ILIPOISHIA...,
Akaachia mshonyo mkali, huku akiongea kwa sauti ya chini chini, akisema,
" mmh!, yani hata ukisikia nimechanganyikiwa ndo nikufanyie wema mtu kama wewe?!,
utasubiri Sana kwa hilo, sasa subiri furaha yako yaja, mimi ndo mama Vero wa ukwee e! ".
Turi alisikia maneno hayo vizuri tu,
Lakini, hakuelewa ni nini mama yake alikuwa anakimaanisha!, maana ametoka kuongea naye kwa upole na bashasha muda si mrefu!,
ila,
Turi akaamua kujipa imani, huku akajisemea kimoyo moyo,
"labda itakuwa ni watu wake wa kwenye Vikoba wamesha mkera tayari, maana mama naye, mmh...!,mmh...!, mmh...!".
Lakini, Turi alipotoka nje, alimkuta mama yake pamoja na mdogo wake ambaye ni Vero, wakiwa wamesimama na Kijana mmoja ambaye kimuonekano ni chizi kabisa!,
maana, alikuwa amevalia mavazi ya kuchakaa na machafu kuriko kawaida!, huku nzi wakimzunguka kama mkaanga samaki wabichi!, tena akiwa anaongea peke yake na kucheka.
Turi alipofika karibu, akamuuliza mama yake akisema,
"Masikiniii!, mama!, huyu mgonjwa katokea wapi mama!?, au inawezekana anajisikia njaa!, nikamletee chakula? ".
Loooh!, lakini, jibu alilolitoa mama Vero lilimfanya Turi akajuta kuzaliwa kabisa, na kujiona kama mtu mwenye makosa makubwa kwa kuzaliwa kwake kwenye hii dunia!,
maana, hakuna siku imewahi kupita hivi hivi, tangu alipokaa na mama huyo bila kumwaga machozi ya hudhuni!,
maana, Mama yake huyo, huku akiwa anaongea kwa kejeri na kumkata jicho Turi kuanzia miguuni mwake mpaka utosini, Akasema, "
ahahaha!, haloooh!, na bado mwaka huu, eti!, huyu mgonjwa katokea wapi?, yani mumeo unamwita mgonjwa,
utaachika uwe na adabu!,
sasa huyu ndo mumewako wewe kinyago!, utake na usitake utaolewa naye".
Turi, akawa kama mtu aliyechanganyikiwa kutokana na matatizo yasiyoisha kwenye maisha yake, akaanza kulia kilio chenye sauti ya juu kabisa!, huku makamasi yakimtoka puani kama Mtoto mdogo,
kutokana na hudhuni ambayo, ilimfanya mpaka akakumbuka wazazi wake,
labda wangekuwepo hayo yote yasingemkuta akasema,
" mamaaa!, nimekukosea nini lakini kwenye maisha haya mimi,
mbona najitahidi Sana kufanya kila kitu unachonielekeza kwa wakati na utiifu mkubwa, na wala sijawahi kukuchukulia kama Mama wakufikia hata siku moja ,
bali nakuona kama Mama yangu mzazi,na wala hakuna siku nimewahi kukuvujia heshima mama!,
lakini, sitaki kuamini kuwa haya ndio malipo yake, mimi nitaishije na kijana huyu,na unaona hali Yake ilivyo?!,
Bora ungenitafutia hata kazi, ningejua nitaishi naye vipi,
ila!,
nashukuru kwa yote Mama ".
Baada ya maneno hayo ya Turi ambayo yalijawa na hudhuni na ukweli mtupu!, Lakini, hayakubadirisha chochote kwenye roho mbaya aliyokuwa nayo Mama Vero, ndo kwaanzaa!,
akamshindilia na maneno mengine ya ziada ya kero akasema,
" ebu nitokee hapa mimi we takataka, unajiliza liza hapa,eti!, mama...!, mama!, mama!, nilikuzaa Mimi wewe?!".
Maneno hayo, yalimfanya mpaka kijana huyo anayesemekana kuwa ni chizi, macho yake Yakajawa na machozi ya hudhuni,
lakini hakuna aliyemfuatilia wala kugundua ,maana wote walikua bize na majibizano tu!.
Ghafla!, Mama Vero akaingia ndani na kuchukua mfuko mweusi wa rambo ambao,
ulikuwa na nguo mbili tatu za Turi kisha akamtupia Turi miguuni, na kusema,
"chukua na maforonya yako haya wewe!, usiache nuksi zako humu ndani, umuachie mwanangu Mimi!,
unadhani na yeye amekosa radhi za wazazi wake kama wewe eeeh!?".
ila, chaajabu!, baada ya malumbano hayo ya muda mrefu, kijana huyo chizi alikuwa mpole kabisa,
tofauti na vile ambayo mama Vero alivyomzoea kumuona mtaani akiwa na fujo za hapa na pale za uchizi wake,
lakini alipoa kabisa!, mpaka mama Vero akajisemea kimya kimya,
" huyu kichaa naye sijui anakahuruma?!, mbona amepoa hivi na si kawaida yake?, bwana eeh! ,
wataenda kujuana wenyewe , na jumba lake bovu lile, sijui wataishije, hahahaha,ilimradi mpango wangu wa kumuondoa Turi kwenye urithi umetiki, siwazi!".
Haikupita muda mrefu, mara!, kijana huyo chizi huku akijichekesha chekesha, akamshika Turi mkono akaondoka naye huku akiwaaga Vero na Mama yake,
Turi alijaribu kujinasua kutoka katika mikono ya kijana huyo, ili angalau atembee mwenyewe , maana alikuwa anatoa harufu isiyo ya kawaida kabisa!.
Mama Vero hakuisha kuongea hata Baada ya Turi kutoka pembeni kidogo ya nyumba ,akamsindikiza na maneno ya mwisho mwisho akisema,
" nenda mwana kwenda, Yani watu hatufanyi mambo yetu kwa uhuru kisa kukufikiria wewe, we kama nani!?".
Lakini, kijana huyo chizi alimshika Turi kwa nguvu hadi Turi akawa na wasiwasi moyoni, huku akijiuliza maswali juu ya usalama wake huko aendako,ila, hakujua lipi ni jibu sahihi!,
ila, chakushangaza!, walipofika mbele kijana huyo ambaye mwanzo walikotoka alikuwa anajichekesha kama chizi, ghafla!, akawa siriasi!,
akamwambia Turi maneno lilofanya akabaki mdomo wazi kwa mshangao, kijana huyo chizi alisema,
" Turi!, usilie Mimi Sio chizi, kila kitu kitakuwa Sawa tu tofauti na alivyotarajia mama yako.!,
ITAENDELEA....
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments