ONE NIGHT ONE MISTAKE Chapter 15 Baada ya sauti nzito ya baba yake Romex kimnya kilitawala, Mama yake alikuwa bado ameshikilia kanga yake mkononi.
Romex mwanangu mbona unataka kutibua nguo, familia ya kina Lilian unatuamini sana na ukizingatia tumeshsungana kibiashara kuna mambo tuna share pamoja. Kwanini unataka kuuvunja huu muungano mwanangu. Aliongea mama Romex huku machozi yakitaka kumtoka.
Hali ilikuwa ngumu kwa Romex alikuwa kasimama katikati yao, moyo wake ukidinda kwa kasi lakini bado akiendelea kushikilia msimamo wake hakutaka kabisa kumuondoa Salsa kwenye maisha yake.
"Baba, mama... naomba msinihukumu kwa hasira. Nimefanya makosa ndio. Lakini huu sio wakati wa kuniona kama adui yenu.
Niko tayari kubeba majukumu ya matokeo ya matendo yangu, ila siwezi kuishi maisha ya uongo kwa sababu ya heshima ya kifamilia. Siwezi kuishi na Lilian kama kimvuli, huku moyo wangu upo kwa mwanamke mwingine. Mama yake alijaribu kusema jambo lakini Romex akaendelea kuongea.
"Salsa ni mjamzito, ana miezi nane sasa. Nimemuandalia kila kitu, nimeweka mazingira bora kwa ajili ya mtoto wetu. Kitu pekee ninachotaka sasa ni baraka zenu. Sitaki niwe mtoto nisiefaa kwenye nyumba hii, niishie kama nipo uwanja wa vita na wazazi wangu.
Baba yake alinyanyuka kutoka kwenye kiti taratibu, macho yake yakimuangalia Romex kwa ukali.
"Kwa hiyo unatuambia hivi leo kuwa umeamua kutuounga wazazi wako kwa sababu ya mwanamke? Hivi ndivyo tulivyokulea? "Hapana baba, siwapingi Nataka muwe sehemu ya maisha yangu ya sasa, sio kuingilia maamuzi yangu ya maisha ya baadaye.
Mama yake aliongea kwa sauti ya upole iliyojaa na maumivu. "Romex, tume mpokea Lilian kama binti yetu. Sasa leo unakuja kutuambia maneno haya ghafla?
Tunawezaje kukubaliana na hili? Na wazazi wa Liliani watatumia sisi watu wa aina gani? Na vipi Lilian, umefikiria atalipikeaje hilo? Kwani hujui kumuacha mwanamke namba hii ni kumtia mikosi?
Romex alimsogelea mama yake, akapiga magoti mbele yake huku akimshika mikono.
"Mama, naomba. Naomba unielewe. Lilian ni mwanamke mzuri, lakini moyo wangu hauko kwake. Nisingependa kuishi maisha ya ndoa ambayo ndani yake hakuna upendo wa kweli. Mtoto wangu yuko njiani siku yoyote anazaliwa. Naomba unisaidie kumpokea Salsa, muone
kama binti yenu. Tafadhali mama. Mama yake alishindwa kuzuia machozi, akaanza kulia kimyakimya.
Baba yake aligeuka na kutoka sebuleni hakutaka kuendelea na mazungumzo hayo kwa wakati
huo.
Romex alibaki akiwa amepiga magoti, akiwa anamsihi mama yake amuunge mkono. Baada ya kimya kirefu, mama yake alisema kwa sauti ya taratibu:
"Romex, moyo wa mzazi unaumizwa sana pale mtoto wake anapompinga. Lakini bado ni mtoto wake. Nitakufikiria mwanangu. Nitafikiria. Romex alinyanyuka, akamkumbatia mama yake kwa upole.
"Asante mama, nakupenda mama yangu.
Sawa, sasa wewe usikae hapa nenda, baba yako bado ana hasira na wewe. Sawa mama, kitakachotokea naomba tuwasiliane.
Salsa alikuwa kajilaza kwenye kitandani chake huku akiwa ameweka mikono tumboni kwake akiwa anatabasamu. Tumbo lake lilikuwa kubwa, mtoto wake akipiga piga mateke tumboni. Alihisi furaha isiyoelezeka. Upendo wa Romex ulimfanya ahisi thamani yake, alikuwa anaota ndoto ya kuwa na familia bora na yenye furaha. Mara Simu yake ililia, alinyanyuka na kuichukua,
Ilikuwa ni ujumbe kutoka kwa Romex.
"Mama kijacho, nimeshawaambia wazazi. Haikuwa rahisi, lakini nimeweka kila kitu wazi. Nitapambana mpaka mwisho kwa ajili yako na
Salsa alicheka kwa huku machozi ya furaha mtoto wetu. I love you. yakimtoka. Nae akajubu "Asante kwa kupigania penzi letu baba kijacho wangu, Nitakuwa nawe siku zote. Najua bado kuna changamoto lakini upendo wetu ni silaha yetu. Nakupenda Romex.
Kwa upande wa Lilian alikuwa amekaa na wazazi wake wakawa wanaongea. "Yani akili ya Romex haipo kwangu kabisa anamuwaza mwanamke wake anaitwa Salsa. "Kwahiyo mpango wetu ndio utafell?
"Hapana mama siwezi kushindwa na msichana
wa hali ya chini aliyebeba mimba kwa bahati mbaya, nitahakikisha nafunga ndoa na Romex baada ya hapo tutachukua kila kitu tulichopoteza. Ni lazima baba yake Romex alipie kwa kile alichonifanyia baba yangu. Baba yake Lilian aliachia tabasamu kisha akasema
"Nilijua mtoto wa kike ataniabgusha lakini ona sasa anavyoona amua mali zake, huyu ndie damu yangu sasa
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni