USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 16
ENDELEA......
Basi nilitolewa juu ya meza kwa amri ya Mfalme.
Kama utani hivi lakini niliondoka na Mfalme.
Sadia Mimi nilipatiwa malango yangu, ilinilazimu ni kae ndani kwa ajili ya harusi itakayo fanyika siku tatu zijazo.
Waja watake wasitake jambo litakuwa..... Mfalme ndio kashapitisha hivyo.
Taarifa zilitumwa nyumbani kwetu , vile Baba yangu hana subira aliingia malangoni kwangu kwa siri kubwa.
"Naomba utoroke mbwa wewe, umewezaje kuthubutu kutembea na Mfalme hadi umependekezwa kuwa mkewe wa pili hakika sitakubaliana na hili"
"Makasiriko ya nini sikutaka pia lakini kila kitu kimetokea chenyewe.... kwahiyo upo hapa kuniambia nitoroke? siwezi kutoroka kwa sababu kama nitafanya hivyo basi Mimi na watu wengine wa ukoo wangu tutakuwa hatarini. Siwezi kuingiza watu hatarini kisa wewe. Tena usinikasirishe nisije kukuitia Walinzi wakutoe hapa "
"Wewe huyo kwahiyo tayari umeshakuwa mtu wa kutoa amri" Baba yangu aliingia kwa kebehi.
Nilitaka kumuonesha kuwa sitanii nilivuta kengele ya dharula.
Badala ya kuingia Walinzi aliingia Malkia Shamsa....sijui tu ilikuaje lakini Baba yangu alijificha siku nyingi.
"Naona sasa hata kuua mende imekuwa kipengele ni mwendo wa kuita tu Walinzi " Malkia Shamsa aliongea huku akimkanyaga mende.
Sikutaka kumuambia kama kengele ya dharula ilikuwa ni kwa ajili ya Baba yangu.
"Karibu..." Niliongea huku nikimpa ishara akae kwenye kiti.
"Ni kweli umeadhamiria kuwa mke wa pili wa Mfalme " Aliniuliza huku nikikaa.
"Sikuwa nimedhamiria lakini kwa kuwa bahati imekuja sina namna zaidi ya kupokea "
"Kwahiyo ni kikufanyia mpango wa kutoroka kabla ya hizo siku tatu utatoroka "
"Kwa ajili ya watu wa ukoo wangu siwezi kufanya hivyo naomba uache tu mambo yaende kama yalivyopangwa" Niliongea bila kufikiria.
"Baba yako ni Mwalimu mzuri sana, sielewi kwanini hakukufunza kusoma nyakati, Mimi hapa sitakuambia utoroke tena Ikulu badala yake utakutana na matukio ambayo hujawahi kuyaona tangu uzaliwe " Malkia Shamsa aliongea kisha akatega mgongo asepe, sijui alikumbuka nini aligeuka nyuma.
"Mwalimu toka humo uvunguni huna haja ya kujificha " Aliongea kisha akaondoka.
Sikujua hata amejuaje kama Baba yangu yumo uvunguni, huenda wawili hawa wamekuwa Mwalimu na Mwanafunzi kwa muda mrefu.
Baada ya Malkia Shamsa kuondoka Baba yangu alitoka uvunguni.
"Ikulu ni sawa na wacheza kamari, ukiujua udhaifu wa adui yako unatoboa lakini ukiwa hujui chochote kuhusu adui yako kutoboa kwako ni kugumu sana.....siwezi kukufundisha chochote endelea kujipambania lakini usisahau kama Malkia Shamsa ni hatari kuliko hata Malkia Ada " Baba yangu aliongea kisha akaondoka.
Sikutaka kuumiza kichwa changu kufikiria maana ya maneno yake.
Hatimaye siku ya jambo letu liliwadia, nilipendeza sana na watu wote wakawa wananiangalia Mimi.
Watu wa ukoo wangu walikuepo pia isipokuwa Baba yangu.
"Chagua kitu kimoja unachotaka nitakutimizia " Mfalme aliongea.
"Naomba umtoe Mtabiri Mkuu kwenye kifungo alichowekwa. Mrudishe katika nafasi yake " Niliongea.
Watu wote walionekana kushangaa.......
ITAENDELEA..........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni