UTRAMUU WA MABOSS??????
SEHEMU YA 01
Linda ni bint mwenye miaka 22 alilelewa na mjomba wake baada ya wazazi wake wawili kufariki...
Maisha katika familia ya mjomba yalikuwa ya manyanyaso sana????????hata hivo baada ya Linda kukua na kujitambua alitoroka huko ujmbani akaenda kujitegemea mwenyewe????????
Siku moja aliamka asubuhi akaoga na kujiremba kisha vizuri kisha alijiambia
"Nina enda kutafuta kazi leo na naomba nipate kazi bora zaidi,
Alichukua vitu muhimu vilivyohitajika na kwenda kutafuta kazi.
Upande wa pili kuna kijana mmoja jina lake ni Alex asubuhi hiyo nayy alienda kwenye kampuni yake mapema kwa sababu alikuwa na marundo mengi sana ya kazi za kufanya.
Alex anaperson assistance wake anaeitwa Shirley..
shirley alikuja na kahawa ya Alex ya asubuhi.
"Habari za asubuhi Alex" alisalimia na Alex bado aliendelea kubonyeza laptop yake.
Shirley Alimuita boss wake Alex kwa sababu yeye ni mmoja wa washirika wake wa utm lakin wafanyikazi wengine wanamuita boss au mr
Alex alinyoosha mkono wake mbele ili ampe kahawa lakini kwa bahat mbaya alimmwagia na Alex akashtuka.
."Samahani sana Alex" Alisema na kuanza kumsafisha shati lake lililokuwa na madoa lakini akafungua kifungo chake kimoja, na mwanzo alex aliona ni kosa lakini Shirley alikuwa akimtazama Alex kwa macho ya ????????????
Baada ya alex kuyaona yale macho ndipo alipojua mambo ya kahawa yalikuwa kama mtego tu
Alex aliushika mkono wa Shirley na kuukunja kwa hasira akaanza kulia kwa maumivu.
"Nilikuambia usifanye hivi ofisini. Wewe ni mpnz wangu wa huko nje ya kampuni hapa ofisini wewe ni msaidizi wangu????????????
"Samahani, sitafanya tena" alisema Shirley na Alex akatabasamu.
"Usijal jambo ulilolifanya halitatokea tena maana umefukuzwa kazi" akasema Alex kwa sauti ya ukali.
"Mimi....ni......hivyo...so..samahani. Alex tafadhali" akaanza kulalamika Shirley
"Hey, niwaite walinzi au. Unajua itakuwa aibu sana kwako walinzi wakija kukutoa hapa" alisema Alex na kuchukua simu yake na akatoka nje.
Katika upande wa Linda amezunguka akitafuta kazi kwa karibu masaa 3 sasa lakini hakubahatika hata sehemu Moja
"Labda niendelee kutafuta kazi kwa saa moja zaidi na nikikosa nirudi zangu nyumban , akawa anajisemea Linda.
Baada ya dakika chache Linda alitembea akaona bango kubwa la baa mbele yake aliifuata baa ilipo
Linda aliingia ndani na kumuona mtu akisafisha kaunta. Alifika kwake na akamtazama akitabasamu.
"Aah..... Habari za asubuhi bwana" Linda alisalimia kwa upole.
"Nikusaidie vipi" aliuliza yule aliye mkuta pale kaunta.
"Nataka kuomba nafasi ya kazi hapa Linda alimwambia na akaelekezwa ofisi ya meneja.
Linda alifika pale na kugonga mlango
"Ingia" sauti ya kiume ilisema na Linda akaingia ndani.
"Habari za asubuhi bwana" Linda alimsalimia
"Nikusaidie vipi" aliuliza.
"Nipo hapa kwa ajili ya nafasi kazi" alimwambia akimpa CV yake.
" Jina lako nani " akauliza yule mwanaume
"Linda" akajibu Linda
"Sihitaji CV yako kwani unaweza kuwa mhudumu wa usiku wa leo tu"akasema huyo mwnme
"Oh" Linda alisema huku mdomo ukitengeneza alama O "Hakikisha unakuja mapema kwani sitakuwa nafanya kazi ya kukuangalia kama umekuja mapema au laa" Alisema huyo mwnme
"Ina maana nimepata kazi" Linda alimuuliza yule mwanaum kwa furaha na huyo mwanaum akaitikia kwa tabasamu.
"Hongera sana Linda"
"Asante bwana"
"Hapana, niite tu Bryan" Alisema huyo jamaa
"Sawa Bryan" alisema Linda na kutabasamu
"vipi naweza kupata mawasiliano yako" Alisema Brian
"Sawa" Linda alimwambia na kumpa mawasiliano yake..
Kwenye Kampuni ya Alex.
Baada ya tukio la kumfukuza kazi Ashley Alex , alimpigia simu Michael, rafiki yake wa karibu sana.
"WhatSup" alisema Michael mara baada ya kupokea simu..
"Tafadhali unaweza kunipatia msaidizi wangu binafsi mpya" akasema Alex
"Subiri usiniambie umemfukuza kazi Shirley" Alisema Michael na Alex akamueleza kila kitu.
"Siku zote nilijua Shirley alikuwa ma.... TU, alikuwa anaringa sana na Bora umemfykuza kazi, akasema Michael.
Tuachane na mazungumzo yote na
nipatie msaidizi wangu binafsi mpya" Alisema Alex.
"Leo kutakuwa na party utaweza kuja, Michael akasema.
"Sina uhakika kwa maana Nina kazi nyingi ila nitajitajidi..
Huku kwa Linda baada ya kupata kazi alirudi nyumbani kupumzika alilala kabisa maana kazi aliyopata ilitakiwa aingie usiku....
aliamka baada ya kulala na kuangalia saa na tayari ni saa nane mchana.
Alioga haraka haraka na kuvaa gauni lake fp la zambarau alipendalo.
Alifunga nywele zake vizuri akavalia viatu kisha alibeba mkoba na kuanza safari ya kwenda kazini..
Jioni ilifika Alex akampigia Michael..umeshanitafutia msaidizi wangu binafsi?? Hapana sijampata bado..Fanya haraka ambatanisha picha zangu kwenye matangazo ukifanya hivo atapatikana haraka..
Michael alicheka huyu mshnz kwa vile sura yake nzuri anaitumiaga kama kigezo cha kuwatumia ovy mabnt wa watu..
Michael alimwambia jiandae uje kwenye party leo lazima utampta bnt utakaemtaka..
Linda alifika baa akashangaa kila mahali palionekana ni pazuri na taa ya kilabu zilimulika kila mahali.
Linda alimfuata mtu aliyemuajiri pale
"Habari za jioni " Linda alisalimia
"Wewe umekuja mapema kuliko nilivyotarajia"
"Asante. Nifanye nini" Linda aliuliza
Alielekezwa aanze kuhudumia wateja waliokuwepo pale baa Linda alienda katika meza moja ile amefika tu kuuliza wanatumia nini Boss mmoja akamgusa naniliu..
Boss mwenyewe hakuwa mwingine ni Alex????????
Linda aliwakaa akamuuliza kwanini unshke bila ridhaa yangu??????????????Alex alianza kuleta mashauzi
Linda alimnasa kibao kimoja kilichopenya kwenye masikio ya kila mtu aliekuwepo baan pale????????
kila mtu pale alishtuka????????..wakaulizana huyu dm kapata wapi jeuri ya kuwapg matajiri????????
Itaendelea..
Full 1000
WhatsApp 0742133100.