ILIPOISHIA...,
Lakini hata hiyo, Vero alikua msichana mwenye moyo wa huruma kidogo ukilinganisha na mama yake ambaye alizidi ugaidi!,
Vero akawmambia mama yake kwamba,
"ila mama!, unaonaje tukiachana tu na dada Turi, maana , sasahivi tumepata pesa, tukaanza hata biashara ya mama nitilie,
kuriko kumfuatilia mtu ambaye Kila kukicha mungu anambariki yeye tu!?".
ila maneno hayo yaliyojawa na busara na ukomavu wa fikra kutoka kwa Vero, yalionekana kama takataka tu mbele ya Mama Vero!,
maana alimshushia Vero maneno yasiyo ya kawaida kana kwamba hakumzaa yeye mwenyewe! ,
" na wewe mwendawazimu mkubwa nisikilize kwa makini ,
sijui umetoroka uchawini wewe, eti dada dada dada...!, unamjua wewe yule Binti!?, yani mimi nataka nikupambanie unaniletea ujuaji hapa!,".
Vero akamjibu Mama yake kwa uwoga Mkubwa,
" basi mama nisamehe bure, sirudii tena".
Asubuhi ya siku iliyofuata, Mama Vero hakutaka kulaza damu!, akaamua kufuatana na mwanaye Vero na kuelekea kwa mganga.
Na baada ya kuwasili kwa mganga, walikaribishwa na kuingia hadi ndani, mganga akamuuliza mama Vero kwamba,
"tawile tawile tawileee...!, karibu mama, eleza shida yako iliyokuleta , hapa ndio kwa mganga tekero, lolote linawezekana, ahahahaaaahaa!".
Mama Vero akamjibu mganga huyo akisema,
" Ahsante Babu!, mimi shida yangu naomba yule Binti Turi asiolewe na yule mume anayetaka kumuoa,
Bali, mwanaume huyo amuoe mwanangu Vero,
ukifanikiwa hilo babu nitakupa pesa ndefu sana hutoamini maishani mwako Yani,
maana Mtoto jeuri Sana yule na anamajivuno sana...!,
eti anathubutu kuniambia mimi ni mbaya ndo maana siolewi hadi leo tangu alipofariki baba yake Loooh!".
Mganga akasema," kwahiyo wewe unataka tumfanyeje!?,
tumuondoe kabisa ?, au tumtie utahila au tumnyang'anye mume?!".
Ghafla!, Vero akadakia na kusema ,
" mganga kwakweli mimi binafsi naomba tu umnyang'anye mume tu basi!, wala usimfanye chochote kibaya tafadhari babu!",
Mama Vero naye kama kawaida Yake hana dogo, akamjibu mwanaye kabla ya mganga, ' heee!,
hii dunia ina watoto matahila kweli !, yani jitu tunalipambania, ila mawazo Yake ya kitoto toto tu...!".
Kwa bahati nzuri!, Babu akakubariana na wazo la Vero la kumyang'anya Turi mume, Kisha Babu huyo mganga akatoa dawa iliyoviringishiwa kwenye karatasi nyeupe na kumpatia Mama Vero, na kusema ,
" nisikilize Kwa makini Sana juu ya masharti ya dawa hii, ukikosea tu kila kitu kitakuwa ovyo Sana!,
utamuita Turi aje nyumbani kwako,
kabla ya siku atakayoondoka kwenda mjini na utaiweka dawa hii kwenye maji na utampa anywe na mumewe ataanza kumpenda Vero hapohapo, nadhani tumeelewana ”.
Baada ya Mama Vero kurudi kutoka kwa mganga, kwenye mida ya jioni akampigia Turi kwa bashasha huku akijikosha na kujichekesha kama chizi aliyeona jalala jipya! ,, akasema,"
halooo..!, Turi mwanangu, kuna usia wa Baba Yako aliacha kuhusu mali zako za urithi , maana kama unavyojua Vero yeye ni mwanaye wa kufikia tu, kwahiyo, naomba uje ili ukabidhiwe kila kitu".
Turi naye akajibu kwa furaha tu, akisema" Sawa mama , ngoja nifanye upesi hapa".
Maana,kwa hakika Baba Yake aliacha Mali nyingi Sana ikiwemo ,
viwanja na mashamba pamoja na nyumba ambayo Vero, Turi na mama Yao walikuwa wanaishi wote.
Turi alimuomba mumewe Amani juu ya safari hiyo na Amani hakuleta kipingamizi kabisa maana alikuwa anamuheshimu vizuri tu kama mama mkwe...!,
ITAENDELEA...,
JE WAJUA kwamba unaweza kukamata sms za mwenza wako anazochart na watu wake na ukazipata kupitia simu yako bila yeye kujua
Kwa huduma ya sms tracking ncheki whatsapp 0710204647 nkuunge kwenye group letu.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments