ONE NIGHT ONE MISTAKE Chapter 14 Maswali yote aliyoulizwa Romex hakuna hata moja ambalo salsa alijibu. Romex walinyoosha mkono wake akamgusa
mkononi, salsa akashituka.
Salsa sipo hapa kuhukumu najua kilichotokea usiku ule ilikuwa ni makosa yangu na yako pia. Kwanini haukusema chochote, kwanini
hakuongea hata kujitetea?
"Romex sina majibu ya maswali yako hata mimi sielewi kwanini nikishindwa kujitetea ila mimi.
nilienda kwenye chumba chako kwa sababu Domi waliniambia nimpeleke kiti lako bila yeye haya yote yasingetokea.
"Ok, ok kwahiyo hiyo mimba ni mimba yangu? Ndio, sikuwahi luwa na mwanaume, sikuwahi
kuingiliwa na mwanaume mwingine zaidi yako, hii ni mimba yako Romex tena kwa asilimia mia
moja ni yako.
"Oooh sasa kwanini haukusema Nilisema mara nyingi ila uliishia kucheka ukachukulia kama utani.
"Haukuwa serious Salsa.
Salsa alikuwa kajiinamia huku machozi yakiwa yanamtoka, Romex alinyanyuka kwenye kiti na
kwenda kukaa karibu yake, alimfuta machozi Basi salsa haupaswi kulia tena nipo hapa sasa nitasimamia kama baba wa mtoto wetu akae. Sahau yote yaliyopita tuanze upya.
Romex alimkumbatia na kumbusu.
Wakiwa kwenye kumbatio simu ya Romex iliita alitoa na kuangalia aliekuwa anapiga alikuwa ni Lilian
Hakujali simu ya Lilian akiweka pembeni na kuendelea kuongea na Salsa huku wakiwa na tabasamu, tumaini jipya na nuru ya upendo iling'aa mbele yao.
Waliondoka pale hotelini wakiwa na amani Romex alimrudisha salsa nyumbani kwake.
Kuanzia siku hiyo mambo yalianza kubadilika, Romex alianza kufanya mabadiliko makubwa. kwenye maisha ya Salsa, kwanza alimuonyesha
upendo wa hali ya juu, penzi lao kilichoanza mfano wa uwa saa sita.
Romex alianza kumuita majina mazuri mazuri ya kimahaba. Aliamua kumtafutia apartment safi huku akimwambia. Mwanamke wake hawezi
kuishi kwenye nyumba za hadhi ya chini na mtoto wake hataki azaliwe kwenye nyumba za changanyikeni.
Kuna muda ilimbidi salsa amuulize.
"Romex kwanini unafanya yote haya? Nina majibu mengi sana ya hilo swali lako Alijibu Romex huku akiwa kashika tumbo la Salsa
"Nipe machache.
Ok, moja ni jukumu langu kuwalinda na kuwaangalia wewe pamoja na mtoto. Mbili, kila unachofanya ni malipo ya kujifunza kila chozi liliwahi kukutoka.
Salsa aliachia tabasamu.
Umelidhika mama kija wangu. "Bado.
"Mmmh unataka nini ili uridhike?
Nini hatuna yangu mimi na wewe?
Romex alichukua kiganja cha mkono wa salsa na kukubusu
Hatma yangu ni kuanzisha familia bora, kuwa na wewe mpaka kifo kitutenganishwe. Umeridhika?
*Bado swali moja.
"Uliza.
"Vipi kuhusu Lilian?
Romex alishusha pumzi kisha akasema. Sina chochote kwa Lilian hivyo hana nguvu kwangu kama ulivyo wewe. Siwezi kuishi na
Lilian sababu sio chaguo langu ni chaguo la
wazazi.
Vipi kama wazazi wakitaka umuowe? Siwezi kutoa jibu la moja kwa moja ila nitajua jinsi ya kuongea na wazazi wangu na kila kitu
kikawa sawa.
"Sawa baba kuja wangu nimekuelewa.
Kuna jambo lingine nataka tuzungumze. "Jambo gani? Hivi ujauzito una miezi mingapi vile?
Miezi nane sasa.
Mmmmh miezi imeenda sasa naona habari ya
kwenda kazini iishie hapa. Nataka upumzike
uilinde afya yako na mtoto wetu. Kwakuwa boss wangu umesema sina
pingamizi.
Achana na jina la boss bwana hebu niite vizuri. Mume wangu, baba wa mtoto wangu. Hapo sawa.
Siku zilienda Romex alikuwa yupo Bize sana па Saisa na kumsahau kabisa Lilian Lawama zilikuwa hazitoshi kila siku ilikuwa ni mashitaka
mara hupokei simu zangu, mara hujibu messege zangu, siku hizi hunijali. Malalamiko ya Lilian ndio yalizidi kumkimbiza Romex hakutanani hata kuonana nae siku moja Mida ya saa tano Romex
alikuwa ametoka kwa Salsa akamkuta Lilian akiwa nyumbani kwake akiwa anamsubiri. Vipi mbona upo hapa?
"Nina maongezi na wewe.
"Muda huu?
Kwani napangiwa muda wa kuongea na wewe
mpenzi wangu.
Sawa Romex alikaa kwenye kochi akawa anamsikiliza.
"Romex mbona siku hizi umebadilika sana?
"Umeanza mambo yako. Sio kuanza na hapa nimekuja tuweke mambo
sawa na sio ugomvi. Hakuna kitu nisichokipenda kama lawama na
wewe kila mara ni kunilaumu tu Kupambanua penzi langu ni kulaumu?
Hebu kwanza nikuulize. Hivi ilishawahi kunipenda au na wewe umetafutuwa mwanaume kama ilivyo kwangu kutafutiwa ?
wewe Khaaaa inamaana wewe haujanipenda? "Umeona sasa akili zako yani swali juu ya swall.
Sikiliza Lilian wewe nenda nyumbani kwenu mimi nataka kupumzika.
Romex alienda chumbani kwake na kumuacha Lilian akiwa kakaa.
Mfyuuuuuu! Ungekuwa wala sibabaiki na wewe ila nipo hapa kwaajili ya mipango yangu wala usingejifanya shababi mpuuzi mmoja wewe. Alisema Lilian kisha akaondoka.
Baada ya siku mbili kupita Romex alienda nyumbani kwa umwazazi wake.
Baba, mama samahani kwa kuchukua muda wenu ila kuna jambo moja muhimu sana nataka kuongea na nyinyi.
"Jambo gani?
"Wazazi wangu mimi sitakuwa tena Lilian. Wazazi wa Romex walishitushwa na kauli ya
mtoto wao.
Unasemaje Romex? Mama yake aliuliza Nina mwanamke ambae ninaempenda na tayari ni mjamzito.
"Mama weeee... Ni aibu gani hii mume wangu. Baba yake Romex alimuangalia kwa hasira kisha akamuuliza. "Inatufanya sisi wajinga si ndio?
"Hapana baba
Kwanini umemsaliti mtoto wa watu na kwenda kuzurulisha kiuno chako huko kwa wanawake wengine?
Sijawahi kumsaliti na huyo mwanamke ndie
allyetangulia kabla ya Lilian Hata hivyo Lilian sio chaguo langu nimejipazimisha sana kumpenda lakini siwezi kusema ukweli sijawahi kumpenda.
"Nyamelaza wewe mpuuzi. Aliongea baba Ake kwa sauti ya juu huku akiwa kamtolea macho.6:04
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni