USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 7
ENDELEA.......
Kama nilivyo tarajia tu, maneno yalisambaa kwa haraka sana.
Goma halikulazwa niliitwa malangoni kwa Malkia.
"Unajisikiaje kufananisha mtindo wa nywele na Malkia " Shamsa aliuliza.
Nililitambua kosa langu, sikutaka kuendelea kusimama nilianguka chini kuomba rehema.
"Siyo kosa lako nitamkumbusha Mfalme Pangani, kuna muda anakuwaga mwema sana kwa Vijakazi kiasi cha kukosea. Naamini kosa hili halitajirudia tena.....nitabadilisha mtindo wa nywele kuzuia watu kuzungumza " Malkia aliongea.
Nilishukuru kwa kusamehewa, niliendoka huku mapigo ya moyo wangu yakienda zigzag kwa kifupi yalikuwa yamevurugika.
"Malkia Ada anakuita..." Kijakazi wa Mama yake Ada alinidaka.
Nilimfuata kwa nyuma hasa baada ya kukumbuka ahadi tuliyo wekeana.
Mjukuu wangu anaonekana kukupenda na kwa lugha nyingine hauonekani kama Yaya " Mama wa Mfalme aliongea, acha watu wadondoke chini kuomba rehema
Maneno aliyoongea yalikuwa ni magumu, endapo yatapenya masikioni mwa Malkia Shamsa yataleta shida kubwa.
Mtabiri Mkuu alifika pia, watu wote waliondolewa isipokuwa Mimi.
"Nikimuangalia huyu binti kuna maono ya haraka nayaona..... usisahau kama hata Mimi nina uwezo kiasi wa kuona nyuma ya pazia" Malkia Ada aliongea akiwa katika uso usioonesha kucheka kama mwanzo.
"Naweza kujua ni maono gani ambayo wewe unayaona Malkia wangu " Mtabiri Mkuu aliuliza kwa unyenyekevu.
"Nilipomuona mara ya kwanza tu moyo wangu uliniambia yupo hapa kuvuruga moyo wa mfalme, lakini siku ya leo nimemuona akiwa kavalia mavazi ya Kimalkia. Naweza kujua Kwanini ulimchagua awe Yaya wa mwana wa Mfalme!" Ada alifoka.
Yaani mb...wa Mimi nimeonekana machoni kwake nimevalia mavazi ya Kimalkia? isije kuwa alikuwa amelewa.
Mtabiri Mkuu alitoka kwenye kiti kisha akapiga magoti. Haikueleweka kwanini anapiga magoti.
"Bado sijayaona hayo maono ikitokea nimeona na kuahidi kukuletea taarifa bila kujalisha ni usiku au alfajiri "
"Hapana, unanitania..." Malkia Ada aliongea kisha akavuta upanga uliokuwa mezani aliuelekeza shingoni mwa Mtabiri Mkuu.
"Naomba urudie kuongea ukweli wako wote "
"Nipo radhi kupoteza kichwa changu lakini Mimi hapa sijaona maono yoyote kwa huyu binti " Mtabiri Mkuu aliongea.
"Kwanini kule gerezani ulipoteza fahamu baada ya kuutazama uso wa huyu binti "
Mtabiri Mkuu alikosa majibu bila shaka alibanwa kona nzito.
"Nadhani ni muda wa wewe kupumzika, nitaichinja shingo yako kisha nitakuzika bila Mfalme Pangani kujua " Ada alitishia.
"Nitaongea ukweli " Mtabiri Mkuu aliongea.
"Sema huo ukweli wako kabla sijamwaga damu yako "
"Sadia ni roho ya Mfalme Pangani "
"Roho ya Mfalme Pangani?....hebu nyoosha maelezo yako "
"Muda unakuja ambapo Mfalme Pangani hatoweza kufurahia maisha bila kumuona Sadia, uwezekano wa kuwa Malkia wa Taifa hili ni mkubwa pia " Mtabiri Mkuu aliongea kwa kujing'ata.
"Kubabake bila kukutishia usingezungumza haya maneno" Malkia Ada aliongea kwa hasira kisha akarudisha upanga mezani.
Niliamriwa kuondoka, mmmh hili ni balaa ile napiga hatua kumi tu nilisimamishwa.
"Sadia " Sauti ilisikika.
ITAENDELEA.........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni