?NASEMA KWA MAMA
"" "" "" Hapana mama.. Usichukie.. Huyu binti siyo mtu mbaya. Na angekuwa ni mbaya kwako angekuacha hata ufie porini...
Kwanini kakusaidia ndio swali la kujiuliza.. Jana amekesha hapa hadi kunapambazuka ili kujua hali yako. Angekuwa ni mbaya kwako sisi tungekwambia ukweli.
Mimi ni daktari hapa kwa zaidi ya miaka ishiri sasa. Nimekutana na matukio mengi sana.....
Nakuomba msikilize huyu binti huenda ni msaada kwako....
Aliongea Daktari mmoja huku anamtazama yule mama kwa umakini sana...
"" "" "Uuuhhhhh.. Kwanza naombeni nipewe dawa nilizohitaji nijitibu upesi kisha mengine yafuate..
Alishusha pumzi yule mama na kuongea....
Nesi alieagizwa alikuwa ndio anaingia kwa muda ule na madawa aliyoagizwa...
Yule mama aliyapokea na kuanza kujitibu baadhi ya makovu na kumeza dawa ya maumivu..
Alikunywa na maji ya kutosha kisha kukaa vizuri kitandani...
"" "" "Hapa sawa... Pia msishtuke madaktari.
Mimi pia ni daktari tena bingwa sana hasa wa mifupa.. Nimejaribu kujikagua hapa hakuna sehemu nimevunjika, ni maumivu ya hapa na pale tu.. Lakini ndani ya dakika chache nitakuwa sawa.
Mnaweza kuondoka madaktari mniache niongee na huyu binti..
Aliongea yule mama na kumtazama Lidya aliekuwa kimya tu akitazama matukio yote...
Madaktari walitoka wakabaki wawili tu mule ndani..
""""""Mama.. Kwanza nitangulize pole na Samahani sana....
Jana nilikuwa na kazi ndiomaana nikachelewa kidogo kufika ulipo niita..
Nilivyofika pale nikaambiwa kuna mabinti wawili walikuja kukuchukua..
Nilihisi kuchanganyikiwa sana.. Nilimpigia Frenk lakimi hakupokea sim.. Nilikupigia sana na wewe pia ila hukupokea sim...
Hapo niliamini umetekwa mamaangu...
Lakini usiwe na shaka. Upo kwenye mikono salama kuanzia sasa.. Kuna watu walijaribu kudukua taarifa zangu na m kuanza kufuatilia kila simu ninayo ongea..
Kama unavyojua mtu anae tetea haki huwa na maadui wengi sana...
Naomba nisamehe mama.. Mengi utayajua tukifika nyumbani.. Kwasasa unajisikiaje.???
Lidya aliongea kwa hisia sana hadi machozi yalikuwa yakitaka kumtoka...
********
"" "" "" Basi binti.. Nimekuamini. Naomba uniimarishie ulinzi tafadhali... Nimetokea kupachukia sana hapa Dar es salam..
Nakuomba tutoke hapa hospitali, naendelea vyema sasa..
Nipelekea pale Lodge nilipochukua chumba ili nikafuate baadhi ya nguo zangu kisha nihame kabisa maeneo yale...
Mama aliongea na Lidya aliitika..
Lidya alishika simu yake na kuita Tax upesi..
Muda huo mama hakuwa na maumivu yeyote. Dawa alizomeza zilisaidia kumaliza maumivu kwa kiasi kikubwa..
Walitoka njee ya hospitali na dakika si nyingi Tax ilifika kisha kuondoka..
"" "" Tupeleke maemeo ya Ubungo.. Aliongea Lidya na Tax iliondoka..
Hawakuwa na maongezi sana wakiwa kwenye tax, ilitembea hadi ubungo..
"" "" "Haya nenda mbele kidogo.. Ingia kulia nyumba ya Ubungo plaza hapo.. Haya kata kushoto.. Okyyyyyy... Simamisha kwenye Lodge unayo iona hapo mbele.." "" " Aliongea Lidya....
Walifika wakashuka kisha yule mama akaingia chumbani kwake na kuchukua vitu vyake..
Kwasababu alilipia siku mbili basi hakusumbuliwa....
Alibeba mizigo yake yote na kupakia kwenye gari kisha wakaondoka...
" "" "Tunaenda wapi.????? Aliuliza mama yake dayana..
" "" "Nyumbani kwangu ndio utakuwa salama zaidi kuliko sehemu nyingine yeyote kwa hapa mjini...
Pia kuna mtego tunataka tumuwekee yule mzee aliekuteka...
Aliongea Lidya na kumtazama yule mama.....
" "" "" Sawa........ Nimetokea kukuamini.. Naomba unilinde hadi nitakapo rudi salama kwenye majukumu yangu Moshi.. Pia kama kuna tatizo la pesa utaniambia tutaongeza sawa.?????
Aliongea mama yake Dayana....
Gari ilitembezwa kwa mwendo wa haraka hadi Sinza Mori alipokuwa akiishi Lidya.. Nyumba aliyopangishiwa na Boss wake..
Lidya alilipia tax na kuingia ndani wakiwa na yule mama..
Waliketi kwenye kochi kisha Juice ya matunda ikaletwa na mazungumzo yalianza kuhusu baadhi ya mambo...
Siku ya Leo lidya alikuwa na usingizi sana kwasababu hakupata mda wa kulala vizuri kwa takribani Siku mbili...
*************
"" "" "" Mama yangu... Nadhani hadi unakuja hapa ni kwamba tayari unaijua kazi yangu...
Mimi nipo kitengo cha intelijensia ndani ya jeshi la ulinzi na usalama wa raia...
Nadhani mambo yote Frenk alishakwambia kiundani zaidi.. Sina haja ya kuyarudia sana...
Pia naomba nikutoe hofu kwasababu najua ulitekwa na kuteswa na bado unahofu sana hata na mimi au Frenk...
"" "" Mama Frenk ni mtu Mwema sana na nimesoma nae elimu ya Sekondari tena alikuwa rafiki mkubwa sana kwangu....
Kwahiyo hadi wakati najiunga na jeshi Frenk alikuwa akijua..
Hadi nakwenda Marekani kuongeza ujuzi na hatamie kupewa kitengo cha siri kama hiki pia Frenk alikuwa akijua...
Ndiomaana hata ulivyopatwa na tatizo Frenk alikuagiza kwangu kwasababu ananijua vyema....
**********
Pia nadhani unajiuliza sana kwanini ulitekwa.?????
Ukweli ni kuwa hiviii....
Kwa kazi ngumu kama hizi lazima niwe na maadui...
Kwa jana nilisahau nikakupigia simu kwa namba zangu za kawaida ambazo najua kabisa lazima kuna watu wamedukua na kusikiliza maongezi yangu...
Nilipaswa kukupigia kwa namba za Kazini ambazo hakuna mtu wa kuweza kudukua mawasiliano yale.
Naomba nisamehe kwasababu mimi ndio chanzo cha yote hayo.....
Pia ninamashaka sana kuwa aliekuteka ni mzee mmoja anayo kampuni ya kuingiza na kutoa mizigo Tanzania na China...
Yule mzee anatabia mbaya sana ya kuajiri watu kwa kutaka apewe rushwa ya ngono...
Kama mpelelezi basi ilinibidi nikaombe kazi ili kujithibitishia hilo na nimpeleleze kwa undani zaidi.,
Baada ya kumpa taarifa zile mkuu wangu wa Upelelezi hakufurahi sana, nadhani walikuwa na urafiki na yule mzee..
Kwahiyo mkuu wangu aliamua kumpa ukweli boss kuwa mimi ni mpelelezi kwake na siyo mfanyakazi..
Yule mzee ilibidi adukue mawasiliano yangu ili ajue vyote ninavyo vifanya..
Pia alinitafuta na kuniwekea mtego wa kutaka kunibaka mbele ya walinzi wake,
Nashukuru nilifanikiwa kumdhibiti na kuwapiga walinzi wake pia....
Baada ya hapo tulienda kumtupa mzee yule kwenye misitu ya kibaha nikiwa nimempotezesha fahamu....
******
Kilichonifanya niamini kama ni yeye muhusika wa tukio hilo, ni kwamba alikutupa na wewe kwenye sehemu ileile niliyowahi kumtupa yeye...
KWAHIYO HUO NDIO MKASA WENYEWE KWA UFUPI...
ONDOA SHAKA JUU YANGU NA JUU YA FRENK... sisi ni watu wema na nipo kwaajili ya kuwasaidia...
Alimaliza kuongea Lidya na kuinua glass ya Juice kisha kunywa fundo moja zito...
*****
*****
"" " Pole sana Lidya... Umenifumbua mengi nisiyo yafahamu kuhusu wewe..
Kwasasa ninakuamini na tunaweza kuendelea na kazi iliyonileta hapa..
******
" "" "Mwanangu.. Kwa ufupi ni kwamba... Frenk alivyofika Moshi ilibidi nimpe makazi kwenye nyumba yangu.
Kwasababu alikuwa ni mwalimu basi niliona atanisaidia kumfundisha mwanangu hata baadhi ya masomo....
Aliendelea kuongea yule mama.....
" "" "" Lakini bahati mbaya nilijikuta nimeingia kwenye dimbwi la kumpenda Frenk, nilijikuta naingia kwenye mapenzi na kijana yule na siku hiyo tulikutana Lodge na kufanya mambo hayo..
Chaajabu ni kwamba... Nilitumiwa picha za chumbani nikiwa na Frenk na hata video tuliyokuwa tukifanya mapenzi..
Pia mtu huyo alitaka nimpe Milioni 30 ili asisambaze habari zile kwenye mitandao....
Niliwaza sana kwasababu nikimpa hizo pesa huenda akanisumbua tena kutaka zingine zaidi kwasababu wao wanazo picha na video zote na wananitisha kuzisambaza mitandao..
Hii ni kashfa kubwa sana kwangu kwasababu ninaheshimika sana pale Moshi...
Mimi ni daktari mkubwa sanaa na ninayo hospitali kubwa pia inayokaribia kuitwa ya rufaa sasa kwasababu ya huduma zipatikanazo hapo....
Hizo picha zikisambaa ni kashfa kubwa sana...
Aliongea mama yake Dayana huku anamtazama Lidya kwa umakimi sana...
*********
*********
Usijali mama.. Hilo tutalitatua.. Je Naweza kuona hizo picha ili nijue namna gani zilipigwa na je ni nani aliepiga.. Huenda ni mhudumu kahusika au hakuhusika...
Aliongea LIDYA..
Picha nilizibeba jana na nilipoteza baada ya kutekwa.... Sikujua ni wapi niliziacha.....
Lakini kuna baadhi nilizihifadhi kwenye begi.. Niliogopa kuzibeba kwasababu zilikuwa za uchi sana na tulikuwa tupo kwenye Tendo la ndoa....
Aliongea Dokta kwa hofu huku anafungua moja ya mabegi yake...
Alitoa picha zilikuwa za kudhalilisha sana... Lidya alizitazama kwa muda na kumrudishia yule mama zile picha....
"" "" Mmmmhhh Frenk nae jamani... Aliwaza Lidya kimya kimya na kujikuta anacheka kwa Sauti....
Alishika mdomo kujizuia na kuinuka kukimbialia ndani kwake...
ITAENDELEA.....
Full 1000.
Whatsp 0784468229.
Maoni