MAPENZI NI HISIA TAAM SANA epsd 14.
Baada ya muda kufika siku hiyo nilipatwa na uchungu nikapelekwa hospital
Nilifanikiwa kujifungua watoto mapacha wazuri wenye afya ni watoto wakike warembo
Tuliruhusiwa kuludi nyumbani Mama alikuwa msaada kwangu
Mpaka nilimaliza arobaini baba akasema niludi kwangu
Nikaongea na mama kisha mama aliniunga mkono niende dar kumtafuta Chris
Hivyo alinipa kiasi cha pesa kidogo nikaenda na wanangu hadi stendi nikapanda basi hadi dar
Nilipofika nilichukuwa tax hadi nilipokuwa nikikaa bahati mbaya sikumkuta Chris
Niliambiwa aliondoka miezi tisa sasa
Nikaulizia alipo sasa niliambiwa kuwa hawajui hivyo niliondoka na kwenda chuo alichokuwa anasoma
Nikamuulizia wakaniambia tayari anafanya fild hivyo nimsubili amalize
Alitoka fild alinitizama kisha akaniambia kwasasa twende nyumbani kwanza
Alinichukua kwenye gari yake hadi nyumbani kwao nilipokelewa watoto
Nikakaribishwa sebreni kisha Chris alienda kuoga na mimi nililetewa juice pale sebreni
Baada ya muda Chris alitoka akaniambia twende tukazungumze kwenye bustani
Nilimfuata akaniambia haya niambie nini umefuata ukiwa na watoto alafu nimke wa watu wewe
Nilimjibu kuwa kwanza kabisa hawa watoto niwako wewe niliozeshwa nikiwa na mimba ya miezi mitatu tayari
Tangu nimeolewa hadi leo ni miezi saba
Kama utakuwa hujaoa na kama bado nipo moyoni mwako nipo hapa kwaajili yako na wanangu
Chris alistuka alimuita mdada awalete watoto maana hakuwatizama hata
Waliletwa watoto alisogea na kuwatizama vizuri
Kisha akamuita bibiake bibi tafadhari naomba njoo
Bibi alikuja na kumuonyesha watoto na kumuuliza hawa niwetu au
Bibi alipo watizama maramoja tu akajibu niwetu mjukuu wangu hawa wamekufanana wewe mtupu
Chris alipiga kelele za furaha woooo????asante mungu kisha akanigeukua na kunikumbatia
Akaniuliza majina yao nilimjibu sikuwapa mimi majina
Nilikuwa nataka utaje mwenyewe majina kwakuwa niwanao
Chris akasema mpigieni baba ataje majina ya wajukuu zake
Ilipigwa sim na kuwekwa sauti akaambiwa mweshimiwa unawajukuu mapacha wakike hivyo tunangoja utaje majina
Waziri alifurahi sana na kuuliza wanani hao watoto mbona Chris aligoma kuoa kitambo
Walimjibu yule binti aliekuwa anaishinae kule uswahilini
Hivyo Waziri alifurahi kusikia na kuwaambia nakuja sio muda nitatoaajina sawa kwanza waandalieni vizuri
Wakaribishwe na pati hapo nyumbani kwao
Endelea kufuatilia............