Menu






Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track
Tangazo - SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili

GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 10 Nilipo mkumbatia kwa nyuma alishtuka na kunishika mikono

17th Dec, 2025 Views 200

kisha aliniachanisha na kugeuka ndipo aliponiona mimi akasema:


"Laura?


"Ndio mimi Laura "


"Mbona upo hapa mpaka sasahivi si mmeruhusiwa kuondoka wewe imekuwaje umebaki hapa?


"Nilikuwa nakungoja wewe General"


"Mimi,  kwanini?


"Nilikuwa nataka kuongea na wewe General"


"Haya niambie unataka kuongea kitu gani Laura?


"Nikweli nakupenda  sana General,    japo nilikuwa nazikataa hisia zangu zakweli,   lakini tangu umeondoka kambini hisia zangu juu yako zimezidi kuongezeka,   nimeteseka sana sili silali nakumis sana mwenzio,  kunamuda  nilikuwa  nalia tuu nikitamani kukuona ata kukusikia tuu  japo sauti yako,   moyo wangu  umeondoka nao General nisamehe mimi nakuhitaji mno"


Niliongea huku nikilia kwa hisia zandani ya moyo,  General alinitizama kwa romantic sana  kisha alinivuta na kunikumbatia,   kisha akaniambia:


"Haya ingia kwenye gari tuondoke sasa,   au unamsubili mjomba wako"


Alinifungulia mlango wa gari,  kisha  nikamjibu:


"Hapana nilimuambia atangulie,   kwani nakusubili wewe kunajambo nataka kuliweka sawa"


"Wow!  Mbona hujamuambia ukweli unaenda kulipambania penzi lako eeh! Hahahaaa"


Aliongea kwa utani  tukacheka wote kwa pamoja,   tuliingia kwenye gari na kuanza safari ya kurudi mjini Dar-es-Salaam, akaniambia:


"Laura  kiukweli nilijua nimekupoteza,   nilihisi kuwa nilikuwa najidanganya mwenyewe kwamba unanipenda,  na kumbe haukuwa unanipenda kweli, hakuna siku nilijisikia vibaya kama ile siku uliyiniambia hunipendi nawala hutokuja kunipenda,  niliumia sana sikufichi na machozi yalinitoka nilijikuta nalia kwa mara yakwanza,   sijawahi kumlilia mwanamke ila ulinifanya nilie wewe, na hata nilipo ondoka nilikuwa najitahidi sana kukufuta kwenye kumbu kumbu zangu,  hata nilipokuja hapa sikutaka kukuona kabisa,   ndio maana nilipo maliza kilichonileta hapa nikaingia haraka  kwenye kikao,   ili nilitegemea nikitoka nitakukuta umesha ondoka kabisa maeneo haya,  asante mungu kwa marahii naona umenipa kile nilichokuwa nakitaka nilichokuwa nakiota sikuzote,  Laura nakupenda sana hujui tuu"


Aliongea na kunitizama usoni kwa macho yake mazuri,   kisha alinyanyua mkono na kunishika usoni kwangu,   huku akiwa ananitizama kwa macho yamahaba, nilijikuta machozi yananitoka kwa raha niliyokuwa nayo, nikamuambia:


"Ethane siamini  upo namimi hapa leo hii hapa,   Ethane hujui tuu nilifikia hatua kila alieniona kambini aliniona kama nimechanganyikiwa,   nilikuwa kichaa kwaajili yako,  namshukuru sana Nancy kwani alikuwa nami bega kwa bega kuhakikisha namalizia mafunzo yangu,  sizani kama ningefika leo hii hapa nahisi hata ningefukuzwa kambini au ningekufa,  kwani nilidhoofika kabisa sikuwa nakula wala kulala mimi mwenzio,  sikujua kama mapenzi ndio yananguvu namna hii,  nilichukia huu ulimwengu ulioniingiza alafa sikuoni kabisa nilikuwa gizani pekeangu"



"Ssshii"


Alinishika mdomo na huku akinizuia nisiendelee kuongea huku machozi yalikuwa yakimtililika, akaniambia:


"Nipo hapa sasa sitaki kuona huli wala hulali,   nataka kuona tabasam lako tuu,   mimi ndio taa yako kwenye huu ulimwengu mpya  haupo mwenyewe tena,  sawa kipenzi changu"


Niliinuka nanilivyo mwembama sasa,   nikaenda kumkalia miguuni huku akiendesha gari ,   nilimkumbatia kama mtoto mdogo  huku nikimbusu kila mahali, nampenda sana General Ethane,  aliniambia:


"Tulia hapa siku zote,  kwani hapa kifuani kwangu  ndio sehemu sahihi kwako tulizo lamoyo wako,  namimi pia"


"Asante sana Ethane,  upo sahihi kabisa"


Aliendesha gari kwa kasi sana niliwa nimetulia tulifika sehemu moja njiani  nimaharufu kwa chakula General aliingiza gari hapo na kupaki,  kisha alifungua mlango na kunifungulia nishuke, akaniambia:


"Nataka nikakulishe mtoto mzuri,    maana sitaki kuona unapitia kipindi kigumu tena,   wakati upo namimi  sawa?



Nilitabasam kisha alinishika mkono baada ya kufunga mlango  wa gari,  na tuliingia moja kwa moja restaurant,   hapo tuliandaliwa meza nzuri na muhudumu kisha walitusikiliza nini tunataka,  General aliniambia:


"Kipenzi changu agiza chochote unachotaka kula sasahivi,   nitakulisha"


Kiukweli General  alikuwa ni mkaka mwenye mahaba sana,   kwa kumtizama tuu yaani utajua,   na ndio maana wadada wengi wamekuwa wakivutiwa kuwa nae,  lakini bahati mbaya hakuwa anapenda kujiingiza tuu hovyo kwenye mahusiano,  mpaka alipokuja kukutana namimi, japo kuwa nilikuwa namkataa ila kiukweli moyoni nilimpokea kwa mikono miwili kabisa, na kumkaribisha ndani ya uvungu wa moyo wangu,  nampenda mpaka mimi mwenyewe najishangaa,  basi bwana chakula kililetwa hapo,  nikataka kuanza kula lakini  General akanianbia:



"Nilisema leo nakulisha mimi,   hivyo tulia hivyo hivyoo sawa"


Nilitabasam nakuitikia kwakichwa,   kisha alinawa mkono General na kuanza kunilisha,    tena huku akikipuliza kwa mdomo wake  kwanza  ndio ananilisha kama mtoto,   na kunifuta mdomo vizuri yaani  achatuu,   nilikuwa naona aibu lakini General ndio kaamua, wakati tunakula hapo muda ulikuwa umeenda, General akaniuliza:


"Unakaa dar sehemu gani mpenzi?


"Mimi nakaa maeneo ya kunduchi,  wewe je?


"Mimi naishi dodoma ila hapo dar huwa nafikia kambini,  nitakupeleka hadi kwenu  usihofu, alafu nyumbani unaishi na nani?



"Mimi nilichukuliwa namjomba  tangu nikiwa mdogo,   mjomba  na mkewe wamenilea kama mtotowao wakuzaa"



"Ok vizuri"


Tuliongea huku akiendelea kunilisha chakula hapo  muda huo wakati General ananilisha kumbe mjomba nae alishuka hapo kula alishukudia General akipuliza chakula nakisha akanilisha mjomba aliganda akinituzama  nilishtuka nilipomuona nilishindwa hata kujitetea




Je unavyo dhani mjomba wake Laura atafanyaje na kushuhudia kabisa Laura analishwa kimahaba na General nini kitatokea endelea kuifuatilia.............
Tangazo - SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20

SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 10 Nilipo mkumbatia kwa nyuma alishtuka na kunishika mikono  >>> https://www.gonga94.com/semajambo/general-sili-silali-juu-yako-sehemu-ya-10-nilipo-mkumbatia-kwa-nyuma-alishtuka-na-kunishika-mikono



#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #war

#love #photooftheday #fashion #beautiful #happy #tbt #followme #picoftheday #art #nature #travel #fitness #motivation #life #fun #instagram #friends #smile #food


 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
MWENDELEZO SOMA HAPA

Maoni

You're not logged in


gonga94 official track
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi general-sili-silali-juu-yako-sehemu-ya
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO    SEHEMU YA 05  Hatimae nilifika  kwa General
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 05 Hatimae nilifika  kwa General
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO         SEHEMU YA 09    Kisha niliinuka taratibu na kuondoka zangu
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 09 Kisha niliinuka taratibu na kuondoka zangu
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO   SEHEMU YA 04  Kulipokucha tena alfajiri namapema,   filimbi ilipigwa,  wote tuliamka na kwenda mazoezi
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 04 Kulipokucha tena alfajiri namapema,   filimbi ilipigwa,  wote tuliamka na kwenda mazoezi
GENERAL SILI  SILALI   JUU YAKO       SEHEMU YA 08  Nilimtizama sana nilikuwa natamani niipore simu,  lakini nikajisemea kama kweli
GENERAL SILI  SILALI   JUU YAKO SEHEMU YA 08 Nilimtizama sana nilikuwa natamani niipore simu,  lakini nikajisemea kama kweli
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO   SEHEMU YA 03  Walipo fika Catrine alikuwa chini na mimi nilikuwa juu nampiga Catrine
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 03 Walipo fika Catrine alikuwa chini na mimi nilikuwa juu nampiga Catrine
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO    SEHEMU YA 12   Nilipoweka vocha  kisha nilienda chumbani kwangu,  nikachukua kadi ya General
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO  SEHEMU YA 12 Nilipoweka vocha  kisha nilienda chumbani kwangu,  nikachukua kadi ya General
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO    SEHEMU YA 13    Nilikurupuka na kuinuka nikaifunga suruali yangu na kukaa kisha General
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 13 Nilikurupuka na kuinuka nikaifunga suruali yangu na kukaa kisha General
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO   SEHEMU YA 02  Asikuambie mtu nilijisikia vibaya kweli kufokewa mbele
GENERAL SILI SILALI JUU YAKO SEHEMU YA 02 Asikuambie mtu nilijisikia vibaya kweli kufokewa mbele
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
You're not logged in


Tangazo - Ajnabi Mujhko Itna Bata - Pyaar To Hona Hi Tha
Ajnabi Mujhko Itna Bata - Pyaar To Hona Hi Tha
Ajnabi Mujhko Itna Bata - Pyaar To Hona Hi Tha
Enzi zetu
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest