,Chapter 9
'Ameshaniacha, haya pambana ukampe utamu ninao mpa, nikajikuta naropoka...
" hivi unajikuta nani na hako ka mimba chako, usifikiri kaka yangu anakupenda, ni kwamba anakuonea huruma kwa sababu ulimsaidiaga utotoni..
"najua anipendi ila ndio anataka kunaoa, usijali tutapendana wakati wa ndoa, na wewe ndio utakuwa mshenga wetu...
Akataka kuja kunileta vurugu, mama yake akatokea kisha akasema " kuache huyo asije akatufia na hiko kitumbo chake, sikutaka kumjibu, maana nilifundishwa kuwaheshimu watu wazima, wakaingia zao chumban nikasikia wanaongea mpaka wanacheka, nilikuwa na njaa sana, nikaenda jikoni nikakuta mkate na mayai, aisee nilipiga mkate mzima na mayai matatu nikashushia na juice kwa raha zangu, sasa kama mimba ndio inataka nile hivyo mimi ni nani niisononeshe....
Wameshamaliza kujichekesha kama wamehongwa bia za offer wakatoka na Yule wifi yangu wa mchongo ni kama alikuwa anampelekesha mama yake, kwa sababu alimuambia mama yake akamletee chai na mama akaanza kwenda jikon kumletea chai kweli..
Nashangaa anaanza kulalamika na kusema nani kala mkate wote huu na chai kamaliza... " ni mimi, nikasema kwa sauti ya kujiamini....
Yule mama akatoka jikon kwa jazba kisha akaanza kugomba kwa kusema "unahisi hapa ni kwenu, unajua ule mkate tulitakiwa kula nyumba nzima na shea yako haikuwepo..
sasa kama mtoto alikuwa anasikia njaa, kwanini nisimlishe, ety mama mwanao akisikia njaa hautampa chakula, nikasema kwa sauti ya kujiamin...
"wewe binti umechanganyikiwa, yaan unaongea kabisa kwa kujiamin, kwani hio mimba ni ya mwanangu, kwanza mwanangu hakupendi anakuonea huruma tu, alafu unakuja kwenye nyumba unajifanya wewe ndio mother house unataka kuongoza kila kitu humu ndani, akawa anasema Yule mama, ila kabla hata sijajibu nikasikia sauti nyuma yangu ilikuwa ni ya Solomon akisema ww mwenyewe mama unajua kuwa alice ndio kila kitu kwenye hil nyumba, sasa mchefueni akiwafukuza mimi sina pa kuwapeleka....
"yaan unampa kibali huyu kibaka wako cha kutunyanyasa, na wakati unajua kabisa kuwa mimi ni mama yako na huyu ni mdogo wako, na hauna familia nyingine zaidi ya hii, au huyu mwanamke amekuroga, akawa anaendelea kulalamika mama yake na Solomon akaanza kucheka kisha akasema " ubaya ni kwamba hajaanza kuniloga sasa hivi, alianza kuniloga wakati ambapo nina miaka kumi, wakati ambapo alikuwa anaiba vyakula nyumban kwao vyenye libwata na akawa ananiletea mimi nile, wakati ambapo hata huyo anaesema ni ndugu yangu hakuwepo kabisa.
mama nikakuongezee mkate mwingine, sitamani mwanangu akae bila njaa, akasema Solomon, kiukweli huwa sitaman kufarakanisha familia za watu, ila nilikuwa najisikia vizuri sana wakati ambapo Solomon alinichagua mimi na akanitetea mbele ya ndugu zake...
"nataka lollipop nikasema, akatabasamu kisha akasema " kaaa hapa naenda kukuletea na mtu yoyote Yule ambae atakukera nambie nikirudi nitashughulika nae, kisha akaondoka kuelekea dukani...
Nikajikuta namuangalia huku natabasamu, sasa kama alikuwa ananipenda hivyo wakati wote huo, kwanini hakuwa ameniambia kipindi chote hicho mpaka nilipoanza kufundishwa na dunia, nikawa najiambia pale, na mama na mwanae wkaakunja sura kama wanajisaidia kinyesi kigumu vile kisha wakaondoka kwa hasira na kwenda kwenye vyumba vyao.....
ITAENDELE
AChapter 10
Basi kweli Solomon wangu alikuja na lollipop. mbili zile kubwa nyekundu pamoja na chocolate, sijui nani alimuambia kuwa napenda, kisha akanishika mkono tukaingia zetu chumban, nikaanza kula huku natabasamu, akawa ananiangalia, nimemaliza akanisogelea kisha akasema " haurusiwi kumpandishia sauti mama yangu, hata kama anakunanga kiasi gani, naomba usije kubishana nae, maana Yule atabaki kuwa mama yangu, ila jane akikuletea za kuleta, kama una uwezo wa kumzaba vibao wewe mzabe tu mpaka awe na adabu...
siwez kubishana na mama yako, wewe mwenyewe unajua, nikajibu akatabasamu kisha akanambia nimeenda kutafuta mshenga, maana sio ustaarabu kukaa na wewe na wakati wazaz wako wapo, tena wapo mtaa huu huu, leo naenda kukutolea posa, na kabla haujajifungua nitahakikisha tunafunga ndoa, nimechoka kukaa mbali na wewe mamaa, nataka niwe karibu yako, nilihisi joto lako, na kila ninapotaka huduma yako niipate tena kwa wakati....
"wanasemaga kulala na mwanaume ambae sio baba wa mtoto, kuna sababisha changamoto wakati wa kujifungua, huoni kama ukiendelea kunitaka kimwili utaniletea shida wakati wa kuzaa...
Nikashangaa anacheka kisha akasema " kwani baba wa mwanao unamjua..
"hapana simjui, nikajibu..
"vipi kama mimi ndio baba wa mwanao?..
hauwezi kuwa wewe, maana wewe ni mstaarabu na hauwezi kumlazimisha mtu kimwili bila ridhaa yake alafu ukakimbia, Yule kijana ni mshenzi, amesababisha mpaka wazaz wangu wamenifukuza nyumban, bila kujua kuwa hata sikuwa na mahusiano nae, nikaanza kulalamika alafu nikakaa kimya kana kwamba kuna kitu nawaza kisha nikamuuliza Solomon..
hivi kuna uwezekano jinni akakubebesha mimba?..
"kwanini umeuliza hivyo?..
" nahisi ni jini, lakin alitumia umbile la mtu ninae mjua, kwa sababu kwanza alikuwa anatokea kama jinni, kisha namna ambavyo ananirudisha nyumban hata wazaz wangu wakifunga mlango hata hawajui nimeingizwaje ndani, na wakati mimi ni mtu mzima na ni mzito, hivyo mpaka afanikiwe kuniingiza ndani ni lazima wangesikia tu, nikaanza kusema...
Solomon akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kucheka na kusema " Mungu wangu, lazima atakuwa jinni, huyo, sasa itakuwaje na una mimba ya jinni, alafu wanasemaga kuwa mimba za jinni huwa haziwag za muda mrefu, yaan unaweza ukabeba mimba leo alafu kesho ukajifungua, sasa wewe mbona unaenda mwenzi wa sabaa huu, au anataka uje uzae kobe..
Kwa namna ambavyo solomon alikuwa anaongea, nikajikuta naanza kuogopa, akawa ananicheka na kunambia " hatimae mke wangu kabeba mimba ya jinni, alafu huyo jinni sijui amenifata na mimi, maana ni kama ananilazimisha nikuoe na wakati una mimba. yake...
"basi kama ni hivyo usinioe, sitaki kuja kukuletea matatizo, nikasema kwa sauti ya wasiwasi sana, aisee Solomon alicheka sana kisha akasema " sikujua kama wewe ni muoga kiasi hicho, kama ingekywa ni mimba ya jinni, ungeshazaa na wangekuwa wameshachukua mtoto wao kitambo, hio mimba nina uhakika ni ya mtu unaemjua, naomba tusiongelee hilo, kwa sababu mimi nakupenda na sitaki hata umuongelee jinni kwa sababu naona wivu, maana nilishaapa kuwa wewe ni wangu pekee yangu....
Basi akanisogelea kisha akanipakata na kusema "nakupenda sana alice..
Nikajikuta natabasamu tu..
Sasa nilidhani ni utani kwenye swala la mshenga, ila kwenye majira ya kama saa sita tukasikia hodi, nikahsangaa solomon anasema " wameshafika wewe kaa hapa nitakuja kukuambia kinachoendelea.... "kina nani?, ikabidi niulize...
"washenga, akasema kisha akatoka zake nje..
.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni