ONE NIGHT ONE MISTAKE Chapter 13 Romex alikuwa na wasiwasi alihisi huenda Lilian akawa amesikia
Romex nimekusubiri sana naona Hauji, na mimi muda wa kukaa hapa umeisha acha niondoke tutaonana kesho.
Sawa. Lilian alimsogelea Romex na kumbusu kwenye shavu kisha akaondoka. Romex na Simu walimsindikiza kwa macho mpaka alipotoka nje ya geti.
"Hivi hajasikia kweli au ananiiigizia?
Atakuwa hajasikia, kwa tabia za wanawake
huwa hawawezi kuvumilia lazima angelianzisha.
"Afadhali nianze kumilizana na swala moja baada ya lingine.
Alisema Romex kisha akaingia ndani.
Usiku kucha Romex alikuwa mtu mwenye mawazo mengi, alijiuliza maswali mengi na kukumbuka maneno ya Salsa alipo kuwa akimwambia kuwa ni mimba yake nae akachukuliwa kama utani.
Hatimae kulikucha Romex akijiandaa na kwenda kazini. Siku hiyo alijitahidi sana kufanya kazi lakini hakuwa sawa, hakuweza kufanya kazi kabisa.
Alinyanyuka kwenye kiti chake na kuanza kuzunguka pale ofisini kwake huku akikuna kichwa.
Siwezi kuja na huu mzigo ndani ya moyo wangu.
"Salsa nataka tuongee jambo muhimu sana.
Alitoka ofisini kwake kisha akaenda kwa Salsa.
"Sawa boss. Salsa alikubali waongee akijua ni maswala ya kazi.
"Inamaana sio maswala ya kiofisi?
"Tunaweza kwenda kuongea nje ya ofisi?
"Ndio ni maswala binafsi.
"Sina cha kuongea na wewe boss.
"Salsa acha ubishi, usitake kuwaoa watu faida.
Mimi wala sijali kwanza mtu mwenyewe nimeshajichokea kwanza miguu yangu ina
vimba. Yani nipo tayari hata kubeba ilimradi twende tukaongee.
"Basi ongea hapa hapa.
Hapana, nikiwa naongea na wewe sitaki usumbufu.
Salsa alikaa akajifikiria akaona bora akubali hata
hivyo Romex ni boss wake.
"Sawa nitaenda unakotaka ila kwa sharti moja.
"Sharti gani?
"Sitaki kufuatana na wewe, tangulia nitakuja
kwa usafiri mwingine.
"Sawa tutakutana Diamond hotel, sasa ole wako
usije. "Mbona kama unanitisha?
Romex hakujibu alipiga hatua kuondoka alipofika mlangoni alisimama na kumgeukia
tena
"Na tangulia, uje bila kuchelewa.
Baada ya Romex kutoka Salsa akianza kujiuliza maswali.
"Huyu mtu kapatwa na nini, jana kaja kwangu ghafla, na leo hii anakuja na kunilazimisha
niende sehemu ambayo sihusiki kwenda hapa kutakuwa na kuna wema kweli? Na anataka
kuongea nini na mimi?
Salsa alijiuliza maswali bila kuyapatia majibu Aliweka vitu vyake pale mezani baada ya hapo akachukua pochi yake na kuondoka.
Alifika Diamond hotel na kumpigia simu Romex. "Nimefika nipo getini.
"Nakuja.
Baada ya dakika mbili Romex alifika na kumshika mkono.
"Twende huku.
Wakiongozana mpaka ndani ya hoteli, Salsa alishangaa anapelekwa kwenye chumba cha hotel. Alisita na kusimama.
" Vipi mbona umesimama?
"Huku ni chumbani unataka ukaniganye nini na
hili tumbo langu kubwa, kumbe wewe huna huruma eee....
"Acha mawazo yako finyu hakuna kitu kibaya naenda kufanya.
Pamoja na Romex kumuaminisha lakini Salsa alikuwa muoga.
Romex alimvuta wakaingia chumbani.
"Kaa pale kitandani na hata ukitaka kulala pia lala.
Salsa alikaa kitandani, Romex alivuta kiti na kukaa mbele yake wakawa wanaangaliana.
Salsa nataka kujua jambo moja na sitaki unifiche jambo lolote.
Siku hiyo Romex alikuwa serious sana hakuwa yule wa siku zote ambae salsa alikuwa kamzoea.
"Unataka nikwambie nini?
"Nataka kujua hiyo mimba iliyobeba ni mimba
ya nani?
Salsa aligeuka akaangalia pembeni kisha akajibu
"Ni mimba ya mwanaume.
Najua ni mwanaume ila ninachotaka kujua mimi huyo mwanaume ni nani?
"Ni siri yangu, kwanini unataka kujua mambo yangu binafsi?
"Mmmmm... Hivi nia yako ni ipo hasa? "Boss unajua sikuelewi.
"Twende taratibu utanielewa tu
Romex alitoa ile bahasha na kuifungua kisha akatoa hereni zote mbili.
"Unazijua hizi?
Salsa alikuwa katia nacho mdomo ulikuwa mzito
kufunguka. "Hizi hereni sio zako?
Salsa bado alinyamaza kimya.
Hii nilichukua kwako nilipokuwa jana na ulidondoshwa na mwanamke kwenye chumba
cha hotel. Je huyo mwanamke alikuwa ni wewe Salsa?
ndio Romex atanielewa vibaya labda kuwa alikopelekwa mwenyewe chumbani. Salsa alijiinamia huku machozi yakiwa yanadondoka
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni