VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 12
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Basi bana shughuli ikaendelea na alipo maliza akanigeukia na kusema “ nakupenda sana zinura, hakika wewe ndio nuru ya maisha na roho yangu, nakuomba sana uwe mvumilivu na usimuambie yoyote ulichokigundua kisha akaondoka zake…
Nilijisikia vziuri sana na kuiona ile hadithi yangu ya mapenzi ambayo nimeianzisha kuwa inaelekea kwenye nafasi nzuri sana, sikuwah kufikiria hata mara moja kama lile penzi langu lililoanzia kwenye utoto wangu kuwa nitakuwa nalo na litatimia siku moja…
Nilikuwa nahisi naota ndoto ambayo sikuwa nataman hata kuamka kwa kweli, nilikuwa nataman kuendelea kuishi kwenye ndoto hio siku zote za maisha yangu…
Basi omari au nabil hakuwa anakaa karibu na mimi mbele ya wazaz wake wa mchongo, ila wakiondoka alikuwa anakaa karibu na mimi, na alikuwa ananitreat kama mwanamke wake, zile tabia zake ambazo nazijua nikaziona kabisa pale…
Hakuwa anataka niteseke, ni mara nyingi tu naamka asubuh nakuta amefanya kazi na kuniandalia chai kabla hajaenda kazini, yaan nilikuwa ni mfanyakazi wa ndani wa kawaida, ila nilikuwa naishi maisha mazuri sana ambayo ndio ndoto ya wanawake wengi…
Hakuwa anataka tuchart wala kuongea na simu, ila alikuwa anarudi nyumban tunaongelea kila kitu nyumban, na penzi letu likarudi, ila kila nikimuuliza imekuwaje mpaka ameishia kuwa mtoto wa hawa watu hakuwah kunipa jibu la moja kwa moja zaidi ya ni mipango ya Mungu tu..
Basi maisha yakaendelea na kama mnavyojua hisia huwa hazijifichi, hata wazaz wake na baadhi ya ndugu zake wakajua mimi na nabil tunapendana sana, wazaz wake walifurahi sana, mpaka nikahisi amani, ila baada ya watu kujua nikaona nabil au omar anakosa kabisa amani, yaan hakuwa na raha kabisa akawa ni mtu wa mawazo na wakati nilidhani ni jambo la kheri sana kwa wazaz wake kujua na walikuwa wanataman sana kumuona kijana wao anatulia, na walikuwa wanataka pia kuwa na mjukuu na kizazi cha uhakika, kwa sababu nabil alikuwa pekee yake…
Siku moja nimelala zangu, nikataka kwenda kuchukua maji jikoni wakati natoka, nikasikia kama chumban kwa nabil kuna mtu anaongea nae, sasa kwa wivu wangu wa mapenzi nikasogea mpaka mlangoni na kusikiliza wanaongea nini, ndio nikamsikia mama yake anasema “ kumbe umesharudisha kumbukumbu unatuficha tu, huyu binti hatakiwi kuishi tena hapa na anatakiwa aende mbali sana, hatakiwi kusema kuwa wewe sio mtoto wetu, maana pekee yake ndio anajua kuwa wewe umetoka wapi, maana ukoo wangu wote unajua kuwa wewe ni mwanangu, sitaki tena kumuona nyumban kwangu, akawa anasema mama yake nabil…
Omary alikuwa analia huku akisema “ mama najua unanipenda sana na unataman siku zote niishi na wewe, nakuahidi nitaishi na wewe, ila naomba usimfanye chochote kile zinura wangu, kwa sababu kwanza nampenda sana, na kama unanipenda kama mwanao naomba sana uniache niwe na zinura maana ndio mwanamke pekee ambae ninaweza kumuoa, kwa sababu, akili, hisia na kila kitu changu kiko kwake…
“ nimesema wewe ni mwanangu, ndio nataka uoe ila sitaki umuoe huyu binti, mtaenda kwenu na kuwaonesha wazaz wako kuwa mimi sio mama yako, mimi sio mgumba, mimi nina mtoto na mtoto wangu ni wewe, akawa anaendelea kulalamika Yule mama na mume wake akawa anampooza tu, kuwa awe mpole, na hilo swala sio kubwa atalimaliza tu, sasa kwenye kulimaliza ndio nabil akaanza kulia na kusema “ naomba msimuuwe zinura wangu please baba nakuomba sana, nipo tayar kuacha kila kitu ili niwe na zinura tu..
ITAENDELEA …
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
