VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 10
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Nikaanza kukaguwa lile brufcase, nikakuta kuna barua nyingi sana alikuwa ananiandikia mimi na nyingine anaandikia familia yake, na picha zangu nyingi kuanzia za utotoni, na namna anavyosaidia familia yake kwa siri sana, na mimi alishawah kumbe kumsaidia mama yangu…
Mama alikuwa na uzito kupitiliza, akaambiwa sijui amino acid imezidi mwilini, maana miguu ilikuwa inamuuma mpaka anashindwa kutembea, mwanzo hospital walituambia matibabu ni laki mbili na nusu, ila ghafla tu wakasema tumepata mdhamin hivyo tutatibiwa bure, tulitaman sana kumjua huyo mdhamini ila hatukuwah kufanikiwa kumfahamu hata mara moja…
Na hata nyumban kwao kumeanzishwa ujenzi na kuna uvumi ulikuwa unaenea kuwa, kuna mzungu alisikia tukio ambalo alifanyiwa kijana wao , ambao ndio muhimili wao hivyo alitoa kama msaada, wakati naondoka kulikuwa bado kuna jengwa na ilikuwa ni nyumba ya maana sana na kila wakati wazaz wake wakawa wana waombea dua sana huyo mdhamini bila kujua anaeyafanya hayo yote ni kijana wao mwenyewe…
Nikakuta barua moja ambayo ndio iliniumiza sana ilikuwa inasema “ zinura mamaa, kuanzia nimekuona nashindwa kabisa kuzuia hisia zangu, nakupenda sana na sio kweli kama mimi ni Malaya, najua huwezi kuamin ila nilivyolala na wewe ndio nimelala kwa mara ya kwanza na mwanamke, nimeshawah kukiss, na kuanzisha mahusiano, ila kabla hayajafika mbali naanza kuhisi kama nimekusaliti, nikawa nabadilisha wanawake nawashika shika tu, au najionesha kwa watu kuwa nina wanawake wengi ila ukweli ni kwamba sijawah kuwa na mwanamke yoyote Yule kwenye maisha yangu, kwa sababu niliamini, hisia zangu na moyo wangu mmiliki pekee ni wewe zinura wangu, nilikuwa nikimuomba sana Mungu nikutane na wewe, na nilikuwa nataman sana usije ukawa na mahusiano wala kuolewa maana nahisi nisingeona thamani yah ii dunia bila wewe mamaa, nipo hapa ila kuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea ambayo yananifanya nisiwe omari wako niwe nabil, kuna siku utakuja kunielewa, ila naomba usiwe na ukaribu na mwanaume mwingine yoyote mamaa, kwa sababu naumia mpaka nahisi kuchanganyikiwa, kwa sababu mwanaume pekee ambae natakiwa kukumiliki ni mimi, na sio faisali wala kidudu mtu yoyote Yule, nivumilie mamaa angu nivumilie kidogo tu, nitaenda na wewe mbali tukaanzishe maisha yetu kwa sababu nakupenda sana, ila naomba usiwe na ukaribu na wanaume, maana najiona nitashindwa kujifanya sikufahamu, maana wivu wangu kwako ni mkubwa sana kuliko hata akili zangu…
Ilikuwa ni barua ya kawaida, ila nilijikuta naanza kulia, nililia sana na kuamin kuna mambo anayahofia ndio sababu yupo vile alivyo, nikajiapia kuwa nitakuwa mtulivu ila angalau nimeshajua kuwa ni omari wangu, hivyo nitakaa kwa kutulia mpaka atakapo kuwa tayari kusema ukweli yeye pekee yake mbele yangu…
Basi nikarudisha kila kitu kwenye hali yake ya kawaida na baada ya hapo nikaendelea na shughuli zangu, na kama kawaida, nabil akawah sana kurudi nyumban, nikamtengea chai kwa sababu anapendaga sana chai ya tangawizi, nikampa, akaniangalia kisha akatabasamu na kusema “ asante zinura, nikampa na vikaranga , akaniangalia kisha akatabasamu tu…
Tabasamu lake lilikuwa kama nguzo yangu, name nikamuangalia, tukabaki tunaangaliana kwa sekunde kadhaa, mwisho mimi ndio nikajishtukia nikashusha macho chini kisha nikaenda zangu chumban kwangu…
Siku hio nilikuwa na amani sana, maana hatimae nilikuwa nina uhakika kuwa omari wangu yupo hai nab ado ananipenda, ingawa nilikuwa nataman sana kujua ilikuwaje mpaka akawa pale, ila nikaona haraka hazijawah kuwa na Baraka hata mara moja…
ITAENDELEA…
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
