Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

*NIMEKOMA MIMI 🙌* *1-5* *________________________________________*  *SEHEMU YA : 01*  Mapenzi ni kitu cha kijinga sana. Yaani yanaweza kukufanya ufanye ujinga ambao hata wewe hukuwahi kufikiria
Gonga94 · Stories

*NIMEKOMA MIMI 🙌* *1-5* *________________________________________* *SEHEMU YA : 01* Mapenzi ni kitu cha kijinga sana. Yaani yanaweza kukufanya ufanye ujinga ambao hata wewe hukuwahi kufikiria

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
unaweza kufanya. Na mimi ni mfano halisi wa ujinga huo🫩.

Ukiniuliza, nitakupa jibu simple kuwa maisha yangu ya mapenzi yalikua ya bahati mbaya kila mara. Nilikua natumiwa alafu naachwa kisha nalia kama zuzu😂.

Na kibaya zaidi nikipenda mtu, napenda mpaka napoteza akili kabisa, nakua sioni wala sisikii mtu akinionya. Hapa sasa ndo nikakutana na kijana mwingine anaitwa Michael.

Lakini kabla sijaongea sana kuhusu Michael, ngoja niwaelezee kidogo kuhusu mimi na familia yangu.
Jina langu ni Shege na jina la baba yangu ni Banza. Kwa hiyo full name yangu ni Shege Banza🤣.

Sijui baba yangu alipata wapi hili jina, ila ninalichukia sana. Yani halikai kabisa kama jina la kike. Nadhani hata bahati yangu mbaya ya mapenzi inatokana na hili jina💔. Utamuitaje bintii yako mrembo Shege???🤷‍♀️

Anyways, Nilizaliwa na kukulia Mbeya nikiwa na wazazi wangu pamoja na wadogo zangu wawili. Ambapo Mimi ndio first born wa familia.

Na kama mnavyo jua ukiwa first born eti ndo unakua mfano wa kuigwa Ila kwangu mambo hayakwenda ivyo. Kwanza nilipata zero form 4 hata cheti cha kuombea maji sikupata! Na hata nilipojaribu kusaidia nyumbani, kila kabiashara nilichofanya kilikua kinafeli. Mwishowe baba akaona bora niende Dar es Salaam kwa shangazi yangu Atu.

Nilifika Dar, nikakaa kwa shangazi kidogo! Nikawa tu nasaidia vikazi vya nyumbani, sina mbele wala nyumba ndipo siku moja Shangazi akaniambia
“We Shege, sasa ni muda wa kuanza maisha yako mwenyewe” Yaani analimaanisha nikajitegemee.

Nilishangaa maana sikua na kazi wala godoro. Nakumbuka Shangazi alinipangishia chumba na kunilipia kodi ya miezi miwili tu! Akadai msaada wake ndo uliishia pale🤦‍♀️.

Sikuwa na jinsi, nikakubali na kuanza maisha. Nikapambana pale, mwezi ule ule Nilipata kazi kwenye kibanda cha Mama Ntilie. Nilikuwa napika, naosha vyombo, naserve wateja. Mwisho wa siku kidogo nilicho lipwa kilijitosheleza kwa namna yake.

Nili kigawa kidogo kwenye kodi, umeme, chakula, dharura, alafu kingine niliwatumia wazazi nyumbani. Ilikuwa ngumu sana lakini sikukata tamaa, Nilijua ipo siku nitafanikiwa💪.

Sasa turudi kwa Michael, Labubu wangu🤣.
Baada ya miezi mitano hivi kupita nikiwa nafanya kazi pale pale, ndo nikakutana sasa na Michael. Alikuja kula kama wateja wengine ila ndo ivyo tukajikuta tu tunaanza mazoea. Kufumba na kufumbua eti tushazama penzini. Wallah Michael alini wekea kidawa maana sio kwa kumpenda huko.

Na siwezi hata kumlaumu maana Michael ni jamaa flanii ivii white, ana mwili wa mazoezi, anapenda gym, tena ana confidence sababu anajijua kabisa ni handsome wa maana.

Lakini hakuna kizuri kisichokuwa na doa. Michael hakuwa anapenda kufanyakazi. Na mfano akipata hela kidogo ananunua nguo, viatu, saa, perfume, simu mpya, ananyoa nywele na kuzingatia engo, anakua smart kabisa! Lakini mfukoni? Kapu tupu🤦‍♀️.

Na anapenda starehe, usiku club, pombe, party na marafiki zake wote ni watu wa bata! Na hata hajawai kunitambulisha kwao! Ananificha kama jipu🤣

Lakini mimi nilikuwa sioni shida, Ilimradi nilijua ananipenda basi moyo wangu mweupeee. Na kila siku nikajikuta nakolea hadi nikamuomba tuishi kwenye chumba changu kimoja🙌.

Mimi Nikienda kazini asubui, yeye analala akisubiri nirudi jioni kumpikia na kumpa hela akatumie na wenzake. Yaani mimi nikawa kama mwanaume namhudumia yeye pamoja na Mama yake.

Watu walianza kuniangalia kama vile nime nimechizika, Hasa jirani yangu na rafiki yangu, Lily, alikuwa ananiambia kila siku, “We Shege, Una akili kweli? Unatumia hela zako zote kwa mwanaume? Huoni kama anakutumia??”😳

Mimi nilimpuuza, Maana kwa mara ya kwanza toka nilipo jua mapenzi nilijisikia napendwa kweli. Sasa kwa nini nisimtunze mtu anaenipenda?🤷‍♀️

Nilianza hata kufanya kazi mbili, maana Michael alihitaji vitu vingi na mimi sikutaka alicho hitaji akikose🤣.

Mwanzo mambo yalikuwa yanaenda vizuri lakini baadaye yakawa mabaya. Boss wangu alifunga biashara tukawa hatupiki tena! Na kazi ya pili niliyokuwa nafanya nayo ikayumba yumba. Nikawa sina kazi, sina pesa, na nyumbani hali mbaya. Mara nyingi tulilala bila kula vizuri🙆‍♀️.

Siku moja nakumbuka nilienda kutafuta kazi. Niliporudi nyumbani, nikakuta Michael kashafungasha mizigo yake akitaka kuondoka.

Nikamuuliza “Unapanga kwenda wapi?”

“Narudi kwa mama yangu” akavuta mdomo kabisa🤣

“Kwanini unataka kuondoka?”🥹

Akanza kulalamika “Maisha yamekua magumu. Wakati mwingine hatuli vizuri. Na angalia ngozi yangu inaharibika sababu lotion yangu imeisha ni mwezi sasa. Niliomba ununue hukununua. Now iPhone 17 imetoka, umeshindwa kuninunulia pia. Rafiki zangu wote wana iPhone 17, mimi pekee ndo sina”😠

Nikamtazama kwa sekunde chache, nikavuta pumzi ndefu…
Unajua nini? Ngoja kidogo, nakuja………

SEHEMU YA : 02

We fikiria Michael alitaka nimnunulie iPhone 17 mpya kabisa! Wakati mimi mwenyewe natumia Nokia ya kibatani ambacho nimeifunga na raba bendi ili kipate mawasiliano 😂🤣.

Lakini kwa sababu nilimpenda vibaya, sikuona kama ni tatizo. Nilimtazama tu nikamwambia “Kwa sasa baby mambo hayako sawa lakini subiri kidogo Michael, nitakununulia kila kitu unachotaka. Lotion, iPhone 17, raba na chochote unacho taka nitakupa”

Michael akaniangalia kama vile haniamini.
“Mara ya mwisho uliniambia utaninunulia iPhone 16, haukununua. Now 17 imetoka, unadhani kweli utaninunulia? Unajua bei yake? Ni Milioni sita…”🤨

Nikacheka kwa aibu maana moyoni nilijua sijawahi kuona hata laki 5 kwa bahati mbaya. Nikamsogelea nikamwambia kwa upole “Nitafanya chochote kuhakikisha unapata hiyo simu. Tafadhali usiende, nakupenda. Unajua nakupenda baby, sio?”🥺

“Yeah, najua… na mimi nakupenda pia. Anyways! njaa inaniuma! sijala tangu asubui”

“Sawa baby, nitapika msosi chap ule! Ila please usiende”🥺

Akauliza “Utapika nini?”

“Kuna maharage na unga, tutakula ugali na maharage”😊

Michael akakunja uso, “Ugali tena? Hii ni siku ya tatu tunakula ugali. Sitaki ugali, Nataka chipsi kuku”

“Chipsi?? Hali ni mbaya Michael hata wewe si unaona jamani”

“Nilijua tu! Hata elfu 6000 ya chipsi inakushinda! Unataka nikonde nipauke wenzangu wanicheke?? Mama yangu akiniona nimekonda wakati wewe ulimhakikishia utanihudumia vizuri unadhani atakufa nyaje??….. au Shege umepata mwanaume mwingine ndo maana unanitesa??”

“Hapana baby unaelewa vibaya???…. Si chipsi kuku unataka??? Basi utakula baba hata usijali”😰

Aliposikia hivyo akafurahia sana, akanikumbatia, akanibusu nikajikuta naburudika mwenyewe. Chap chap Nikamsaidia kurudisha mizigo yake aliyoifungasha na kupanga upya nguo zake kabatini. Baada ya hapo nikatoka nje.

Kichwani nilikuwa nawaza nitatoa wapi hela ya chipsi kuku ili labubu wangu ale??… Ndo nikamkumbuka Lily rafiki yangu. Nikaenda chumbani kwake, nikagonga mlango akanifungulia. Bahati nzuri hakua katoka jioni hiyo.

Niliingia na kukaa kwenye sofa akaniuliza,
“Mbona una sura ya huzuni?”

“Michael ana njaa sana na anataka kula chipsi kuku na mimi sina hela”😪

Lily akacheka mbavu hana. Kuna mda huwa anajiuliza pengine Michael aliniloga maana sio kawaida “Yaani wewe uko serious? Huyu mwanaume anakupa nini mpaka unajitesa hivi kumfuraisha? Au Yaliyomo yamo??”🙄

“Lily nakuheshimu, please usiongee vibaya kuhusu boyfriend wangu. Ananipenda, nami nampenda”🫤

“Acha ujinga Shege. Huyo jamaa hakupendi, anakutumia tu kwa sababu anajua ukipenda mtu unakuwa dhaifu. Hebu amka!”😳

Nikakataa “Hapana. Najua Michael ananipenda na mimi nampenda Basi! Sisikilizi ushauri wa watu wengine”

“Hii ni mara ya kumi nakushauri lakini hauelewi. Inaonekana Michael amekufunga macho na masikio huoni ukweli”

“Acha izo Lily Sijaja hapa kubishana, nimekuja nikuombe uniazime elfu kumi na tano! Pleasee…”

Akauliza “ya kazi gani?”

“Ili nikamnunulie chakula Michael si nimekuambia Ana njaa?? na mimi pia njaa inaniuma. Nisaidie please…”

Lily akaniangalia na macho ya huruma akasema “Nitakupa kwa sababu nakuhurumia, si kwa sababu ya huyo mwanaume wako bwanyenye sawa?”😤

“Sawa”😣

Akasimama Akaenda kabatini, akatoa hela akanipa. Ilikua ni elfu ishirini badala ya elfu kumi na tano.
“Asante Lily”

“Usijali! Pia bado nashughulia swala lako la kazi nikisikia sehemu wanatafuta mfanyakazi nitakuambia! sikusahau ombi lako”😊

Nikajibu “Asante sana Lily” baada ya hapo Nikatoka nikaenda kununua chipsi na kuku.

Niliporudi nyumbani Michael alikua amekaa akinisubiri. Aliponiona nimeshika mfuko mkononi akafurai kama mtoto amepewa ice cream.

“Umeona sasa! Hapa ndo nimeamini unanipenda baby” akani sifia pale mimi kichwa kikajaa kama boga🤣

Nikatoa sahani chap chap, nika sevu chakula kisha Tukakaa tukala wote. Labubu wangu Alikua na furaha sana.Na sijui kwa nini nilimpenda kiasi kile wakati yeye alichojua ni kulalamika tu na kunichuna🫩.

Unajua nini kitatokea baada ya hapo? Subiri kidogo… Nakujaa

SEHEMU YA : 03

Tangu siku ile mambo yalizidi kuwa magumu, yani magumu haswaa Hadi Michael Akaamua kuondoka. Siku hiyo nilitoka kutafuta kazi, nikarudi jioni sikukuta vitu vya Michael kuanzia nguo, viatu mpaka boksa, aliacha tu nguo ambazo hakua akizivaa tena💔.

Nilikaa chini nikaanza kulia kwa sababu Michael alikuwa kila kitu kwangu, sikuwa na uwezo hata wa kuvumilia akiwa mbali na mimi. Nikatoa simu nikampigia lakini cha kushangaza hakupokea😭

Tena kwa makusudi panya yule akaamua kuzima kabisa simu yake ili nisi msumbue. Hapo nikahisi moyo unataka kunisimama. Mbio mbio nikatoka Nikaenda chumbani kwa Lily nikiwa nalia.

Kitu cha kwanza Lily alicho nijibu baada ya kumuambia Michael kaondoka ni “Labda kuondoka kwa Michael ni kitu kizuri kwako”

Nilimwangalia huku nalia nikamjibu “Hapana, siwezi ishi bila Michael, nampenda”😭

“Huwezi kuishi bila yeye ni baba yako yule?? Kwani huoni kama hii ndo chance ya kuishi maisha yako bila presha ya mwanaume yeyote? Michael kashaondoka, si wako tena. Wewe sasa focus kutafuta hela mtotoo wa kike”😤

“Hapana, kwenye mapenzi mimi sijawahi kuwa na bahati. Michael ndiye mtu wa kwanza kunionyesha mapenzi ya kweli! Mimi siwezi muacha”😭

Lily aliniangalia kwa hasira akitamani anilambe kibao sema ndo ivyo alishindwa. “Shege Una uhakika kweli huyu jamaa anakupenda?”🤦‍♀️

“Ndiyo, nina uhakika”

“Lakini yeye ni mwanaume, anatakiwa kukutunza wewe si wewe umtunze yeye! Unalea jitu zima ambalo kazi yake ni kulelewa tu”

“mambo yake si mazuri, akipata kazi atanihudumia na mimi”

“Kwa akili zako unaona Michael ni mtu wa kufanya kazi?? Mwanaume mlenda mlenda kama yule?? Ata ndoo ya maji anaweza kubeba kweli??…. Taa yenu ikiungua hawezi hata kubadilisha……. Alafu now umechacha huna chochote ndo maana kakimbia.
Wewe mwenyewe huna kazi”🤨

“Please nisaidie nipate kazi! Nikipata kazi tu Michael atarudi kwangu”

“Ivi shege umesikia kweli nilicho kushauri?? Mbona kila ninacho kushauri wewe husikii? Una mapepo???” Lily aliishiwa pozi

“Huwezi elewa jinsi gani mapenzi yanani changanya” Nilimwangalia kwa macho ya huruma, akaonekana kunisikitikia.

“Ok Kazi pekee iliyo wazi sa hivi ni ya mlinzi wa getini na wanataka mwanaume. But vumilia kidogo nikisikia kazi nyingine nitakuambia”

Sikusema kitu nikaendelea kuugulia zangu maumivu ya kukimbiwa na Michael. Jioni ile Lily alipika, tukala pamoja na nikalala kwake, sikuweza kurudi kwangu.

Sasa Asubui kesho yake nikaamka mapema nikaenda kwa Michael. Wallah sikuweza kuendelea kuvumilia maana nili-mmiss sana. Michael yeye Anaishi na mama yake, kwa hiyo nilijua lazima nimkute huko.

Nilipofika moyo uliniuma sana kumwona Michael anashuka kwenye gari moja kalii sana alafu anaendesha mwanamke maji ya kwanza. Yani mwanamke nangai haswaa🙆‍♀️.

Nilipoona vile roho ikaniuma vibaya nikajikuta namkimbilia. Bahati nzuri yule mwanamke aliondoka lasivyo nilipanga kuleta fujo asinge amini macho yake. Ajabu Michael alipo niona hakushtuka!

Nikamuuliza “Huyo mwanamke ni nani?”😡

Akanijibu kwa dharau “Mwanamke gani?”

“Uyo aliyekudrop kwenye gari?”

Michael akacheka, “Unajua siwezi kukupa maelezo yoyote coz Tulishaachana”🙄

“Hapana hatujaachana. Mimi najua bado tupo kwenye mahusiano na bado tunapendana”

“Nop! hatuko. Wewe huwezi tena kunimudu Shege! Tumekuwa tukiteseka wiki ya nne sasa Kila siku ugali na maharage. Angalia ngozi yangu jinsi ilivyo paukaa? Sing’ai tena wala siyo handsome tena. Siwezi kuishi maisha ya shida ivi. Acha niende kwa wanawake wenye pesa, wanaoweza kunitunza”🤨

Maneno yake yaliniumiza sana lakini sikuweza kumuacha. “Please, nipe nafasi nyingine. Michael Unaniacha kweli?”😭

Akanijibu “Ndiyo. Kama Ukitaka turudiane tafuta kazi yenye mshahara mzuri ili unihudumie. Vinginevyo yule mwanamke aliyenishusha ndiyo nitakua nae maana ananitaka alafu anapesa sio kitoto! Si unaona chuma anayo endesha???”

Kwa makusudi Michael Akatoka mfukoni noti nyingi za elfu 10 alizo hongwa na yule mwanamke. Weeeeh Nilihisi kuchanganyikiwa, nikaanza kutetemeka kama mtu mwenye baridi kali😰.

Binti Nikapiga magoti nikaanza kumuomba msamaha nambembeleza labubu asiniache. Mara
mama yake Michael akatokea. Akaja haraka, akamvuta Michael pembeni “Wewe msichana mbaya sana! Umemfanya mwanangu apate tabu hivi? Angalia alivyo, kakonda kama mshumaa??! Kapaukaa kama anapaka majivu!! Una wazimu wewe??? Unataka kuniulia mwanangu??”

“Mama samahani, nampenda Michael siwezi kumuacha ateseke”🥺

“Hapana! Kama unamtaka mwanangu, letee pesa. Nionyeshe una uwezo wa kumtunza. Michael ana warembo wenye pesa kibao wanaotaka penzi lake. Wewe hata hauko kwenye list yake. Michael kuwa na wewe ni huruma tu”

Baada ya kusema hivyo akamvuta Michael wakaingia ndani, wakafunga na geti. Nilibaki pale nje sijui nifanye nini. Nikaapa nitafanya chochote ili Michael arudi kwangu.

Nikiwa bado pale chini Ghafla wazo likanijia kichwani. Nilikumbuka Lily alisema kazi pekee iliyo wazi niya mlinzi wa geti na wanataka mwanaume. Nikaona sio shida kama nitajifanya mwanaume nipate hiyo kazi. Nikishapata kazi, Michael atarudi kisha tutaendeleza penzii letu kama zamani🤔.

Haraka Nilisimama, nikajifuta machozi nikakimbia kurudi nyumbani. Nilipofika nikakuta Lily anajiandaa kwenda kazini maana yeye anafanya kazi kwenye duka moja la Wahindi kariakoo.

Aliponiona nikiwa mchafu, macho yamevimba kwa kulia, akauliza “Kuna nini? Umeamka mapema, umeenda wapi?”😳

“Nilienda kwa Michael. Ila sio muhimu, cha muhimu sasa ivi ni mimi nataka kazi”

“Kazi gani?”

“Ile ya mlinzi wa geti”

“Lakini mwenye nyumba anataka mlinzi wa kiume”😳

“Nitajifanya mwanaume! Niko tayari kujifanya mwanaume ili nipate hiyo kazi. Please nahitaji kazi”

Lily akaniangalia kwa mshangao “Unamaanisha utajifanya mwanaume kwa ajili ya kazi tu, au kwa sababu ya Michael? Wewe uko sawa kweli?”😳🙄

“Lily ukishapenda utajua kwanini nipo ivi ila kwa sasa wewe tu nisaidie kuipata iyo kazi….pleasee” nikambembeleza pale weeh maana alikua hataki kabisa. Mwishoni akakubali kishingo upande

“Sawa, nitaongea na yule jamaa aliyeniambia kuna nafasi then nitakuambia” Kisha akaondoka zake kuelekea kazini.

Itakuaje???
Nakuja…….

SEHEMU YA : 04

Siku ile nzima nilikuwa mwenyewe tu. Nilichokuwa nafanya ni kumtumia Michael meseji bila kuchoka. Nilimtumia voice notes WhatsApp, nikamuomba arudi, lakini hakujibu hata moja. Ila kuziona aliziona na meseji akasoma, mfeeew🫩

Alijua kunitesa sana kipindi icho, sababu tu nilimpenda kweli mpuuzi yule. Baada ya saa nyingi za kusubiri kujibiwa, nilijikuta nimelala bila hata kujua nilipitiwaje na usingizi💤.

Majira ya Jioni nikashtuka niliposikia mtu anagonga mlango wangu. Kitu cha kwanza kilichonijia kichwani ni kwamba, Michael amerudi. Lakini wala hata hata hakua Michael na ilo lilinikata stimu balaa.

“Khaaaa! ulidhani Michael karudi eeh?” Lily alicheka huku akiingia ndani. Ndo alikua karudi toka kazini.

“Lily tacha, sina nguvu sa ivi”🫩

“Ok ngoja niseme kilicho nileta! Nimeongea na Tobias. Nimemdanganya wewe ni cousin yangu na Sijamwambia wewe ni msichana. Nimemuambia unaweza kazi so akasema ufike keshokutwa kwaajili ya kuanza kazi. Mshahara ni laki 6 mpaka laki 7 ni wewe tu na uchangamfu wako”

Niliposikia hivyo nilifurahi sana na lile dau la mshahara lilizidi kunichanganya mazima nikatamani nikaanze kazi mda huo huo.

Lakini Lily akaniambia, “Ila hii kazi ni hatari. Kujifanya mwanaume si kitu kizuri. Wakijua ni wewe ni msichana, itakuwa shida Shege”🫤

“Hawatagundua. Nitafanya kazi vizuri sana na hakuna atakae nishtukia wala hata usiwe na hofu”

“Ila mwenye nyumba na Boss wako anaitwa Byron, ila watu wamezoea kumuita Bishop. Kwaiyo Tobias ni kama tu msaidizi wake! Shege, huyu Bishop Ni mtu hatari sana. Anafanya mambo machafu na sio mtu wa utani. Kama unakumbuka kipindi kile lile kontena la silaha na madawa lililo kamatwaga bandarini??…….enhee lilikua lake ila hapakua na ushahidi wa kumkamata! Na asilimia kubwa anafanya kazi na wanaume tu hakuna mwanamke hata mmoja kwaajili ya usalama wake. Ndio maana nina hofu sana, maana akijua wewe ni msichana unajifanya mwanaume anaweza kukuua hata maiti yako tusiipate!”

Nikajibu kwa ujasiri “Usiwe na hofu Lily, Nitakuwa makini”

“Sawa, lakini ukiona mazingira si mazuri please rudi. Au kama unahitaji msaada wa haraka umuambie Tobias maana ni rafiki yangu wa zamani. Tulisoma wote sekondari. Kwakua nimemuambia wewe ni binamu yangu ana uwezo wa kukusaidia haraka zaidi”

“Hakuna shida”😊

“I wish Michael aone jinsi gani unajitoa kwaajili yake! Yani unapambana ili kuhakikisha anapata kila kitu alafu yeye hakujali hata kidogo! Shege unastahili mwanaume wa maana na sio Michael! Anyways hata nikikushauri namna gani huwezi kuelewa”

“Kwanini unasema ivo??”

“Unadhani sikujui?? Najua ushauri wangu unaingia sikio hili linatokea lile!”

Tulicheka kwa pamoja kisha Usiku ule tulikaa wote tukipanga jinsi ya kuigiza kama mwanaume. Tulifanya mazoezi ya kuongea, kutembea hata kuvaa. Ilikuwa ngumu lakini lazima nijitahidi kwaajili ya Michael.

Basi Kesho kutwa yake baada ya mazoezi ya kutosha nikaiva kwaajili ya kazi!🔥. Nilifungasha nguo chache za kiume ambazo Michael alikua akizivaa zamani. Nilihakikisha kila kitu kipo sawa ndipo nikamwambia Lily

“Shoti niombee nifanikiwe”

“Usijali! Ilo tu??? Nitakuombea mpaka uchoke” Tulikumbatiana pale kisha nikaondoka zangu.

Lakini kabla ya kuondoka, nilisema lazima nipitie kwa Michael kwanza. Sikuweza kuondoka bila kumuaga labubu wangu.

Haya nikatoka mguu mosi mguu pili mpaka kwao. Nilipofika nilimkuta amekaa nje kibarazani akichezea simu. Aliponiona nimebeba na begi alishtuka

“We Shege Unaenda wapi?”

“Nimepata kazi”😊

Aliposikia hivyo, uso wake ukabadilika akaanza kutabasamu “Mbona hukuniambia mapema baby??”

“Ni kazi ya ghafla tu alafu nilikutumia meseji lakini hukujibu”

“Nilikuwa nimekasirika baby si unajua tena??? Kwaiyo mshahara kiasi gani??”

“Laki sita”

“Woooow! Kwaiyo ina maana utafanikiwa kuninunulia iphone 17 na viatu??…. Alafu kuna perfume mpya imetoka ina trend sana nayo utaninunulia??”

Kwa mara ya kwanza nilikerekwa sana maana hakujali hata huko ninapo enda itakuaje kuhusu usalama wangu! Hakutaka hata kujua kazi yenyewe ni kazi gani! Yeye aliwaza mshahara wangu tu na vitu ambavyo angenunua kwa hela ya jasho langu🫤

Kwa kiasi fulani nikajikuta naanza kupata mashaka na hisia zangu kwa Michael. Wala sikutaka kabisa kubishana nae! Nilijibu tu “Sawa, nitakununulia”

Nikashusha pumzi nikaendelea kuongea Nikamwambia “Hii kazi inanibidi nilale huko, kwa hiyo sitakuwa na nafasi ya kukuona mara kwa mara. Ila nataka urudi nyumbani, Hizi hapa funguo. Please rudi nyumbani. Nikipata nafasi nitakuja kukuona, na nitakutumia pesa pia”

“Uko serious? Sasa umepata kazi na utalala huko, sitasahaulika kweli? Itakuaje ukiacha kuni hudumia??”

Nikacheka kidogo “siwezi kukusahau! Usijali kabisa”😊

“Sawa, nitarudi nyumbani ila hela ya matumizi utume sasa! Kwenye iyo laki sita najua utakua unanitumia laki nne au laki nne na nusu, si ndio baby?”

“Laki nne na nusu??”😳

“Ndio! Kodi ya nyumba?? Mimi nitakula nini?? Nitavaa nini?? Apo bado sijanukia, sijatoka out ku-party na masela! Come on baby laki nne na nusu haitoshi kabisa! Sema una familia inakutegemea ila ilitakiwa laki 6 yote uwe unanitumia mimi”

Mnajua nilihisi mpaka maini yanatikisika kwa ile kauli yake. Nilichofanya ni kumkumbatia alafu nikabadilisha mada “Nitakumiss. Nitarudi kukuona kila baada ya wiki mbili”

Akasema “Sawa, nitakusubiri”

Nilitaka anibusu lakini ni kama hakutaka. Nilielewa kwaiyo Sikulazimisha, Nikamuaga pale nikaondoka zangu👋🏻.

Nilipofika mbele kidogo nilitafuta sehemu tulivu nikabadilisha nguo, Nikavaa kama mwanaume kabisa! Nilifanya vile ili watu wasishtukie na kuniuliza maswali mengi yasiyoisha.

Je nini kitajiri???
Nakuja……….

SEHEMU YA : 05

Sasa basi, Tobias alimpa Lily location mahali ambapo nyumba ilipo! Niliambiwa nikifika pale nimsubiri Tobias nje ya geti mpaka atakapo rudi ili anipe maelekezo.

Ile nafika pale kwanza nilishangaa ile nyumba ilivyokuwa kubwa ajabu. Na imejitenga kabisa na nyumba nyingine, hata ukipiga kelele majirani hawawezi kusikia.

Lakini cha kushangaza, hapakua pasafi utadhani hapaishi mtu. Majani kila kona, maua hayajamwagiliwa kabisa na vumbi kila sehemu. Hata mazingira yenyewe yalikuwa ya kutisha. Ila Kamera zilikuwa kila kona, picha linaanza getini kulikua na kamera tano! Apo bado hujaingia ndani🔥.

Nilikaza moyo pale nikakaa pembeni ya geti kusubiri mwenyeji wangu Tobias aje! Wacha nikae zaidi ya masaa mawili bila kuona mtu. Nilichoka kusubiri nikasogea karibu nikagonga geti sababu kuna mda nilisikia kuna watu wanaongea ndani.

Ila ajabu ni kwamba hakuna aliyejibu. Nilipojaribu kugonga tena geti likafunguka kidogo lenyewe. Nikasema ngoja niingie tu ndani nikamsubirie huko huko coz pale nje palinichosha sana.

Huyo Binti Banza Nikaingia ndani. Ile nimeingia tu nikakutana na vidume vitano kifua wazi wamekaa wanavuta cha Arusha, moshi mwingi kama wanachochea moto😱.

Kuona sura zao tu nikasema hapa nimeyatimba! Kihere here hiki cha kuingia kwa watu bila ruhusa😂.
Alafu vile vidume vilikua vimeshaniona kwaiyo kurudi nilipo toka nilishindwa.

Mmoja kati yao akasimama akaniuliza kwa sauti ya ukali “we unaingia tu kama chooni! Unajua umeingia wapi hapa?”😡

Nikajibu kwa uoga “ndiyo… hapana… yani ndiyo, lakini…”😨😰

“uligonga geti?”🗣️

“ndiyo…….niligonga, lakini hakuna aliyejibu”

Akanicheka kwa dharau, “kwa hiyo ulitegemea tuache starehe zetu tuje kukufungulia geti?”

“hapana, samahani……”🥲

“Aya tutajie kitengo chako chap chap!”

Nikabakaki nashangaa “kitengo??….”😳😰

Wale wengine waliokuwa wamekaa chini wakaanza kucheka, mmoja akasema, “haa, kumbe hajui mahali alipofika! Uyu bhana apige kwanza push-up mia moja!”

Nikastuka “eh?”😳

Yule aliyesimama akasema “hujasikia? Mia moja push-up sasa hivi!”😡🗣️

Nilihisi damu inakauka, Mimi ni msichana ujue na sijawahi hata kufanya push-up moja! Sasa izo 100 nitaziwezea wapi???

Ila kwa hofu nikainama apo kijasho kikawa kinatoka. Nikaanza jaribu push-up ya kwanza, ya pili, ya tatu… nikachoka mbaya nikalala na tumbo. Basi Walianza kucheka mbavu hawana🤣🤣.

Mmoja akaropoka “huyu ana push-up kama demu bana!”

Mwingine akadakia “na bado anajifanya kidume kuingia kwa manyapara! Oyaa chalii, hautoki hapa mpaka ukamilishe hizo push-up zote!”

Machozi yalikua yanakaribia kutoka hamuwezi amini. Bahati nzuri tukasikia honi nje ya geti. Wote wakanyamaza sekunde moja Kisha kila mtu akakimbia haraka kuvaa t-shirt. Alafu wakajipanga kwa mstari kama wanampokea Rais. Wawili kati yao wakakimbia kufungua geti.

Mimi pia nikainuka moyo unadunda nusu ya kuchomoka. Sikujua ni nini kinaendelea, ila jinsi walivyokuwa wanakimbia kama wamepagawa, nikajua lazima ni mtu wa maana anaingia😰.

Walipofungua geti, magari matatu makubwa yakaingia kwa kasi. Gari la katikati likasimama, mlango ukafunguliwa kisha kuna mtu akashuka. Nilipomuona tu usoni, nilijua huyo ndiye Bishop mwenyewe.

Alikuwa amevaa suti nyeusi yani kila kitu cheusi. Nilipo mtazama vizuri nikagundua ana alama ndogo kwenye shavu kama alichanwa na kisu. Ila jamaa ana tisha sio siri! Izo tatooo shingoni??? Utasema ni karatasi mtu alikua anajifunzia kuchora. Sema ukimuangalia kwa jicho la rohoni bila uoga ni handsome wa maana🤣.

Nilihema kidogo nikiwa nimesimama pembeni, moyo unaniambia, “huyu ndiye Boss wangu???? Mungu nisaidie…” 🤣

Je nini kitaendelea?
Nakuja……..

Maoni

You're not logged in


Tangazo - SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*NIMEKOMA MIMI 🙌* *1-5* *________________________________________* *SEHEMU YA : 01* Mapenzi ni kitu cha kijinga sana. Yaani yanaweza kukufanya ufanye ujinga ambao hata wewe hukuwahi kufikiria

unaweza kufanya. Na mimi ni mfano halisi wa ujinga huo🫩.

Ukiniuliza, nitakupa jibu simple kuwa maisha yangu ya mapenzi yalikua ya bahati mbaya kila mara. Nilikua natumiwa alafu naachwa kisha nalia kama zuzu😂.

Na kibaya zaidi nikipenda mtu, napenda mpaka napoteza akili kabisa, nakua sioni wala sisikii mtu akinionya. Hapa sasa ndo nikakutana na kijana mwingine anaitwa Michael.

Lakini kabla sijaongea sana kuhusu Michael, ngoja niwaelezee kidogo kuhusu mimi na familia yangu.
Jina langu ni Shege na jina la baba yangu ni Banza. Kwa hiyo full name yangu ni Shege Banza🤣.

Sijui baba yangu alipata wapi hili jina, ila ninalichukia sana....

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/nimekoma-mimi-1-5-________________________________________-sehemu-ya-01-mapenzi-ni-kitu-cha-kijinga-

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nimekoma-mimi
 *NIMEKOMA MIMI 🙌*  *19&20*  Aisee ngoja niwaambie ukweli.. sijawahi kufurahia mapenzi kama jinsi ninavyo yafutaia ya Bishop Bishop
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *19&20* Aisee ngoja niwaambie ukweli.. sijawahi kufurahia mapenzi kama jinsi ninavyo yafutaia ya Bishop Bishop
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *Chapter 16&17*  Ile siku jioni akili yangu yote ilikuwa kwa Bishop
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *Chapter 16&17* Ile siku jioni akili yangu yote ilikuwa kwa Bishop
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 15  Baada ya Bishop kuondoka, nililala kwa sababu nilikuwa nimechoka sana na mwili wote
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 15 Baada ya Bishop kuondoka, nililala kwa sababu nilikuwa nimechoka sana na mwili wote
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 14  Kwa sababu Tobias alijua mimi na Lily
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 14 Kwa sababu Tobias alijua mimi na Lily
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 12  Basi Akauliza "Mbona hujala?"
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 12 Basi Akauliza "Mbona hujala?"
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *SEHEMU YA KUMI NA NANE*  Basi lile busu lilikuwa tamu sana kama chokoleti, yani lilinipeleka mbali kabisa dunia nyingine. Nikajikuta Nampa
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *SEHEMU YA KUMI NA NANE* Basi lile busu lilikuwa tamu sana kama chokoleti, yani lilinipeleka mbali kabisa dunia nyingine. Nikajikuta Nampa
NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 13  Baada ya kugundua kuwa mimi ni mwanamke, alishuka kwenye gari
NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 13 Baada ya kugundua kuwa mimi ni mwanamke, alishuka kwenye gari
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*  Mimi sikujua lolote lililokuwa limeendelea. Baada ya kumaliza kuoga, nikajifuta, nikavaa
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA* Mimi sikujua lolote lililokuwa limeendelea. Baada ya kumaliza kuoga, nikajifuta, nikavaa
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 9  Kesho yake asubuhi niliamka mapema sana, maana ndo siku ya pati. Bishop
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 9 Kesho yake asubuhi niliamka mapema sana, maana ndo siku ya pati. Bishop
 *NIMEKOMA MIMI 🙌*   Chapter 10  Basi turudi kwenye ile pati. Yule jamaa aliyenisukuma kwenye pool alifukuzwa
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 10 Basi turudi kwenye ile pati. Yule jamaa aliyenisukuma kwenye pool alifukuzwa
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *SEHEMU YA SITA*   Bishop hakuja peke yake, Alikuja na wanaume wengine watano
*NIMEKOMA MIMI 🙌* *SEHEMU YA SITA* Bishop hakuja peke yake, Alikuja na wanaume wengine watano
*nimekoma MIMI 🙌*     Chapter 8  Basi sikuwa na namna, Ilikuwa ni lazima nipike kwa ajili ya Bishop. Nikaanza heka heka pale
*nimekoma MIMI 🙌* Chapter 8 Basi sikuwa na namna, Ilikuwa ni lazima nipike kwa ajili ya Bishop. Nikaanza heka heka pale
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 7  Basi nikaanza kupika fasta ili nimalize mapema, lakini kusonga ugali wa watu kumi sio mchezo
*NIMEKOMA MIMI 🙌* Chapter 7 Basi nikaanza kupika fasta ili nimalize mapema, lakini kusonga ugali wa watu kumi sio mchezo
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

*AAAAAASH BOSS ENZO* *season two*    *SEHEMU YA KUMU*

*AAAAAASH BOSS ENZO* *season two* *SEHEMU YA KUMU*

897
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 9 na 10

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 9 na 10

479
FROM BANGI TO BABY 💞💘  SEHEMU YA 16

FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 16

433
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 8

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 8

412
FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 17

FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 17

298
TIPWA TIPWA NA MR MARVEL   SEHEMU YA 10

TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 10

209
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 11 na 12

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 11 na 12

199
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 23  na 25.

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 23 na 25.

180
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 21  na 22.

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 21 na 22.

138
SHAMIRA sehemu ya 34&35

SHAMIRA sehemu ya 34&35

84

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.43K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.2K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.74K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.2K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.6K
MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

2.44K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tatu.  👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tatu. 👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

2.44K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.43K
I LOVE YOU DADY 💘❤️💘10

I LOVE YOU DADY 💘❤️💘10

2.38K
MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

2.36K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
This pic from Ishq is pure 90s madness and I love it ! You’ve got Ajay Devgn with his serious, intense vibe… Kajol looking all fiery and expressive… Juhi Chawla Post Mpya
This pic from Ishq is pure 90s madness and I love it ! You’ve got Ajay Devgn with his serious, intense vibe… Kajol looking all fiery and expressive… Juhi Chawla
@majario LIVE

with that cute bubbly energy… and Aamir Khan being his mischievous, romantic self. What a combo yaar! Ishq was not just a love story, it was full on drama, comedy,...

 Ili kombora la Iran lifike Israel, linatakiwa kuvuka vikwazo vifuatavyo njiani Post Mpya
Ili kombora la Iran lifike Israel, linatakiwa kuvuka vikwazo vifuatavyo njiani
@majario LIVE

* Meli za kijeshi za Marekani zilizopo Ghuba ya Uajemi * Rada za Israel zilizopo Azerbaijan * Rada za Israel zilizopo Turkmenistan * Mifumo ya ulinzi wa anga ya vituo vya Marekani nchini...

SHAMIRA sehemu ya 34&35 Post Mpya
SHAMIRA sehemu ya 34&35
@majario LIVE

Mwandishi; lissa wa huru media Basi nikajiiinua taratibu tukaingia bafuni. Mwanaume akanikumbatia uku tunaoga. Aseee uyu baba ananipenda ila hataki upumbavu ata kidogo na mkono wake mwepesi kupiga .na yote sababu...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 11 na 12 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 11 na 12
@majario LIVE

Mwandiishi; LISSA Basi nikaona zena kamnyanyua yule mtoto kisha akambeba ,ni amefanana nae sana ,nikajua ni wa kwake tu yani ni lazima utu mtoto atakuwa ni mwanae, kisha akanigeukia...

FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 17 Post Mpya
FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 17
@majario LIVE

Ikabidi nikae tu kwenye piki piki maana sura alivyokuwa kaikaza mmh asije kunipiga, Kimyaa kikatawala sasa mie nilijua tunaenda kwa Tinner na moyoni nilikuwa nimempangia hayo maneno Tinner eeh mbona...

TIPWA TIPWA NA MR MARVEL   SEHEMU YA 10 Post Mpya
TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 10
@majario LIVE

🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋 Maeneo ya pale pale chuoni, Salmon alikuwa amepanga nyumba kubwa ya peke yake. Wakati akiwa chuo ndo alikua anaishi hapo, ila siku za weekends kama hana mambo mengi ndo anaenda...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 23  na 25. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 23 na 25.
@majario LIVE

Mwandishi; lissa wa huru media Basi kuanzia apo nikawa sasa kidogo naelewana na baraka. Tena mimi ndo napenda sana kuongea nae. Yani sanaaa. Napenda kucheka nae sana. Na kun jinsi...

FROM BANGI TO BABY 💞💘  SEHEMU YA 16 Post Mpya
FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 16
@majario LIVE

Usiku wangu ulikuwa mzito sana, maneno ya D kusema kuwa Veda anatembea na wanawake wengi, niliyaamini kabisaaa Bila shakaa kwa maana Yeye tu hana mwonekano mzuri ametuna tuna hovyo anakuwa...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 9 na 10 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 9 na 10
@majario LIVE

Daaah nikaona mtoto kachomoa leo mana sio powa , ana vipengele sana uyu demu , ila unyama, hatachomoa kila siku, ni suala la muda tu, mana sijawahi kumtaka mwanamke ,...

SASA NAKUPENDA Sehemu ya 21  na 22. Post Mpya
SASA NAKUPENDA Sehemu ya 21 na 22.
@majario LIVE

Mwandishi; lissa wa huru media BASI nikapanda kitandani kwangu. Nikijutia sana nilichokifanya mana mh . Nilikuwa nasababisha ugomvi mkubwa wa wazazi mungu wangu. Yani mama yangu alikuwa anaachwa leo...

SARE YA SIMBA YA JANA INA THAMANI KULIKO INGESHINDA.??? Post Mpya
SARE YA SIMBA YA JANA INA THAMANI KULIKO INGESHINDA.???
@majario LIVE

Hatimae jana tambo za Dabi zilipata majibu kwa timu za Simba na Yanga kutoka suluhu ya bila kufungana(0-0). Kwa maana hiyo timu zote ziliambulia pointi moja moja. Mchezo wa jana pamoja...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 8 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 8
@majario LIVE

Zena akasema kwaiyo manager unataka kuniuza ama ni vp, yule manager aksema , naomba uelewe kuwa ukifanya kazi katika hii bar, mteja kukushika sehemu yoyote ya mwili wako ni kawaida,...

*AAAAAASH BOSS ENZO* *season two*    *SEHEMU YA KUMU* Post Mpya
*AAAAAASH BOSS ENZO* *season two* *SEHEMU YA KUMU*
@majario LIVE

Jambo likawa lelelele, Yaani ni patashika nguo kuchanika, Kwa upande wangu Walahi nilikuwa nikifurahi tu, na amina alikuwa akilia tu nakuomba msamaha. Enzo wa watu mwaya akachukua muda wake na kumuelezea...

TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 9 Post Mpya
TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 9
@majario LIVE

🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋 Mbali na ivyo zile zawadi alizo tumiwa Noela zilimuuma vile vile. Alihisi Noela hastahili vitu vizuri wala maisha ya kifahari. Alitaka kila kitu kiwe chake, wanaume wote wawe wake. Hata...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 6 na 7 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 6 na 7
@majario LIVE

Mwandiishi; LISSA Basi bwana , mwanaume wala sikuwa na shaka, kazi zote ambazo nilibakiwa nazo pale ofisini, nikamuachia ibraaa, na ukiacha ushikaji, mi bafo ibra ni mkubwa wake wa kazi,...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest