Juma.....ndio ila ngoja kidogo kwani nilisikia kinaoda
🦜🦜🦜🦜Nikaenda kumwamsha mama kibibi na nilitumia kama dakika 4 hivi mpaka aliposhituka ila alikuwa amechemka balaa na jasho kama lote nikaona hii sio kweli nikatoka nje fasta na kusimamisha Bajaj na tukasaidiana na majirani zake pale safari hospital ya kanisa iliokuwa jirani pale,alipokekewa na Kwa haraka akapewa kitanda
Nesi....ni nani muhusika wa mgonjwa?
Juma...ni mm nesi
Nesi....haya kalipie dirishani aweze kupata huduma na atakupana na risiti
Juma....sawa....habari
Dirishani.....salama tu pole Kwa mgonjwa haya nipe hiyo form na mgonjwa anaitwa nani
Juma.... Duuuh eeeeh daaaaah
Dirishani.....vp kwani humjui?
Juma...ni kweli ila anajulikana Kwa jina la mama kibibi
Dirishani....sawa......haya peleka akapate huduma
🍓🍓💘💘Nilirudisha form na akapewa huduma,nikiwa pale ndio nakumbuka nimefunga sehemu yake ya chakula,nikachukua Boda nikauze tu kwani mpaka aje tayari chakula kinaweza kuharibika,nafika nakutaka na wateja wawili mlangoni wakiongea na nikafungua
Jamaa1...vp mama k wapi?
Juma.... anaumwa
Jamaa2....na ww ni nani?
Juma ....mtoto wake
Jamaa2 ....sawa vp chakula Leo ndio hamna?
Juma....kipo karibuni
🍓🍓🍓🍓Jamaa waliingia na Kwa bahati nzuri kulikuwa na Menu ambayo ilionyesha bei ya Kila chakula ila shida ikaja upimaji anapimaje ila nikapima nijuavyo huku nikiwachanganyia Kila aina ya mboga na baada ya kijiko Cha pili huku Nikirudishia vyakula jikoni vipate moto na harufu nzuri ikiendelea kunukia
Jamaa2....hii balaa yaaani nikitamu sana.