Mwaka 1977 Ilitoka Filamu Maarufu iliyo kuwa ikizungumzia Maisha ya YESU ,Filamu hii iliitwa “Jesus of Nazaleth” iliigizwa na Raia Wa uingereza Robert Powell.Kuanzia apo Dunia ikaanza kukumbwa na Mtazamo kuwa Sura ya Robert powell ndiyo Sura halisi ya YESU.
Miaka miwili mbele Yaani 1979 ilitengenezwa Filamu nyingine ya Maisha ya YESU .mtu mmoja akachaguliwa kuigiza Filamu hiyo Muingereza aliyeitwa Brian Deacon .Filamu hii iliuza Sana Duniani na Watu wakaamini Sura halisi ya YESU ni Ile waliyoiona kwenye Filamu .
Picha za Robert powell na Brian Deacon waigizaji walioigiza Filamu ya YESU zikaprintiwa na kuuzwa Kwa wingi .karibu na kila nyumba ya Mkristo Duniani Sebule Yake ilipambwa Kwa picha za Brian Deacon na Robert powell .Imani moyoni ilituambia sasa Ile Ni picha ya YESU.
Mbaka makanisa zikatengenezwa sanamu zenye Sura ya Robert powell na Bryan Decon na watu wanaamini kuwa hiyo Ni Sura halisi ya YESU Mwana Wa Mungu . inawezekana kuwa picha Brian Deacon na Robert powell inafanana na Sura halisi ya YESU lakini si kwamba huo ndio muonekano Halisi Wa YESU hivyo Tuweni makini isije siku YESU akarudi tukashindwa kumpokea Kwa Maana tumekalili zile picha za Brian Deacon na Robert powell Kwa kudhani kuwa ndio Mwonekano halisi Wa YESU.
Mwandishi na mwanafalsafa Kutoka uingereza George Bernard show aliwahi kusema “kuweni makini na Elimu yenye upotofu Kwa Maana Ni hatari zaidi kuliko ujinga ”
Hapo zamani Mchoraji mmoja Maarufu kutokea katika falme za Byzantine iliyo kuwa chini ya utawala Wa kirumi Miaka 200 baada ya kifo cha Kristo .aliamua kuchora michoro Kwa jinsi anavyo fikiria Kwa akili zake kuwa YESU alikuwa anaonekanaje.kijana huyo alikuwa ni mfuasi Wa Miungu ya Kigiriki hivyo mchoro huo aliuchora Kwa kuufananisha na muonekano Wa Miungu ya Kigiriki.
Zamani kulikuwapo na Miungu ya Kigiriki ambayo sifa ya mionekano yao ni kuwa na nywele na ndevu ndefu.Miungu hiyo Ni Apollo na Zeus.basi hapo zamani katika falme ya Byzantine iliyo kuwa chini ya utawala Wa Roma , Miaka 200 baada ya kifo cha Yesu kijana mmoja Mwenye stadi ya uchoraji aliyekuwa mfuasi Wa Miungu ya Kigiriki aliamua kuchora picha ya muonekano Wa YESU Kwa jinsi anavyo fikiria.Alimchora kijana Handsome akifananisha muonekano wa YESU.
Inawezekana mchoro huo ulitumika kuipotosha Dunia watu waliamini YESU alikuwa na ndevu ndefu na nywele nyingi .kumbe ulikuwa Ni uongo Wa Yule Mchoraji Wa kirumi Ambaye alimchora YESU na kumfananisha na Miungu Yao ya kirumi ZEUS . inawezekana alifanikiwa Kwa kiasi kikubwa kuudanganya ulimwengu.
Kwa wasomi Wa Dini ya Ukristo wanatambua kuwa zamani watu wa kale walipo kuwa wakiandika na kuchora picha za YESU mapangoni au kwenye makanisa ya zamani wote walimchora YESU akiwa na nywele Fupi .
Ushahidi Wa msingi Wa michoro hii ni ule ushahidi wa watu wa kale walio chora mchoro Wa YESU na kuuweka katika kanisa la Dura europos huko Syria ambapo zamani ilikuwa ni mpakani katika Dola ya kirumi katika karne ya 3.Yesu aliishi katika utawala Wa Dola ya Rumi katika karne ya Kwanza .Dola ya kirumi ndio ilikuwa ikitawala Dunia wakati huo.hivyo watu wengi waliishi katika tamaduni za kirumi.
Itaendelea!.
Karibu Nyasa - Mbamba Bay
Karibu (Ruvuma) Songea.