VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 13
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Mama yake ni kama hakuwa anataka kumuelewa, ila nikamsikia baba yake anampooza mkewe, nikarudi zangu chumban kwangu nisije nikakutwa bure…
Nikajikuta naanza kuwa na hofu sana, kwanza nikafunga mlango vizuri sana siku hio, niliogopa nisije nikanyongewa ndani bure, au nikatupiwa masumu, nilikuwa naogopa mno, na siku hio sikutoka ndani kabisa, nikaamka mapema sana, nikafanya kazi zangu haraka haraka, mara mama akatoka, nikamsalimia hata hakuitika, nikajua ehee kasheshe imeanza, ila nilipomsalimia baba akatabasamu na kuniomba nimpikie chai…
Nikapika haraka haraka, kisha nikamtengea, wakati huo mama alikuwa ameondoka, na omari alikuwa bado chumban kwake..
“ mwanangu mzoee mama yako kuna muda anakuwa na matatizo yake binafsi tu, akasema baba huku akiwa anatabasamu..
“ hamna shida baba, nikajibu kwa sauti ya unyenyekevu wa hali ya juu..
“ najua wewe na nabil mnapendana sana, na nabil yupo tayar kufanya jambo lolote lile kwa ajili yako, hivyo nimeamini anakupenda kwa kiasi kikubwa sana na mimi kama baba natamani sana kuendeleza huu upendo wa mwanangu maana furaha yake ndio furaha ya mke wangu na furaha ya mke wangu ndio furaha yangu, akaendelea kusema…
“ ila sasa najua mnajuana kuanzia siku nyingi sana, na huenda ukawa unamjua zaidi ya sisi tunavyomjua, ila nakuomba sana, usiseme jambo lolote lile kuhusu maisha yake ya nyuma kwa mtu yoyote Yule kwa sababu nitakufatilia, kama unataka kuwa salama, na kama kuna mtu anatakiwa kutoa kauli ya mwisho kuhusu familia yangu, kwa maana ya mwanangu pamoja mke wangu basi atakuwa ni mimi tu, akaendelea kusema Yule baba na mimi nikakubali..
“ na mwisho kabisa, hauruhusiwi kutoka kwenda sehemu yoyote ile, na hauruhusiwi kukutana na mtu yoyote Yule mpaka tutakapo kuruhusu, natumai tumeelewana vizuri, akaendelea kusema Yule baba, alikuwa anaongea kwa sauti ya upole yenye msiskitizo wa hali ya juu,na nikaitikia kuwa nimemuelewa, akatabasamu kisha akasema “ asante kwa chai binti yangu…
Siku hio nabil hakutoka kabisa chumban kwake, na mimi sikuwa najua anakula nini au anaishi vipi, na nilikuwa naogopa pia kumfata, kwa sababu ile ni nyumba ya watu na jambo lolote lile litakalo tokea huenda wenyewe wameshaweka mitego yao, hivyo sikutaka matatizo na mtu yoyote Yule…
Basi muda ukaenda na kwenye majira ya kama saa kumi jioni, mama yake nabil alikuja, alikuwa pamoja na mwanamke mrembo sana, akanambia nimuandalie sharubat, sikubisha nikaandaa haraka haraka kisha nikampelekea yeye pamoja na mgeni wake…
Basi baada ya kuwatengea Yule mama akaniangalia kwa tabasamu, alikuwa kawaida kama anavyokuwa kila siku, na hakuwa na kisiran kama nilichomuona nacho asubuh..
“ shenaizah huyu ni mfanya kazi wetu wa ndani nan i mchapa kazi sana, yaan ukiwa na shida yoyote ile utamuambia na atakufanyia vizuri, kwa sababu ana adabu sana, nan i mtiifu kupita maelezo, akasema Yule mama na Yule binti akaniangalia kama nyanya iliyooza, ila sikujali maana hanihusu na dharau zake..
“ zinura.. huyu anaitwa shenaizah ni mkwe wangu na mke mtarajiwa wa wa mwanangu kipenzi nabil..
Alikuwa anaongea kistaarabu kama ananibembeleza hivi, ila yale maneno yaliingia moyoni mwangu, nikasikia kama moyo unachanwa chanwa na viwembe kwa maumivu ambayo nilikuwa nayasikia, sikujua kama natakiwa kupiga kelele kwa nguvu na kulia, au kutulia tu na kujifanya kama sijasikia kitu…
ITAENDELEA …
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
