya kukwepa hilo, alienda chooni kujisafisha baada ya hapo alishuka chini mpaka parking akamkuta Romex akiwa kasimama na mlinzi wake.
*Acha nimpeleke hospitali. Romex alimwambia mlinzi wake kisha akamfungulia mlango salsa wakaondoka kuelekea hospitali.
Romex alimpeleka kwenye hospitali ya gharama na kutaka afanyiwe check up ya mwili mzima na gharama zote ilikuwa juu yake.
Madaktari walimfanyia uchunguzi kwa muda mrefu na kumfanyia vipimo.
Baada ya muda daktari mmoja mwanamke
akatoka na kumuita Romex. Waliingia kwenye
chumba cha daktari wakati huo Salsa alikuwa anashuka kwenye kitanda na kujiweka sawa. Daktari alimuangalia Romex kwa makini kisha akasema
"Habari njema, Salsa hana ugonjwa wowote ila ni mjamzito wa wiki kadhaa. Romex Aligeuka kumtazama Salsa ambaye
aliangalua chini huku chini machozi yakimdondoka.
"Mjamzito...?" Romex aliuliza
"Ndio, pia ana upungufu wa damu, anatakiwa. kula vyakula vya kuongeza damu.
Salsa hakuwa na neno la kuongea Alihisi pumzi zikimbana.
"Asante sana doctor.
Ronei alimshika mkono wakabyabyuka na
kutoka nje.
Salsa alikuwa anatetemeka machozi hayakukata machoni kwake. Huzuni ilitanda
usoni kwake. Romex alimuangalia kwa huruma huku akiwa
ameshika mikono yake miwili. "Salsa, nataka unijibu ukweli. Huu ujauzito ni wa nani?"
Salsa kusikia hivyo alilia kwa sauti, macho yake yakiwa mekundu. *
Basi basi kulia hakuta saidia
"Boss sijawahi kutegemea maisha yangu yataharibika namna hii. Kila siku nimekuwa nikijilaumu kwa kilichotokea sikuwahi kukubali,
sikuwahi...... Maneno yake yakakata katikati kwa sababu ya kilio.
Romex alihisi kuna kitu hakipo sawa huenda mwanaume mwenye huo ujauzito haeleweki au amekataa. Alimvuta na kumkumbatia huku alimbembeleza.
"Usijali Salsa. Hata kama huyo mwanaume
atakuwa amekutelekeza sitakuacha upambane peke yako. Huu mzigo tutabeba pamoja, siku zote nitakuwa pembeni yako na kila atakacho hitaji basi niambie.
Baada ya hapo Romex hakutaka Salsa arudi kazini akimpeleka nyumbani kwake.
Walipofika Romex hakushuka kwenye gari ila aliona nyumba kwa mbali baada ya Salsa kumuonyesha.
Romex alitoa simu yake na kumpa Salsa aweke
namba yake ya simu. Salsa alipokea akaandika namba ya simu kisha akarudisha simu yake. "Asante sana boss.
"Usijall, tupo pamoja. Salsa alishuka kwenye gari kisha akaelekea kwake na Romex akawasha gari na kuondoka.
Akiwa njiani alikuwa akimfikiria sana Salsa. Sijui kwanini nimemuona huruma kiasi hiki,
anatoa huruma sana. Sisi wanaume ni watu wa haya sana sasa amekata mimba binti wa watu
na ameishiwa kumuacha mwenyewe. Romex aliongea vibaya na kuwalaani wanaume
wanaowatia mimba mabinti wa watu na wanaowatelekeza bila kujua yeye ndio muhusika.
Salsa alipofika ndani kwake alijikaza kitandani na kuanza kufikiria kile kilichotokea ule usiku pake hotelini, alikumbuka Romex alipokuwa alimwambia
"Tulia mama, nipe utamu mama, nitulize Merry wewe ndio unaeniweza mpaka maji naita mma... Salsa alinyanyuka pale kitandani na kukaa.
*Hivi huyu mtu ananiligizia, Inamaana hajui
tofauti kati yangu na Merry wake?
Romex anaujua ukweli anajua vizuri sana kuwa
hii ni mimba yake anajitoa ufahamu, siwezi kuharibu maisha yangu kwa kosa la usiku mmoja tu natakiwa kumwambia ukwell. Nitaenda kumueleza huwa hii ni mimba yake acha liwalo na liwe. Salsa aliongea kwa hasira.
Je kesho salsa atauvaa ujasiri na kumwambia ukweli Romex? Na kama atamwambia je Romex atalipokeaje hilo swala?
Full 1000
Whatsp
0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni