AAAAH IMETOSHA BOSS ππ N0 43ππ
Paschal aliendesha gari hadi nyumbani tuliingia ndani chumbani alifunga mlango si akaanza kunifokeaππ sasa mimi nina makosa gani jamani kosa langu ni kumfumania au kosa langu ni niniπ€·ββοΈπ€·ββοΈ nilinyamaza kimya akafoka wee alivyoona simjibu niko zangu nimekunja nne kitandani na simu yangu naperuzi aliamua kuwa mpole alijistukia.....mwenzie niliamua kuumia kimoyomoyo lakini naona sasa anataka kuzidi huyu nyauba kisa et nampenda ndo anafanya yote hayo kwani anajiamini nini au anajiona yeye peke yake ndo mwenye uwezo wa kunitia ππ mzee wa kufoka alivyoona simjibu alitulia tuli akanifuata pale kitandani et akapiga magoti kuniomba tena msamaha wakati kaishafoka vya kutosha hadi kanitamkia et Lia hawezi kuondoka ofisini ameshakuwa mfanyakazi bora atakupisha tu kwenye ile secta yako atahamia kwenye secta nyingine mara ninachokitafuta kukaa namfuatilia kama mtoto nitakipata hehehee ila hawa wanaume wenye sura nzuri ni mtihani tunawapenda lakini ni maji ya moto hatari dkk zero yanakuunguza.... boo alianza kuniomba msamaha sikumjibu yani nilichokifanya niliplay audio ya yale maneno aliyokuwa anayasema kipindi ananifokeaπππ alf nikawa kimya silii sijanuna na wala sicheki ......
Alijitilisha huruma pale niliamka nikamuacha kule chumbani nikaenda kumhudumia mtoto wangu nimemaliza kumhudumia nice nikashuka chini kwenda kuangalia kama msosi wa usiku tayari..... niliandaa chakula mezani baada ya hapo nilipanda juu kwenda kumwamsha paschal ashuke chini tukale my wenu niliita kwani anaitika sasaπππ kimya kama vile hakunapo mtu hapo chumbani niliamua kusogea hadi pale kitandani nikaenda mtikisa tikisa alijigeuzia upande mwingine akaziba na masikio kabisa nilivyoona kumbe yuko macho ni vile tu yuko na kisirani niliamua kuachana naye nilienda nikapakua chakula changu nikala baada ya hapo nilipakua chakula nikampelekea chumbani nilimpangia vizuri mezani baada ya hapo nilirudia kumwamsha lakini aliamka akahamia kwenye chumba cha wageniπππ akakiacha kile chakula bila kukigusa hivi huyu mzungu mweusi ananijua kweli huyuπ€·ββοΈπ ngoja nikuoneshe kitu paschal naona unajaribu kunichukulia kama grandmother wako π€¨π€¨...
Usiku ule nilimtafuta Mr Hemed yule wa kule zanzibar nilimjulia hali baada ya hapo nilimuomba kikao cha mimi na yeye kuna mambo nilihitaji kuongea naye alikubali tulipanga sehemu tutakayoonana tulipanga kuonana nyumbani kwake...... nililala kesho yake mapema niliamkia kujiandaa kama mtu ninayekwenda ofisini nilimuandaa na mwanangu pamoja na kigari chake nikamweka kwenye gari haoo tukaondoka kuelekea nyumbani kwa Mr Hemed ..... paschal nilimuacha nyumbani bado akiwa amekaa zake sitting na computer yake nilifika nyumbani kwa Hemed alinipokea mimi na mtoto wangu akatukaribisha ndani aliniletea kiywaji baada ya hapo alimbeba nice alinitizama usoni kwangu kisha akaniambia hongera sana unazidi tu kuwa mrembo nilimshukuruππ tuliendelea na maongezi ya hapa na pale baada ya hapo nilimwambia Hemed kile kilichonifanya nimtafute yeye nilitaka anifanyie mpango wa kupata kazi katika ile campuni aliyonitafutiaga kazi kipindi kile..... alismile then akaniambia ucjali sweetheart kazi utapata vipi si utakuja tuishi wote hapa nyumbaniπ₯°π₯° oh no Hemed lakini nitajitahidi kuwa nakutembelea mara kwa maraππ alinipatia ahadi ya kunitafutia kazi kabla hata ya wiki tatu kuisha aliniahidi ya kwamba kazi ni lazima atakuwa ameishaipata...... nilitaka kutafuta kazi sehemu nyingine kwa sababu nisingeweza kufanya kazi na lia katika ofisi moja.....
Siku ile mimi na mtoto wangu tulishinda pale nyumbani kwa Hemed anakaa mwenyewe mwenyewe tu...... kwanini usitafute mtu uishi naye lakiniπ€·ββοΈπ€·ββοΈ nyumba yote hii unawezaje kukaa peke yako?? Nilimuuliza Hemed.... oh pendo hata mimi natamani kuishi na mtu lakini huyo mtu ni vyema ungekuwa wewe hapoππ kiukweli niko mpweke sana yani nikishatoka kazini huwa sina mtu wa kuongea naye hata kupiga story nakaaga mwenyewe tu kuongea hadi nikishafika kazini siipendi hii hali natamani kuwa na mtu na huyo mtu natamani uwe wewe mi nakupenda pendo nakupenda wewe na mtoto wako wote nyie mnaishi kwenye moyo wangu nakuomba usiache kufikilia juu ya upendo wangu kwako ni wewe tu ndo mwanamke ambaye moyo wangu unatamani kuwa karibu na wewe pendo I love youππ Hemed aliniambia hivyo huku akiwa anaipapasa mikono yanguππ anaongea vizuri ana ile rafudhi ya kizanzibarπ tatizo mie msabato yeye muslim lakini mbona kama vile naanza kumuelewa huyu mwarabu jomonπ€·ββοΈπ€·ββοΈ au ni kwa vile moyo wangu umeingia ganzi la maumivu aliyoanza kunipatia boss paschalπ€¨π€¨ Hemed alivyoipapasa mikono yangu nilipata kama kishort fulani hiviππ mvutano wa hisia ulikuwa ni mkali sana kati yetuππ
tuliangaliana machoni huku kila mmoja akiwa anahema kwa hisia lakini ghafla simu yangu iliita alikuwa anapiga paschal sikupokea bado nilikuwa na hasira haiwezekani akosee yeye alf atake mimi ndo nimbembeleze yeyeππ niliamua kuizima ile simu nikaiweka pembeni...... naomba nikuagizie chakula kipenzi niambie kitu utakachopendelea kutumia mida hiiπ«°π..... hapana Hemed mimi nitapika mwenyewe naomba nipike tule then nitakubakizia na chakula cha kutumia usiku...... wow asante my love kiukweli nimemis sana chakula chako kitamu kama ulichokuwaga unakipika kule zanzibar...... hahahaa basi wacha niingie jikoni niandae kwa ajiri yakoπ«°π«° Hemed alichukua maziwa akawa anamnywesha nice huku akiwa anamuimbia nyimbo za kumbembeleza mimi niliingia jikoni nikaenda andaa chakula lakini nilikuwa namchabo Hemed the way anavyombembeleza mtoto wangu kwa mapenzi mazito kama baba yake mzazi alimaliza kumnywesha maziwa akachukua kitowel kisafi akamsafisha baada ya hapo alimlaza kwenye kile kigari chake akaanza kumwendesha taratibu pale sebleni hadi nice akasinzia...... alimbeba akaenda kumlaza na baada ya hapo alikuja jikoni kunisaidia kupika......
Tulipika chakula kikaiva nilipakua mezani tukaketi mimi na Hemed tukala kwa pamoja baada ya hapo nilivisafisha vile vyombo then tulienda zetu kucheza game mimi na Hemed nilijikuta siku nzima nimeimalizia kule nyumbani kwa Hemed jioni mida ya saa 12 tuliondoka pale kwa Hemed kwa ajiri ya kurudi nyumbani mimi pamoja na mwanangu jomon Hemed hakutaka tuondokeππ alibakia mpweke pale tulipokuwa tunaaga kwa ajiri ya kuondoka pale nyumbani kwake alitaka hadi kulia ...... nakumbuka vile ndo nimemkumbatia kumuaga hakutaka nitoke kifuani kwake alinipiga kiss kwenye lips zangu etππ baada ya mimi kupanda kwenye gari aliushika mkono wangu hakutaka niondoke et alirudia tena kuniambia kuwa ananipenda sana....... nilinyamaza japo kuna tuvituvitu nilikuwa natuhisi mwilini kwanguππ niliondoka pale kwa Hemed nikaelekea nyumbani kwangu nilifika nikamkuta paschal yupo nyumbani amefumeππ vile nimefika tu alinifuata pale kwenye gari alimshusha mtoto wake akambeba alinikata jichoπΉπ najali kwani niliipark gari yangu vizuri nikatelemka nilitoa vya kutoa kisha nikafunga vioo na milango kisha nikaanza kutembea mwendo wa kujiachia kuelekea ndani nilitembea kwa pouz ili mtoto wa mama mkwe ajue kuwa yaliyomo yamoππ nilimtikisia na vile siku hiyo nilivaa pigo fulani hiviππ aliniangalia huyoπππ nilikuwa namcheki tu kwenye kioo vile anavyonicheki huko nyuma nilimuacha pale nje na mtoto wake nikaingia ndani nikavua nguo nikaingia bafuni......
Nikiwa kule bafuni nilimsikia paschal anafungua mlango wa chumbani aliingia na mtoto wake mwenyewe alikuwa busy kuongea na mwanae sangapi sasa simu yangu isiiteππ na nilisahau kuiweka silent etππ niliomba tu huyo anayepiga asiwe Hemedππ paschal aliipokea ile simu nikasikia anaongea hello simu ikakatwa kwani alivumilia nimalize kuogaπΉπΉ alinifuata kule kule bafuni pendo huyu Boy ni nani?! Boy ganiππ huyu aliyekupigia alf napokea alivyoisikia sauti yangu amekata ni nani huyu kwa hiyo huyu ndo uliyekuwa naye leo siku nzima?! Hey boo live me alone huoni kama ninaogaβΊοΈβΊοΈ kwani nikiwa naye we unaumia kitu ganiπ€·ββοΈπ€·ββοΈ si ni kama vile tu wewe ulivyo na Liaππ hehehe nyieee sangapi ki iphone changu kisidumbukizwe kule kwenye maji niliyokuwa nayaogaπ€¨π€¨ Boo my phoneπ₯Ήπ₯Ή your phone?! Aliniuliza huku akiwa ananikunjaπ₯Ήπ₯Ή boy ni nani?! I ask you pendo who is boy?!
Itaendeleaaaaaaa
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi