VYOTE NDANI GONGA94
BINAMU WEWE UNGEWEZA? SEHEMU 11 ENDELEA.......
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
"Halooooo! Ebu nipishe mie nisije nikakutapikia hapa"πππππ
Bubu leo kasema na badooo!ππππ.
Bhana weeee Manka hakuamini kama nimempa kichambo cha ukweli. Sura hana, shepu hana, nyota hana, Elimu hana, pesa hana alafu ndo ashindane na mie niliyemzidi kila kitu.
"Yaani unanitukana mimi. Ngoja sasa nikuonyeshe. Alinilukia basi na alivyo na limwili kama tembo basi nilikoma mwenzenu π₯Ή.
Watu walikuwa kutuamulia pale mie nilikuwa hoi, Tumbo lilikuwa linaniuma balaa kwasababu alinikalia Juu ya tumbo langu alafu sasa Manka ni bonge nyie.
Damu zilianza kunitoka huku chini kwa bibi, Sony alifika eneo hilo Manka alijidai anaugulia tumbo.
Sony alimkimbilis mama badala yangu mimi ninayechuruzikwa na damu.
"Baby mwanangu jamani. Nice ameniharibia mimba tumbo linauma sana sijui kama mtoto yupo salama. Niwaishe hospitali mtoto atafia tumboni" Manka aliongea hayo huku analia.
Sony aliniangalia mie pia damu xinanitoka na nipo kwenye hali mbaya sana. Anatakiwa achague mmoja.
"Sony naomba mnisaidie nitakufa" niliongea kwa maumivu makali sana.
Manka Nae alizidi kujilegeza, Sophia yeye alikuwa analia tu. Wafanya kazi wengine walikuwa kwenye simanzi yaani ilikuwa kama vile muv aiseeee!
Sony alichagua kuwa upande wa Manka. Walikokotana mpaka nje ya ofisi huko waliingia kwenye gari alimpeleka Manka Hospitali.
Sikuweza kuhimili maumivu niliyokuwa nayasikia Nilizimia sikujua nini kiliendelea. Nilikuja kushtuka nilijikuta nipo hospitali pembeni yangu alikuwepo mama yangu mzazi.
"Umeamka mwanangu?"
"Mamaaa!" Nilimuita na kuangua kilio.
"Basi binti yangu baaasi inatosha sasa. Nyamaza mama yako nipo hapa"
"Mama mwanangu yupo salama"
"Usijali kila kitu kitakuwa sawa kwasasa unatakiwa kuwa mtulivu sawa binti yangu. Ebu kunywa kwanza huu mtori"
Mama alianza kunilisha mtori. Mlango ulifunguliwa nilishangaa baada ya kumuona Iron.
"Iron!" Nilimuita.
"Yes My lady" huyu mwanaume hana hata aibu ananiita mie my Lady wake mbele ya mama yangu mzazi πππ. Niliona aibu mwenzenu.
"Unaendeleaje?"
"Naona nipo sawa japo sijui usalama wa mtoto wangu"
"Mama naomba nikusaidie kumlisha"
Mama alimkabidhi Iron bakuri la mtori yeye akatoka nje.
"Sijui umejuaje kama nipo hapa. Kwanini ulinitenga kipindi chote hicho. Nateseka mno Iron"
"Nisamehe, Nilipoona kimya nilijua huukuhitaji kutoka Dinner na mimi. Kesho yake nilisafiri nje ya nchi, Jana tu ndio nimelejea Tanzania na kitu cha kwanza kabisa nilitaka kuonana na wewe ila bahati nzuri au mbaya nilikukuta kwenye hali mbaya sana. Pole sana Nice kila pito lina sababu zake"
"Ni kweli. Asante sana kwa kujali. Tangu siku ya kwanza kukuona mpaka leo hii umekuwa ni sehemu kubwa ya kuyaokoa maisha yangu. Asante Iron sina cha kukulia MUNGU atakubariki zaidi.
"Cha kunilipa unacho mama πππ" Iron aliongea kwa utani basi tulifurahi kwa pamoja. Aliendelea kininywesha mtori huku akinipigisha Story za hapa na pale.
"Basi tukiwa tunaendelea na yetu Sony aliingia wodini. Alishtuka baada ya kumuona Iron.
"Onhooooo! Bwana mkubwa kumbe upo hapa" Sony alianza kujichekesha.
"Yes nimekuja kumuona mrembo wangu. Karibu sana"
"Asante. Unaendeleaj Nice?" Sony aliniuliza. Sikumjibu niligeuka pembeni, kiukweli tukio la mwisho lilinifanya nimchukia sana Sony. Ni mwanaume niliyempenda sanaaaa ila ndiye mwanaume niliyewai kumchukia kupita kiasi.
Sony alivyoona simjibu alitoka nje huko alikutana na mama.
"Sitegemei kama utakuja kujitokea tena kwenye maisha ya mwanangu. Mahari yako tutailudisha muda wowote kuanzia sasa.
"Sijui kwanini mlinificha ujauzito wa Nice"
"Ni kweli alikuwa mjamzito na siku aliyopanga kukwambia kuwa ana mimba haukumpa nafasi hiyo zaidi ya kumpiga na kumuumiza, na kila alipotaka kukupa taarifa hizo wewe na Manka mliishia kumuumiza. Alichagua kukaa kimya ili muda uongee ila mipango ya MUNGU haina makosa. Manka ameharibu mimba ya mwenzie. Nimesikitika sana na nimeumia mno ila sina la kuwafanya wewe na Manka acha nimuachie MUNGU. Mama aliongea hayo kwa uchungu mpaka aliliaπ.........ITAENDELEA..........
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi binamu-wewe-ungeweza-sehemu