VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 17
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Baada ya kumaliza kufunga ndoa akaniita kisha akasema “ naomba niongee hili mbele ya kila mmoja , akanishika mkono kisha akaanza kusema ..
Najua leo ni siku adhimu na nisiku kubwa sana, najua mtashangaa ila nimefunga ndoa na wanawake wawili, maana dini yenyewe inasema kuwa, “ tuanze na wawili, na naamin nimelifanikisha hilo, na wazaz wangu naomba mlipitishe hilo na mnipe Baraka zenu…
Baba yake akanisogelea na kunambia “ hongera sana binti yangu, hakika mwanangu ni mwanaume bora sana, na anapambana kuipambania furaha yake, na nimeona ukomavu wa nguvu na akili yake, mungu awape maisha yenye furaha na amani, nikajikuta natabasamu…..
Kisha akamfata shenaiza sijui alimuambia nini, ila akanuna huyo, alafu Yule baba akatabasamu zake na kwenda kukaa..
Maneno yalianza ila hata nabil hakujali, akaagizwa watu wanichukue wakanipambe kwa sababu ilikuwa sherehe yangu pia, na kweli mimi ni chombo bana ila sikuwa na matunzo tu…
Basi tukaanza kusherehekea, hapo nabil yupo kati kati na upande mmoja nipo mimi, na upande mwingine yupo shenaiza, ila muda mwingi alikuwa upande wangu ndio nilikuwa naongea na kupiga nae story sana…
Mama yake alikuwa anatuangalia kwa jicho baya, ila nabil ni kama alishaamua kujilipua, wazaz wa shenaiza hawakupendezwa kabisa na kitendo cha nabil na kutaka kuondoka nna binti yao, ila shanaiza akalazimisha kuendelea kukaa pale, sijui ndio alijua anaweza kumshawishi nabil au vipi..
Baada ya watu kutawanyika nabil akamgeukia shenaiza na kusema “ najua unataman sana kuingia kwenye hii nyumba na umekuwa una pambana kwa muda mrefu sana, ila jua kwanza mimi sina mali, na mali zote zina majina yam zee hivyo hautakuwa na cha kurithi, na cha pili kwa kuwa ulikuwa unataka kuwa chaguo la wazaz wangu basi sitakaa nikuguse hakikisha aliekuleta ndio anatekeleza mahitaji yako ya kimwili, kisha akanishika mkono na tukaanza kutoka nje, nikajua hapa sasa napelekwa kwenye fungate, na ndio ilikuwa hivyo…
Yaan hapo ndio niliamin hakikisha mwanaume anaekuoa anakupenda sana kuliko ambavyo wewe unampenda, nikaamin pia furaha ya kweli ya maisha yetu ni kuwa na watu tunaowapenda na wanaotupenda bila unafiki…
Basi tukaenda zetu kula fungate hapo nabil a.k.a omari alikuwa amezima simu, akimaanisha hakuwa anataka kabisa mtu aje amuharibie furaha yake…
Baada ya siku saba tukarudi nyumban, tukamkuta mama yake amekaa ukumbini kana kwamba alikuwa anatusubiri kwa hamu na alipotuona tu akatabasamu ila tabasamu la maumivu, kisha akaniangalia na kusema “ kumbuka na wewe ni mwanamke unataka kimchukua mwanangu, ambae nimahangaika sana kumpata, utakuja na wewe kuchukuliwa mwanao kama unavyonifanyia…
Kwa namna ambavyo huyu mama alikuwa anaongea, alikuwa anaongea kama ana ugonjwa flani hivi wa akili, kwa sababu alikuwa analalamika kama mtoto mdogo vile, baba yake nabil, akaja na baada ya kuja akamchukua na kumpeleka chumban, na baada ya kama lisaa limoja akatoka nae, na kunifata huku akisema “ kwa hio hautamrudisha mwanangu kwao, kwa hio mimi ndio nitakaa nae siku zote, akaendelea kusema Yule mama, nikamuangalia na nabil akatoa ishara kuwa nikubaliane nae, nikakubali, akacheka kisha akasema “ ukimchukua nakuuwa…
“ ukimuuwa na mimi najiua, akasema nabil na alikuwa anaonekana anajua udhaifu wa mama yake ni yeye, Yule mama akaanza kulia, kisha akawa anasem “ basi mwanagu simuuwi tena, usije ukaniacha…
Mume wake akamchukua na kwenda nae chumban kisha baada ya muda akatoka pekee yake na kuanzia tunafika hatukumuona shenaiza sijui ndio alirudi kwao au ilikuwaje..
Ila alivyotoka, akatuangalia kisha akasema “ naona sasa wakati umefika wa kuujua ukweli wote..
ITAENDELEA ….
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
