ILIPOISHIA...,
nimekuwa nikikuchunguza muda mrefu Sana toka nilipotoka mjini, maana niliwaambia familia yangu wanitafutie mke mwenye utu, heshima na upendo, wakanitajia wewe,
na nimefanya hivi makusudi tu ili nipime yaliyosemwa,
Lakini, nimegundua,wewe ni mtu wa pekee sana katika hii dunia ya leo,
kwahiyo, hapa tunaelekea mjiniii, toa hofu kabisa ".
Maneno hayo, yalimfanya Turi akapata nguvu mpya, ingawa hakujua hali harisi ya maisha ya kijana huyo,
ila, kujitambua tu kwa Kijana huyo ilikuwa tosha kwa Turi,
maana, swali alilokuwa akijiuliza sana Turi ni kwamba angeishije na Kijana huyo, ambaye Kila mtu kijijini anamjua kama ni chizi!.
Waliongozana mpaka nyumbani kwa Kijana huyo ili kufanya maandalizi ya ndoa ili waelekee mjini,ambako Kijana anaishi .
watu wengi mtaani walishangaa sana kumuona Kijana huyo ambaye alikuwa chizi, akiwa ameongozana na Binti Turi, tena akiwa anaongea kama mtu mwenye akiri timamu kuriko kawaida!,
Kijana huyo akawmambia Turi kwamba, " waache wanishangae hivyo hivyo, ili wapate somo kwenye maisha la kitomdharau Kila mtu, tena nitazidi kuwashangaza!, aah! ,Turi!, nilitaka kusahau,Mimi ninaitwa Amani".
Turi naye akamjibu Amani akisema,
" ooh!, na mimi ninaitwa Turi ".
Amani akamalizia kwa kusema," ninakufahamu mrembo wangu, nimekuchunguza muda mrefu sana bila wewe mwenyewe kujijua ,
ila,
ninachokusifu!, hukuwahi kubadili mwenendo na tabia Yako,
jambo ambalo watu wengi huwashinda haswa wanapokutana na watu ambao Kila wanapojitahidi kuwafanyia mema,
wao wakawalipa mabaya,
wengi hulipiza ubaya pia, ila wewe umekuwa na heshima mpaka siku unaondoka!".
Baada ya siku kupita, utaratibu wa sherehe kubwa ya harusi ulifanyika na watu wengi kijijini waliarikwa katika sherehe hiyo!.
Mama Vero alipewa taarifa na mmoja wa majirani juu ya utimamu wa Amani,
lakini hakukubari juu ya taarifa hiyo,
" mama Vero, nina ubuyu shoga yangu!, yani!,
juzi nimekutana na Amani yule chizi wa Kijiji ,akiwa anaendesha gari nzuriii!!, akiwa na Binti yako Turi sijaaminiii!!".
Mama Vero akajibu kwa kejeri na kufoka kama kawaida yake,
" mmh!, yani inawezekana hata wewe mwenyewe ni kichaa, huna akili sawa sawa,
maana, hizo taarifa unazonipa haziwezekani!,
ebu toka toka nyumbani kwangu mchawi mkubwa wewe!".
Kisha, mama Vero akamvuta jirani yake huyo kwa maneno makali akimtaka aondoke nyumbani kwake!.
Lakini! , siku iliyofuata asubuhi na mapema, Mama Vero alisikia honi ya gari ikipoga nje ya nyumba yake, akatoka upesi ili kuangalia,
maana tangu azaliwe hajawahi kupigiwa honi ya gari,
tena nje ya nyumba yake, labda zile za barabarani zinazomtaka apishe ili gari ipite tu!.
Toubaaa weeeh!, alipotoka nje Mama Vero alishikwa na butwaa ,akawa kama mtu aliyegandishwa kwa dakika moja mzima,
huku akikodoa mimacho yake kama mjusi aliyebanwa na mlango!.
Baada ya kumuona Amani akishuka kwenye gari nzuri mno kuwahi kuonekana kijijini, huku akimshika mkono Turi wakiwa na mshenga wao!.
Mama Vero akaanza kumfokea mwanaye Vero akisema,
" we veroo!,
inamaana wageni huwaoni au, mtoto unadharau wewe, ebu leta viti ,mwanangu kipenzi Turi kaja huyoooo!" .
Turi akabaki kushangaa tu ,maana mama huyo alikuwa na unafiki wa wazi wazi kabisa,
hadi mshenga akajisemea kimoyo moyo,
" mmh!, hapa kweli kazi ipo,loooh!, yani halina haya hata kidogo...!
ITAENDELEA...,
.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments