Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
02 Jan 2026
637 views
VYOTE NDANI GONGA94
USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 13
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
ENDELEA.......
Niliinamisha kichwa changu kutoa heshima kwa Malkia Ada.
"Nadhani Mimi na Malkia Shamsa tulikufukuza, kwanini umerudi hapa " Malkia Ada aliniuliza.
Nilipokosa jibu alimgeukia Mfalme.
"Pangani, naweza kujua kwanini bini huyu mwizi karudishwa hapa au kaletwa kuchinjwa "
"Hapana.....kama hauna haraka huko uendako unaweza kurudi ndani. Nitatoa tamko kuhusu huyu binti " Mfalme aliongea.
"Kwa kuwa najali kuhusu usalama wa Taifa hili nitarudi ndani...." Malkia Ada alimpa ishara Mtabiri Mkuu wakageuza miguu yao.
Kabla ya kutangazwa rasmi kuhusu vyeo vyangu nilibadilisha mavazi.
Mlinzi alikuja kunichukua akanipeleka kwenye ukumbi wa baraza la Mawaziri ambako Mfalme huendesha vikao vyake.
Nilitoa heshima kwa kuinamisha kichwa changu.
Ile Mfalme anataka kuongea Malkia Shamsa alifika. Ilimlazimu kusitisha kwanza mpaka Mkewe alipokaa.
"Kuanzia sasa na kuendelea huyu binti atakuwa ni Kijakazi wangu pamoja na Mpishi wangu " Mfalme aliongea, nilitarajia atayapima maneno kwa vitendo lakini alinipitisha moja kwa moja kuwa nitakuwa Mpishi wake.
"Nakataa " Malkia Shamsa alipinga.
"Kwanini "
"Huyu ni mwizi alipora nguo ya Kijana wangu pamoja n hereni za Malkia Ada.....nilimfukuza tafadhali sana naomba asirudishwe mahali hapa " Malkia Shamsa aliongea.
"Unawezaje kupinga amri ya Mfalme? mbona ni kama unavuka mipaka Malkia au una sumbuliwa na wivu " Malkia Ada aliingilia kati.
Sijui na wengine waliona lakini nilimshuhudia Malkia Shamsa akikonyezana macho na Ada....Sikujua wanapanga nini.
Nilipitishwa rasmi kuwa Mpishi wa Mfalme pamoja na Kijakazi wake na hakuna mtu mwingine aliyejaribu kupinga tena.
Niliamua kuthibitisha maneno yangu kuwa naliweza jiko kwa kuandaa chakula cha mchana.
Huwa siliogopi jiko lakini siku ya leo nilijikuta ni kitetemeka Mb...wa Mimi, nilijizuia kuficha mtetemo wangu nisije umbuka.
Unajua huwa napika chakula kimzaha mzaha hivi. Yaani ukiniangalia vibaya unaweza kusema hakuna kitu nafanya.
Ndani ya dakika 20 chakula kilikuwa tayari.
Niliamriwa kukionja chakula nami nilifanya hivyo, lengo ni kupima kama kina sumu au la.
Vilikuwa ni vijiko viwili tu lakini nilijikuta ni kizidisha. Nilikula vijiko sita.
Mfalme aliachia kicheko, watu wote tulicheka pia.
Alionekana kufurahia chakula changu kuliko kawaida.
Mida ya usiku nikiwa najiandaa kulala, mlango wangu uligongwa....aliingia Mfalme. Japo suruali yake ni mapana kama ya dobi masumbuko lakini nililishuhudia dudu lake likiwa limenyooka kama rula.
Mie huyu nilitulia nione ni nini anataka kufanya...
ITAENDELEA........
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
MY WANGU❤️ sehemu ya 86 na 87 Wenda mpangilio umekosewa endelea kusoma
Nyieeeee nilinuka.na deraa tu ndani nilivaa chupi tu nilitoka peku peku. Dooh rahul ana balaa et alienda na wenzie kuch...
Maoni