Mama k....aaaaah najisikia kama naumwa hivi ila Haina jinsi inanibidi kupambana Kwa Leo ninaoda ya muhimu sana na kama isingekuwa hivyo ningelala nimechoka mwanangu
Juma.....pole sana haya nilikuwa naenda sehemu ila ngoja nikusaidie kazi kidogo
Mama k.....Haina shida nitafanya mwenyewe
🌼🌼🌼💘Alisema vile ila Hali haikuwa nzuri kabisaaa hapo nikajiongeza,alikuwa Ameandaaa vyakupika pale nikaanzaa huku Yy akijilaza na muda SI muda alilala,nilipika pale huku nikiyakumbuka maneno ya marehemu mama yangu kuwa "mwanangu nakufundisha kupika hii ni Kwa faida yako na familia yako pindi mkeo atakapo kuwa anaumwa hauna haja ya kwenda kununua chakula hotel" na sema kweli mama alijua kuwaumiza watu pua na sio pua tu Bali hata chakula pia kilikuwa Bomba nikisema hivyo namaanisha kilikuwa Bomba,nikiwa nimepika Kila kitu huku namalizia kuunga dagaa Kuna mteja alikuja
Mteja....mama k sio Kwa harufu hiyo ya chakula japo mchana huwa sili kwako ila Leo itanibidi ,mama k....mama k?
Juma....mama anaumwa amepumzika
🍓🍓🍓😭Hapo nikajitokeza ila nilipigwa na bonge la mshangao Kwan nilimuona ni pini la maana
Mteja.....na ww ni nani?
Juma....mwanae
Mteja....mbona hajawahi niambia kama anamtoto mwingine WA kiume zaidi ya karo Binti yake
Juma....na mm pia labda alisahau kukujuza
Mteja....sawa ndio unaitwa nani?
Juma...juma
Mteja.....mmmhhh juma na karo wapi na wapi Kwani majina tu yanaleta uislam na ukristo mama huyu,sawa naitwa Monica mm natoka akiamka mama mwambie Leo aniachie chakula mwambie Monica
Juma....sawa
😇😇😇😇Nikarudi kupika dagaa wangu ambao walinukia sana,nilishindwa kumwamsha mama k baada kuona Nazi iliokunwa ikiwa kwenye kikombe na mm nimemaliza pika na hata hivyo sijawahi pika Kwa kutumia Nazi,ni Saa Saba kasoro kama dakika 4 hivi akaja jamaa Mmoja ambae amejaa mkaa ikiwa na maana ametoka kubeba
Jamaa.....chakula tayari?
Juma.....ndio ila ngoja kidogo kwani nilisikia.