Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
02 Jan 2026
488 views
VYOTE NDANI GONGA94
USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 12
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
ENDELEA......
Safari ya kurudi Ikulu ilianza, ndani ya moyo wangu nilikuwa na mashaka. Sikuamini kama naenda kufanya kazi kweli, isije kuwa ni mbinu ya Mfalme kwenda kunichinja kwa kosa la kutia nguo ya Kijana wake kwenye furushi.
Akili ya kuomba msamaha iliniijia, nilidondoka chini ni kapiga magoti katikati ya safari.
"Sikuchukua nguo ya Kijana wako kwa ubaya....si unajua nimemlea yule. Basi hali ya kuwa naangalia nguo zake kila ni kimkumbuka ilinitawala " Niliongea.
"Nakupeleka kule uwe Kijakazi wangu na si vinginevyo hayo makosa yaliyo kuondoa Ikulu Mimi hayanihusu" Mfalme Pangani aliongea.
"Hayakuhusu na huku Malkia Shamsa ndio amenifukuza, huoni kama utamkasirisha " Niliongea.
"Naomba ukae kimya, sipendelei watu wanao ongea sana...." Mfalme Pangani alifunga mjadala.
Nilifyata mdomo wangu, safari iliendelea kila sehemu tuliyokutana na hoteli, Mfalme alitusihi tule.
"Matumbo sasa mbona yatatupasuka " Niliongea.
Mlinzi wa Mfalme aliniwekea upanga shingoni.
"Mfalme hapendelei watu wanao ongea sana, kwanini huo mdomo wako hausikii " Alinifokea.
"Najaribu kutafuta Mpishi mzuri atakaye furahisha moyo wangu na ndio maana tunaingia kila hoteli huna haja ya kumuwekea panga " Mfalme Pangani aliongea.
"Kumbe hekaheka zote hizi shida ni Mpishi . Najua kupika kila kitu yaani hata hii meza naweza kuipika na ikaiva kabisa " Niliongea ukweli siyo kujigamba.
"Wewe huyo upo vizuri kwenye swala zima la kupika "
"Ndiyo...."
"Tunaelekea Ikulu, endapo utalitendea jiko haki basi utakuwa Kijakazi wangu pamoja na Mpishi wangu " Mfalme Pangani aliongea akiwa kanikazia macho.
Mie huyo, moyo wangu ulishtuka utadhani nimepigwa na kitu kizito kichwani.
"Vipi huwezi kupika mbona umeshtuka" Mlinzi wa Mfalme aliuliza.
"Naweza...."
"Kwa kuwa unaweza kupika ni vyema tukaelekea Ikulu..... sipendelei maneno mengi navutiwa na vitendo " Mfalme Pangani aliongea.
Safari ya kwenda Ikulu iliendelea, ile tunafika tu kwenye lango la kuingilia tulikutana na Malkia Ada akiwa na Mtabiri Mkuu.
Safari ya kurudi Ikulu ilianza, ndani ya moyo wangu nilikuwa na mashaka. Sikuamini kama naenda kufanya kazi kweli, isije kuwa ni mbinu ya Mfalme kwenda kunichinja kwa kosa la kutia nguo ya Kijana wake kwenye furushi.
Akili ya kuomba msamaha iliniijia, nilidondoka chini ni kapiga magoti katikati ya safari.
"Sikuchukua nguo ya Kijana wako kwa ubaya....si unajua nimemlea yule. Basi hali ya kuwa naangalia nguo zake kila ni kimkumbuka ilinitawala " Niliongea.
"Nakupeleka kule uwe Kijakazi wangu na si vinginevyo hayo makosa yaliyo kuondoa Ikulu Mimi hayanihusu" Mfalme Pangani aliongea.
"Hayakuhusu na huku Malkia Shamsa ndio amenifukuza, huoni kama utamkasirisha " Niliongea.
"Naomba ukae kimya,...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/usiku-mmoja-tu-alidata-sehemu-ya-12
Maoni