Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

🎙️ WALIMWOZESHA NA CHIZI KUMBE NI TAJIRI!(Part 4)

27th Aug, 2025 Views 31



ILIPOISHIA...,

Amani, Turi pamoja na mshenga, wakakaa kwenye viti vilivyoletwa na Vero.
Na Baada ya kukaa ,mshenga akasema,
" mama, Sisi hatuna muda Sana hapa, ila tumekuja kuleta kidogo ambacho kijana wetu amebarikiwa nacho, nadhani yeye mwenyewe atasema mengi".

Kisha mshenga akatoa bahasha iliyotuna kweli kweli!, na kumkabidhi mama Vero, kisha mshenga akamalizia kwa kusema,
" hii ni kama shukrani ya muoaji kwako, kwa malezi na kumkuza binti yako mpaka alipofika".

Mama Vero karibia kidogo aanguke chini!,
kutokana na bashasha na hamu ya kutaka kujua kilichokuwa ndani ya bahasha hiyo, huku akitetemeka mikono ,akapokea bahasha na kuifungua,

ghafla!,
Mama Vero akaanza kujiropokea maneno yasiyokuwa na mbele wala nyuma kutokana na furaha, baada ya kukutana na vitita vya misimbazi vilivyo viringishwa kwa raba bendi(rubber band) akasema,
" Yani heshima ya mwanangu Turi imeniheshimisha leo!,
shida Vero ni mtukutu kuriko dada yake, mmh! mmh! mmh!,

Kwahiyo!, Amani Baba!, umeponea hospitali au kwa mganga!?, mmh! mmh!, maana daah nililia mimi kwa kukuonea huruma ,nikasema Loooh!,
ivi kijana wangu atapona kweli huyu, ila mshenga hana baya naye yaaaani we acha tu!".

Kwa kifupi, Mama Vero alikuwa kama kavurugwa akili, hata mwanaye Vero alishangaa akajisemea kimya kimya ,

" Mmmh! , Mama kwa kupenda hela, sasa mbona maneno anayo yasema simuelewi kabisa mmmh!, wala hajiulizi watu wanamchukuliaje!".

Amani naye, akatoa kauli yake juu ya ujio wao, akasema,
" Mama!, hiyo ni mahali ya kumuoa binti yako Vero, nimejivuta vuta nimepata milioni tano, ingawa Sio nyingi, ila naamini itawasaidia kwa vitu vidogo vidogo kwa kipindi hiki.

Na kuhusu swala la uchizi, kiukweli mimi sikuwa chizi hata kidogo, bali nilitaka tu Kutafuta mwanamke mwenye mapenzi ya kweli,
na mwenye nidhamu bila kujali mtu aliyekutana naye yupoje, na kutoka moyoni nasema hapa mbele yako, Turi ndiye mwanamke sahihi".

Ghafla!, mama Vero akapiga magoti huku akimwaga machozi na kuomba msamaha, akasema,
" mwanangu Turi!, nisamehe Sana mwanangu,
hakuna mkamilifu, nakushukuru Sana mwanangu bila wewe leo nisingefurahi hivi mimi".

Turi akamjibu Mama yake kwamba,
"usijali mama , mimi nimeshakusamehe mbona!, usiwe na wasiwasi wowote ,mkubwa hakosei".

Baada ya maongezi hayo kuisha, Amani, Turi na mshenga wakaingia kwenye Gari Lao kisha wakaondoka.

Mara tu baada ya gari kuondoka, .mama Vero akasonya huku akibinua mdomo na kukunja ndita , akasema,
" Mwanangu Vero, usijali, usiwe na hudhuni yoyote mwanangu, siwezi kukubari kuona Turi anaolewa na tajiri kiasi kile ,halafu wewe ubaki nyumbani!, tena kosa walilolifanya ni kunipa hela ambayo, itanisaidia kwenda kwa mtaalam ahaha ahahah!!,
mimi ndo mama Vero wa ukwee' eeh!, haya futa machozi mwanangu kipenzi.

Mimi dunia hii nina mtoto mmoja tu!, ambaye ni wewe, hao mayatima mimi siwajui fwiiiiiiiii!!".

ITAENDELEA...,

JE wajua kwamba unaweza kukamata sms za mwenza wako anazochart na watu wake na ukazipata kupitia simu yako bila yeye kujua??

Kwa huduma ya sms tracking jiunge na group letu whatsapp
https://chat.whatsapp.com/KpHkiAUYVKQIYYgbgsl8HT?mode=ems_copy_c

Au ncheki whatsapp 0710204647 nkuunge na group

#storytelling #fyp #simulizinasauti #story.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

🎙️ WALIMWOZESHA NA CHIZI KUMBE NI TAJIRI!(Part 4)  >>> https://gonga94.com/semajambo/walimwozesha-na-chizi-kumbe-ni-tajiri-part-4

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest