VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 14
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Nikalazimisha tabasamu kwenye uso wangu, ila ukweli ni kwamba tabasamu lilikuwa linatoka ila maumivu ambayo nilikuwa nayasikia moyoni hayakuwa yanaelezeka kabisa, nilikuwa nasikia maumivu makali sana, ambayo hata nikiambiwa nisimulie namna ninavyojisikia sikuwa najua nitasema je…
Basi sikutaka kuendelea kukaa pale, kwa sababu nilikuwa nahisi kupasuka kwa kweli kwa wivu..
Nikaenda chumban kwangu, nikalia sana, yaan sikujua Mungu alikuwa na kusudi gani na mimi, mpaka anipitishe kwenye haya maisha ambayo alikuwa ananipitisha kwa kweli, sikuwa najua kama mapenzi ndio yanauma kwa kiasi hichi..
Mara nikasikia nabil anaitwa ndio akatoka chumban kwake, ila kabla hajaenda huko alipoitiwa akafungua mlango wangu na kunituta nalia, akanisogelea kisha akanifuta machozi na kunambia “ nakupenda sana dhinura wangu na kwenye hili sitanii, naomba niamini kwa jambo lolote lile ambalo utaliona amini wewe pekee yako ndio mwenye haki ya kuwa na mimi…
Hapo angalau sasa nikaanza kupata amani, yaan familia hainitaki ila mwanaume bado yupo na mimi, nikainua macho yangu na kumtazama, akaniangalia kisha akatabasamu na kusema “ mamaa nakupenda sana, kisha akanikiss na kusema “ naomba nikamsikilize mama, kisha akaondoka zake….
Nilikuwa chumban kwangu kimya nimetulia, nikiwa sijui natakiwa kufanya nini, kwa sababu nilikuwa nina uhakika kuwa siwezi kurudi kwetu na kuendelea kukaa pale ni hatar zaidi kwangu…
Mara nikaanza kusikia nabil akiwa ana bishana na mama yake, nikafungua mlango kidogo na kuanza kuwasikiliza..
“ nimesema kama ni kuoa utamuoa shenaizah na sio huyo mwanamke unayemuwaza, kwa sababu hatutakaa tumpokee kwenye hii familia, akasema mama yake..
“ siwez kuoa mwanamke ambae simpendi mama, nimekuwa na kuheshimu na kulinda sana heshima yako kwa muda mrefu sana, na sijawah kukupinga kwa sababu nimekuwa nikikuweka wewe mbele zaidi kwenye maisha yangu kuliko kitu chochote kile, ila kwa hili hapana, naomba uache moyo wangu na hisia zangu zichague zenyewe kuwa zinamtaka nani, kwa sababu nitakuja kumtesa binti wa watu kwa sababu simpendi hata kidogo shenaizah mama na nampenda zinura, akasema nabil kwa sauti ya kujiamin, mpaka kuna namna nikaanza kupata ka amani, kwa sababu angalau mwanaume ambae nampenda alikuwa ananitetea…
Yule mama sijui hata alikuwa na matatizo gani, akaanza kutetemeka kisha akaanguka chini, sijui nabil akamfanya nini akaamka, baada ya hapo nabil akamkumbatia mama yake wa kufikia na kusema “ sawa nitamuoa mama ila nimuoe na zinura ili angalau nitulize moyo wangu na wako mama…
Hapana mwanangu Yule mfanya kazi wa ndani mimi simtaki kwenye familia yangu hata kidogo, sipo tayar kukupoteza kwa gharama zozote zile mwanangu, kwa sababu wewe ni mwanangu na siku zote za maisha yangu utakuwa mwanangu na hautakaa uwe mbali na mimi, akaendelea kusema…
Nabil akaanza kulia, alikuwa ni kama mtu asiekuwa na namna, kwa sababu alikuwa anaonekana wazi kuwa hayupo tayari na chaguo la mama yake, na pia hakuwa anajua atafanya je ili asiniumize mimi kama mwanamke wake na mwanamke wa maisha yake…
Yaan nilikuwa namuangalia namna anavyotoa machozi nikajua kabisa huyu hana namna ila ukweli ni kwamba hampendi hata kidogo huyo mwanamke, ila hayupo tayar pia kumkwaza mama yake, nikaanza kupata hofu kwa sababu niliamin kuwa chaguo la mama yake ndio linaweza kupita kuliko chaguo la moyo wake…
ITAENDELEA …
SHUKRANI – Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
