VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 9
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Nikiwa nimekaa pale mara nabil akapita, aiseee alinikata jicho kana kwamba anaugulia maumivu ya kupigwa teke la chini huko, nikajifanya kama sijamuona, kwa sababu sitaki shida mimi, kisha akawasha gari lake na kuondoka…
Amekuja kurudi saa mbili kasoro, wanafamilia wote tulikuwa tayar tumeshafika mezan tunajiandaa na chakula, kwa sababu ile nyumba yaan saa mbili kamili wanaanza kula, nashangaa nabil anaingia akiwa amelewa mno..
Wazaz wake walishangaa, inaonekana hajawah kuonekana amelewa hata mara moja kuanzia amefika pale, mama yake akamfata na kumuuliza shida nini akasema “ wewe ni nani? Mimi mbona sikujui, hapo anaongea kwa ile sauti ya pombe, mara akaanza kusema “ yaan namkumbuka sana mwanamke wangu wa kijijini, kabla hajamaliza baba yake akasimama haraka haraka na kusaidiana na mama yake wakampeleka mpaka chumbani…
Sote tuliokuwa pale tulishangaa sana, kwa sababu hakuna mtu anajua kama nabil alishawah kuishi kijijini, basi tukaendelea na kula na nilipomaliza kula nikasema nitoke njee angalau nipunge upepo…
Wakati huo nabil amelala na Feisal hakutoka chumban kwake toka tumefika pale…
Mara nikasikia mama yake nabil anasema “ nahisi ameshaanza kurudisha kumbukumbu zake, unadhan mume wangu ataendelea kunichukulia kama mama yake? Nataman anione mama yake katika maisha yangu yote..
Nilishtuka sana niliposikia hayo maongezi, nikajua lazima ni maongezi ya siri sana, nikarudi chumban kwangu upesi na kulala, na kesho yake wakasema vocation imeisha na kila mtu anarudi anapoishi, faisal alinifata akanambia “ ukiweza kunichagua kati yangu na bro, nitakuoa zinura ila ukiona bro ni bora zaidi kuliko mimi, nakuombea kwa Mwenyezi Mungu maisha yenu yawe na furaha na amani siku zote za uhai wenu…
Maneno yake kuna namna yaliniingia, nikaona ni mtu mwenye busara sana, nikataka kwenda kupanda gari la baba na mama, ila nabil alinikata jicho kisha kwa sauti ya ukali akasema “ njoo huku…
Kwa kuwa kulikuwa na watu wengine maeneo yale sikutaka kutengeneza hali ya taharuki nikamfata mpaka kwenye gari, na gari lake ndio lilikuwa la kwanza kuondoka eneo lile kabla ya magari yote…
Basi tukaenda kule nyumban ambapo tulikuwa tunaishi mwanzo, na siku hio ikapita, kesho yake ilikuwa siku ya kazi nhivyo familia nzima iliondoka na kuniacha pakee yangu kama kawaida, pamoja na mlinzi…
Basi kama kawaida, nikafanya usafi, ila nafsi ikanambia niende chumba cha nabil huenda kuna vitu nitaona, kweli nikaangalia sana ila sikuona kitu chochote, nikachungulia chini ya kitanda, kitanda nacho kilikuwa ni cheupe sana, hakina kitu chochote uvunguni, ila ile nainua uso, nikakutana na brufacase ambalo lilikuwa chini ya godoro, nikanyanyua godoro, na kuliangalia, nikataman kujua lilikuwa na nini, kwa sababu linaonekana lina vitu vya siri sana, ila lilikuwa na password, kila nikiingiza password ikawa inakataa, ila nikapata wazo, kama kweli atakuwa ni omari na kwa namna ambavyo alikuwa ananipenda lazima ataweka kitu kinachohusiana na mimi, nikaja kuweka mwaka wangu wa kuzaliwa, nashangaa linafunguka, na juu kabisa kulikuwa na picha yangu pamoja nay eye kwenye siku ya mahafali pale shuleni, kabla ya liletukio la kutisha kutokea….
Nilishtuka sana, na nikajithibitishia kuwa alikuwa ni omari kweli, nikataman kujua imekuwaje mpaka amefika je kwenye ile nyumba na imekuwaje mpaka wale wazee wawili waseme kuwa ni mtoto wao na wanaonekana kumpenda kuliko kawaida…
ITAENDELEA …..
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
