0742133100
Mjomba alisimama kwa nyuma yetu na gari yake, wakati huo hatukuwa hata na wazo alitizama mchezo mzima, kisha General alipo niachia nilitembea kwatabu sana hadi getini, na kisha niligonga geti mlinzi akanifungulia nikaingia ndani, nilienda moja kwa moja chumbani kwangu nilikuwa namaumivu sana,
General alipo nishuhudia tayari nimeingia ndani ndio akaingia nayeye kwenye gari yake na kuondoka zake, mjomba alishindwa afanyeje akasogea na gari yake hadi getini, kisha akapiga honi na mlinzi akamfungulia geti, alafu akaingia ndani alienda mpaka kwenye paking yake, kisha alishuka baada ya kupaki, alikuwa na hasira kweli baada ya kutuona, akaenda mpaka chumbani kwake, mkewe alipomuona na hali hiyo, akamuuliza:
"Mumewangu kulikoni tena, mbona upo hivyo eeh! Niambie Mumewangu"
Kisha mjomba alimuhadithia shangazi kilakitu alichokiona hapo nje, akaongezea na:
"Sijui hata anatatizo gani maana nilivyomuona anavyo tembea, ni kama hayupo sawa kabisa, haya nenda umtizame sijui ananini kama ameaguka kamuhudumia"
Pamoja na hasira zake kwangu mjomba, lakini ananipenda na kunijari sana kama binti yake wa kumzaa hivyo alimuambia shangazi aje kunitizama kama kunakitu kimenipata kweli shangazi alikuja hadi kwenye mlango wa chumbani kwangu na kuanza kugonga huku akiniita:
"Laura!......Laura kipenzi!"
"Mama"
"Ndio kipenzi"
"Fungua ingia"
Kisha shangazi alifungua na kuingia mimi hupenda kumuita shangazi mama kwani ndio alinilea na alinipa upendo mzuri kaka mama hata yeye huniita mwanangu ndio tulivyozoeshana alipo ingia chumbani kwangu alinikuta nimesha jilaza kitandani tena nimejifunika na duvet langu akaniuliza:
"Kulikoni kipenzi mbona umekuja tuu na kupanda kitandani hata hukuniambia vipi huko ulifurahia kuwa na rafikiako Ethane eeh! Na kingine eti vipi umeumia mguu kwani maana mjomba wako kakuona ukiingia ila ulikuwa unatembea kwa tabu sana niambie mrembo wangu?
Nilishtuka kwanza kuskia mjomba kaniona nilipokuwa naingia nikamuuliza:
"Weeeh! Mjomba kwani alikuwa amesharudi?
"Hapana labda mliongozana maana ndio kaingia sio muda"
"Mungu wangu, atakuwa kaniona nikiwa na General sio?
"Nikweli maana kaja na hasira kamazote"
"Sasa nitafanyaje mama nisaidie"
"Hilo halina shida sana nataka kujua umepatwa na nini mpenzi"
"Usijali mama nilipoenda kambini kwa General, niliwakuta wapo mazoezini hivyo aliniambia nijiunge nao, ndio maana hata mapaja yananiuma sana, ila najua nitakuwa sawa baada ya muda tu"
"Ooh! Pole kipenzi je umekunywa dawa zamaumivu?"
"Ndio mama"
"Ila wewe sikuamini hapo kwenye dawa, ngoja nikuchukulie na umeze mbele yangu sawa"
"Dah! Mamaa jamani!
"Tulia hivyo hivyo ngoja nakuja"
Alienda na kuja na box la msalaba mwekundu, linakilakitu vifaa tiba na dawa za maumivu, akaa pembeni yangu kisha alitoa panado na kunipa, kisha alichukua maji yakunywa na kunipa, nikameza na kisha akaniambia:
"Hapo sasa nisawa kipenzi changu"
"Haya sasa naomba nilale"
"Sawa unaweza kulala lakini je chakula umekula?
"Aah! Mamaa"
"Mama nini? mvivu wakula wewe, hulali bila kula hapa, ngoja nikachukue chakula sasahivi"
Kisha mama aliinuka nakwenda jikoni, akachukua chakula na kuja, kisha alikaa na kuanza kunilisha, huyo ndio mama yangu mimi, hatoruhusu kabisa kuona nalala bila kula, kisha alipomaliza kunilisha akaniruhusu sasa nilale, kisha nikajilaza hapo kitandani, na shangazi aliondoka na kuniacha, baada ya muda simu yangu iliita kuitizama alikuwa General, nikaipokea akaniambia:
"Mpenzi wangu tayari nimeshafika nyumbani namimi, ila nime kumis taya mwenzio"
"Asante"
"Baby nakupenda sana Laura, kiukweli umeongeza upendo mkubwa sana ndani ya moyo wangu, na hata itokee kitu gani hakika nitalipambania penzi lako, umenifanya niwe kichaa wa mapenzi"
"Unajua mjomba katuona hapo getini ulivyo nikumbatia na kunichum, hadi mwendo wangu kamuambia shangazi, ila nimejitahidi kuongea na shangazi atalitatua yeye mwenyewe"
"Shangazi yako nimtu bora sana Laura, nimempenda pia"
"Haya sasa naomba nipumzike kwani ninamaumivu sana"
"Natamani ningekuwa hapo, nikukumbatie hadi asubuhi, pole mpenzi wangu na nisamehe kwa dharti yamoyo wangu nakuomba, na ninazawadi yako juu yawewe ulichonitunukia leo, japo haita fikia thamani ya usichana wako, ila nitaomba upokee sawa"
Nilijisikia vizuri sana, kusikia maneno mazuri namatamu kutoka kwa General Ethane, nikajiona kumbe ninathamani kiasi hicho, nikamuitikia:
"Sawa mpenzi wangu"
Je unathani nikweli Ethane anaiona thamani ya binti mrembo Laura na je atamtunukia kitu gani eeh! Tafadhali endelea kufuatilia................
.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni