PILOT SITAKI INANIOGOPESHA SEHEMU YA 12
π³π³dada alishangaa akauliza we mtoto wewe umeanza lini Yan unasiku ya kwanza kazini mshapendana na mtu na mshagombana ilikuwaje, nikamjibu ni stori ndefu ila taarifa ndo iyo, dada akaniuliza kwaiyo we mtoto unatoka na mtu n kakaake au sio umeamua kula boga na ua lake. Ila dadaπkwani mie nimekwmbia natoka na Freeman uyo si shobo zake tuu mie natoka na Kendrick. Dada akasema sawa enhee niambie na wewe Kuna Nini nikaanza kumpangilia nilivomtajia tuu Jayson akaanza kucheka mwenyew π nikajua tu hapa tayar watu wanapendana hawa nikamuuliza sasa kwanini unambania mtoto wawatu kama unampenda, dada akasema mie mtu mzima najua ninachokifanya kwaiyo tulia, eeeeh nikamwambia sawa dada.
Baadae tumekaa na dada tunaangalia tv sms ikaingia kuangalia ivi nimeonganishwa kweny group la kazini alafu Ratiba imetumwa nikafurahi baada ya kuona naingia kazini baada ya siku tatu kutoka Leo, Ila sijakaa saw sms ikaingia kutoka Kwa Kendrick eti ananiambia kwaiyo ukaamua utuchanganye Mimi na kakaangu mkubwa, nikamjibu tu asiejua maana haambiwi maana alafu nikakaa kimya na nikamuweka archive maana ananisubua. Ila ndani kwangu nilikuwa na ugomvi mkubwa sana kati ya Hisia na Akili, Hisia zilikuwa zinakinzana sana maana nasema sitaki kuongea nae Tena ila nilivyomjibu hakunijibu ten nikawa najihisi vibaya nikawa Hadi nakumbuka alichonifanya kule hoteliniπ mambo mazuri ambayo sijawai Fanya Yan nikawa nahisi upuuzi tuu na nilikuwa nimekaa na dada sebleni nikatoka nikaenda chumbani kulala maana nilikuwa nawaza ujinga sana.
Nilivyofika chumbani tuu nikafika kwenye kitanda maana ilikuwa ni usiku sana, nikalala fofofo. Kesho yake nikaamka saa nane mchana, Tena baada ya kuamshwa na simu ilikuw inaita kuangalia ivi alikuwa ni dada kanipigia nikapokea, Dada akaanza na kunilaumu hivi we mtoto unataka kumuua mtoto wa mwanamke mwenzio eeeh nikauliza kwanini akasema Yani Freeman ananipigia simu Hadi anataka kulia mkaka wawatu anasema upo na wanaume wengine uko humpokelei yeye simu yake.
Yan Nikabaki nashangaa π³uyu mwanaume ananini lakini hajanitongoza ila anawivu hivi kwastaili hii nikimkataa sindo atajiua uyu, nikamwambia sawa subri niangalie dada akasema sawa ila nimemuelekeza nyumbani anakuja sasahiv, eeeeh we dada mbona unajichukulia maamuzi mkono akasema utajijua mwenyw ila ndo nshamwambia nikasema Aya sawa. Nikaanza kuangalia missed calls Eeeh Mungu wangu nimekuta Kuna missed calls zake 43, khaaaa π Yan sijawai kuona Aya mambo.
Sijakaa sawa ilinimpigie naskia mlango unagongwa kwa haraka haraka nikajua tuu uyu ni yeye nikaenda kumfungulia akaingia bila hata salamu akaanza kukagua namuuliza we una nini eti anasema namfuta uyo mwanaume wako anaekupa jeuri π³, nikamuacha amtafute akimpata aseme. Nikakaa kweny kochi
Mwanaume akasearch mpaka akachoka akaja sasa limemshuka shuu, nikamuuliza hivi wewe unashida gani lakini hata kama ndo kunipenda au ndo wivu huu wivu gani kwanza hivi unanijua vizur alafu istoshe we siunamchumba wewe, akashusha pumzi kwanza Kisha akawasha simu yake akaingia sehemu ya messages akanipa nisome nakuta Kuna sms zake na mchumba ake eti wamegombana na uyu mwanaume alivyomwehu kamtumia mchumba wake picha yangu eti mie ndo girlfriend wake mpya π‘ivi uyu mzima kwel upstairs.
Itaendelea ......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi